Jumuiya ya Kikristo yamtaka Kikwete ataje viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya

1. Kuorodhesha majina
2. Kufuta kauli
3. Kuhalalisha kudharauluka kwake

yeye kashindwa yote matatu anatuletea hoja za kichekechea hapa. (from the bottom of my heart nilitaman rais awataje ili kupambana na hawa wauza misuba kisawasawa.Hapo angekuwa amelisaidia sana kanisa na jamii kiujumla)
 
rais wetu alitoa hotuba ambayo ni targeted kwa walengwa na alidhamiria kuitoa mbele ya kadinali pengo kwani washauri wake feki walishamdanganya kwamba wakristo wakiongozwa na pengo ni wauzaji wa madawa ya kulevya.

Hawezi kuutaja huu upuuzi akiwa kwenye sherehe za iddi el fitiri au maulid. Hapa amekuja kuonyesha jinsi anavyodharau wakristo na asivyokuwa na imani nao. Mtu ametuletea matusi hadi chumbani tumfanyeje sasa kama siyo kumkataa. Kabla hatujamkataa lazima ashinikizwe hata ikibidi kwa wakristo nchi nzima kuandamana hadi amtaje au awataje kwa ushahidi usiokuwa na mashaka maaskofu wote wanaojihusisha na madawa ya kulevya.

Nampongeza askofu mokiwa ameanza na naomba pct, katoliki, lutherani sda nao watoe matamko makali ili rais aelewe kwamba nchi haiongozwi kizembe bali kwa busara.


cum gladiis et fustibus..............................credo in unum deum.
 
washauriwa ni hao wauza unga mnaowatetea!

Vitoto vya shule vinaligeuza jukwaa kuwa la kanisa.

Maaskofu hawana cha kumfanya jk - karata yao ya mwisho ilikuwa uchaguzi na jk hana la kupoteza kwa sasa.

Tulishawaambia maaskofu ni chui wa karatasi, kama wanaweza wajaribu; halafu ndio mtajua jk alishinda uchaguzi au la!

Mso haya mpo jf!

Shame on you mawakala wa chadema na kanisa!

cui bono?????????kikwete amesema viongozi wa dini bila ku-specify kama ni wakristu au waislamu au wapagani.........lakini nadhani amekuwa jasiri kwa kusema hayo baada ya sheikh yaya mlinzi wake kufariki manake alikuwa akiongoza kwa kuuza unga na kuoa vitoto vidogo pale magomeni.....na hata kwenye list yake alikuwemo ndo maana alikosa ujasiri wa kuwalipua...........angepata wapi ulinziiiiiiii? Ushabiki wa kidini hautasaidia kuijenga nchi yetu,manake na sisi (wapagani) tuna madai yetu ya msingi.........siku tukiwasha moto--------mtajuta!
 
kadharau kanisa ,he must name them, yeye ni mkuu wa nchi hatakiwi kuhisihisi kama mtoto wa kike,unles kanisa limsusie asialikwe kwenye mikutano yao na anajipendekeza sana huko church!anafikiri kanisani ni kwenye vikao vya kahawa na soga! In church we are hungry of facts and prøof

Hivi kusimikwa uaskofu wana mualika sheh kua mgeni rasmi wapi na wapi?
sasa kawatukana kwa kuji pendekeza kwao
 

Swala hapa si ubinadamu wa wachungaji wala mashehe!Swala ni kupwaya kwa nafasi ya urais kama taasisi.Hivi yeye akilalamika bila kuchukua hatua wananchi wa kawaida tufanyeje?Mbona kwa babu seya na wanawe hakuwaomba wajirekebishe wenyewe?
 
Rais wetu alitoa hotuba ambayo ni targeted kwa walengwa na alidhamiria kuitoa mbele ya Kadinali Pengo kwani washauri wake feki walishamdanganya kwamba wakristo wakiongozwa na Pengo ni wauzaji wa madawa ya kulevya.

Hawezi kuutaja huu upuuzi akiwa kwenye sherehe za Iddi el fitiri au maulid. Hapa amekuja kuonyesha jinsi anavyodharau wakristo na asivyokuwa na imani nao. Mtu ametuletea matusi hadi chumbani tumfanyeje sasa kama siyo kumkataa. Kabla hatujamkataa lazima ashinikizwe hata ikibidi kwa wakristo nchi nzima kuandamana hadi amtaje au awataje kwa ushahidi usiokuwa na mashaka maaskofu wote wanaojihusisha na madawa ya kulevya.

Nampongeza Askofu Mokiwa ameanza na naomba PCT, Katoliki, Lutherani SDA nao watoe matamko makali ili Rais aelewe kwamba nchi haiongozwi kizembe bali kwa busara.

Duh,kweli huyu jamaa ana dharau,..
inaonekana kaiba mali nyingi,ana taka watu wapigane ili ahame nchi akale hela bila kudaiwa baadae!
 
hivi nyie wote kwenu hakuna mambo ya utani???? :shock: msichukulie kila kitu siriaz :disapointed:
 
Hivi kwanza tuna rais? (ninamaanisha taasisi)

Hapa mm siwezi kunyoosha kidole ili niitendee haki nafsi yangu maana nikinyoosha nitakuwa mnafiki wa kutupwa. Hivi jamani huyu hawezi hata kufikiri kidogo kwamba yeye maneno yake yana nguvu kiasi cha kuinfluence uchunguzi? Kama wapo waliokamatwa na uchunguzi unaendelea alishindwa nini kukaa kimya mpaka ukweli utakapothibitishwa? Kwanini anapenda vibreaking news visivyokuwa na kichwa wala mkia?
 
