Jumuiya ya Kikristo yamtaka Kikwete ataje viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jumuiya ya Kikristo yamtaka Kikwete ataje viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Katavi, Jun 6, 2011.

 1. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Askofu Mokiwa amemtaka rais Kikwete awataje viongozi wa dini kama alivyosema katika hotuba yake huko Mbinga.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sasa hapo ndo JK atajichungulia na kupenda kuropoka ropoka kwake..nimeona walivomkomalia kuwa awataje hao maaskofu wanaouza madawanya kulevya...
   
 3. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,824
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Mbabaishaji sana huyu ****** yaani yeye anarukaruka mara nawajua wauza dawa mara maaskofu wataje na wapeleke kortini anachekacheka tu..
   
 4. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Na asipotaja mokiwa anasema Rais Si mkweli alikurupuka presidah kusema kanisa inahusika na ishu za drugs!inabidi afute kauli yake
   
 5. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Aibu kwa mkuu wa kaya.
   
 6. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Rais wetu alitoa hotuba ambayo ni targeted kwa walengwa na alidhamiria kuitoa mbele ya Kadinali Pengo kwani washauri wake feki walishamdanganya kwamba wakristo wakiongozwa na Pengo ni wauzaji wa madawa ya kulevya.

  Hawezi kuutaja huu upuuzi akiwa kwenye sherehe za Iddi el fitiri au maulid. Hapa amekuja kuonyesha jinsi anavyodharau wakristo na asivyokuwa na imani nao. Mtu ametuletea matusi hadi chumbani tumfanyeje sasa kama siyo kumkataa. Kabla hatujamkataa lazima ashinikizwe hata ikibidi kwa wakristo nchi nzima kuandamana hadi amtaje au awataje kwa ushahidi usiokuwa na mashaka maaskofu wote wanaojihusisha na madawa ya kulevya.

  Nampongeza Askofu Mokiwa ameanza na naomba PCT, Katoliki, Lutherani SDA nao watoe matamko makali ili Rais aelewe kwamba nchi haiongozwi kizembe bali kwa busara.
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani lazima afute kauli yake ..Mokiwa mi nampenda sana yaani mtu wa aina yake angekuwa rais wa nchi hii ingekuwa raha sana...
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi huyu mzee ana washauri kweli au anakurupukaga tu kusema vitu??? sasa atakoma na kuropoka ropoka.yaani rais anakuwa kama katibu tarafa bwana
   
 9. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Kufuta kauli haitoshi kufuta hili tusi alilowatukana viongozi wa Kikristo bali anatakiwa atoe list yenye water tight evidence hadharani. Na akishakutoa ushahidi wake aeleze kwa nini hakuwakamata watuhumiwa na badala yake anaongea ongea ovyo kana kwamba yuko kijiweni anaongea na wacheza ngoma wenzake.

  Hivi huyu hana washauri jamani? Rais wa nchi yenye vichwa zaidi ya mil.42 kiwango chake cha busara kinaposhindwa kukidhi matarajio ya watanzania lazima kuna mahali tulikosea haswa kwenye sanduku la kura.
   
 10. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Nimeisoma habari yenyewe kuhusu JK kusema viongozi wa demi na madawa ya kulevya.

  Inavyoonekana ni kama mtu asiye na uhakika na anachokisema kwa sababu kwenye maelezo yake anawaomba tena viongozi wa demi wawataje wanaohusika na madawa ya kulevya ili hatua zichukuliwe!

  Kwa kweli kunakazi sana. Inabidi ifike sehemu asiruhusiwe kuongea mpaka apate ruhusa kutoka kwa mkapa angalau itasaidia.
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Unajua ni kauli ya udhalilishaji kwa viongozi wa kanisa na waumini wao.kama raisi na ushahidi upo toa order huyo kiongozi akamatwe afikishwe mahakamani.