Nadhnai kwa maneno hayo na JK mnaona jinsi Udini ulivyopamba moto Tanzania. Yaani kila mtu kashikwa na ghadhabu ya ajabu kwa sababu maneno haya yamesemwa mbele ya Maaskofu..Jamani wakuu zangu hawa viongozi wa dini ni binadamu kama sisi na kuwa kwao viongozi wa dini hakujaondoa matamanio hata kidogo. Na pia kumbukeni kwamba JK hakutaja viongozi hao kama ni wa Kikristu na kanisa katoliki isipokuwa UKWELI ni kwamba viongozi wa dini zote nchini wanajihusisha sana na Unga na pia vyombo vinayotumiwa sana kwa money laundry..Haijalishi hawa ni wa dini gani.

Nimeyasoma majibu ya Ikulu ambayo hata imi niliyasubiri sana na nimegundua kwamba hadi sasa wapo viongozi wa dini waliokwisha kamatwa ama wana kesi za kuhusika na vitendo vya kujihusisha na biashara hizo. Sasa maadam wapo kweli viongozi waliokamatwa na wengine bado wanafanyiwa uchunguzi sidhani kama kulikuwa na kosa kwa JK kutahadhalisha chombo hiki muhimu ambacho hakitakiwi kupakwa tope na baadhi ya viongozi walioshindwa na tamaa.

Kuna kipande kimoja ktk majibu hayo kazungumzia kumwambia jirani yako kwamba nyumbani kwake kuna nyoka hivyo hakuna haja ya kuuliza nyoka huyo ni rangi gani au wa aina gani bali nyoka ni nyoka na anahitaji kutafutwa na kufukuzwa au kuuawa... haya maneno yameniganda sana kichwani na kujiuliza tena mbona Yeye JK tunapomwambia kwamba kuna nyoka ndani ya CCM, hakubali kuwepo kwa nyoka bila kumwambia huyo nyoka ni rangi gani na wa aina gani?..

Zaidi ya hapo wananchi wamefikia kumwambia nyoka gani na wa aina gani bado madai yake ni kwamba nyoka huyo hadhuru watu?... kwa ushahidi gani alokuwa nao? aaaah lakini yeye JK anatuuliza tena sisi - Kwa ushahidi gani tuliokuwa nao kwamba nyoka hao wana wana sumu kali ya kudhuru binadamu!..

Msanii msanii tu yaani hata akibanwa pabaya huja na sababu na pengine kweli hata katika hili kazitunga tu sababu.. Mimi nataka Ikulu iwataje hao viongozi wa dini ambao wapo mahakamani, jela au wanachunguzwa kwa biashara za madawa ili tuwafukuze, tuwatenge, na pengine hata tuwaue kabla hawajaleta madhara kwa jamii yetu.
 
Mkandara,

..nadhani tatizo ni kwamba JK has very poor communication skills.

..tatizo siyo ukweli wa maneno aliyoyasema JK, bali ni jinsi alivyowasilisha ujumbe wake.

..halafu mpaka Raisi atoe kauli nzito kama hiyo kwa viongozi wa Dini basi kunapaswa kuwepo hata na reference ya yeye kufanya hivyo.

..kwa mtizamo wangu palipaswa pawepo na Kiongozi mzito wa madhehebu ya Kikristo aliyehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya kuweza kuhalalisha Raisi kutamka maneno yale mbele ya Maaskofu.
 
Mimi nadhani kuna watu wanatumia nafasi zao kufanya biashara ya madawa ya kulevwya. Wapo wanasiasa , wapo vingozi wa dini. Kuna watu wanatumia dini kama kicahaka. Hili tusibishe wakristu kwa wasilam wapo wengi wanaonekana ku mis use status zao za vyeo vya dini.

JK kama iongozi wa ngazi ya Juu hatakiki kutoa tamo ambalo linatolwa na RC, au DC. JK ana uwezo nguvu na wajibu si tu wa kuwataja bali kuhakikisha wanakamatawa kushtakiwa.

La Sivyo naona kila sehemu watanzania tunaweka siasa. mambo ya Usalama Siasa, dini siasa, Michezo siasa. Alafu kwenye siasa ndo imekuwa dini.
 
Sasa wewe unasema nini na Mokiwa kasema nini, JK kasema kuna viongozi wa dini wanajihusisha na madawa ya kulevya Mokiwa anakazia utekelezaji wake sasa yupi unayedai anapotosha anayezungumzia rumours au anayedai utekelezaji.

Huwezi kazia utekelezaji kwa kutoa ULTIMATUM ya masaa 48 kwa kiongozi wa nchi na wewe ukiwa kiongozi wa imani a.k.a usadikikaji. Suala hapa sio kupeana ultimatum ni kusaidiana kufichua uovu ambao upo makanisani na misikitini. Viongozi wa dini walikua na nafasi ya wao kuipokea rai ya Rais na kuifanyia kazi wakati serikali nayo ikiendelea kuzamia katika hili. leo serikali ikiamua kuwataja na kuwaburuza mahakamani viongozi wa dini wadhalimu wafurukutwa wa dini msije anza kulalama.
 
Inashangaza kwamba mkuu wa
nchi ya Tanzania aliwausia
viongozi wa dini zote yaani
dini za Kiislam, Kibaha'i,
Kihindu, Kiyahudi, Kishinto,
Kikristo, Kibudha, n.k, kuacha
kuuza/kununua "BHANGI"
lakini walio react ni wa dini
moja tu, sijui kwa nini ?
 
Back
Top Bottom