  Ina maana unawajua drug traffickers halafu unawaacha,au ni muendelezo wa EPA cinema kuwa watuhumiwa warudishe walichoiba? Mbona kila siku tunasikia watu wamekamatwa na hizo pipi lakini hatujaskia hao unaowajua wakikamatwa, pls do the needful for the sake of poor tanzanians who are becoming addicted and chronic to drugs..pls pls
   
 12. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,846
  Likes Received: 626
  Trophy Points: 280
  Hivi kama mkuu wa kaya na ananzo nyenzo zote plus resources zote under the sun za kuwakamata maaskofu wauza wauza unga si awakamate tu( maana tayari anawajua na tayari wamekomiti serious crimes). Kuna haja gani kuwatahadharisha? Ili wasikamatwe au anataka kutuambia nini?
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Haya ndio aliyoyaeleza, kipi kibaya hapa?:

  Tuesday, May 31, 2011

  VIONGOZI WA DINI NA TAASISI SAIDIENI SERIKALI KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA - JAKAYA KIKWETE


  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete, ametangaza kuwa ataunda chombo maalum cha kupambana na ongezeko kubwa la tatizo kubwa la biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

  Aidha, Rais Kikwete amewaomba viongozi wa dini na taasisi za dini nchini kusaidiana na Serikali katika kupambana na tatizo hilo lenye madhara makubwa kwa jamii, na hasa miongoni mwa vijana ambao wanaunda asilimia 60 hadi 80 ya Watanzania wanaotumia dawa za kulevya ambazo zinaharibu mwili na akili ya mtumiaji.


  Vile vile, Rais amesema kuwa wakati ni kweli kuwa mikoa yote ya Tanzania inakabiliwa na tatizo hilo, lakini ni mikoa saba inayoongoza kwa kuwa na tatizo kubwa zaidi ikiwa ni Dar es Salaam, Mwanza, Mjini Magharibi – Zanzibar, Arusha, Tanga, Mbeya na Dodoma.

  Rais Kikwete alitangaza kusudio lake la kuunda chombo maalum cha kupambana na dawa za kulevya jana wakati wa sherehe za kusimikwa kwa Askofu Mteule Albert Jella Randa wa Kanisa la Mennonite, Tanzania, kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mwanza ambako alikuwa mgeni.


  Sherehe hizo zilifanyika kwenye makao ya Dayosisi hiyo Nyakato, mjini Mwanza.


  Akihutubia mamia ya waumini wa Kanisa hilo pamoja na wananchi wengine waliohudhuria sherehe hizo, Rais Kikwete amewaomba viongozi wa dini, madhehebu ya dini mbali mbali nchini kuongeza juhudi za kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.


  Akisema kuwa pamoja na kwamba matunda ya juhudi za Serikali katika kupambana na tatizo hilo yameanza kuonekana bado kazi iliyoko mbele ya jamii ya Tanzania ni “kubwa sana”.


  “Mwaka jana, 2010, watu 12,119 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Katika kipindi hicho, dawa za kulevya zilizokamatwa ni heroine kilo 190 na gramu 780, cocaine kilo 65, morphine kilo 11, bangi kilo 279,520 na mirungi kilo 10,317. Takwimu zinaonyesha kuwa mkoani Mwanza tatizo linakua kwa kasi sana,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:


  “Dawa za kulevya zina madhara makubwa kwa watumiaji na kwa jamii. Kwa watumiaji hatima yake ni mtu kuharibikiwa kimwili na kiakili. Watu huwa mazezeta na hivyo kushindwa kutokuwa na manufaa kwa jamii. Hii ni hasara kwa familia, jamii na taifa. Bahati mbaya sana waathirika wengi ni vijana. Tafiti zilizopo zinaonyesha kwamba asilimia 60-80 ya watu wanaotumia dawa hizo ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 30, alisema.”


  Aliongeza: “Hii ni hasara kubwa kwani vijana ndio nguvukazi ya leo na kesho. Ndiyo roho ya taifa na warithi wa familia, jamii na taifa. Wakiharibikiwa taifa letu litaangamia. Tusikubali. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kulichukia tatizo hili na kulikemea kwa nguvu zake zote ili kuokoa taifa letu. Nawaomba viongozi wa dini kushirikiana na Serikali na watu wote wenye mapenzi wa nchi yetu kupambana mpaka tufanikiwe kudhibiti na hatimaye kulitokomeza tatizo hili.”


  Sherehe za leo za kusimikwa Askofu Randa (50) kuwa Askofu wa Kanisa Mennonite, Jimbo la Mwanza, pia zilihudhuriwa na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa hilo na wananchi wengine.


  Kwenye sherehe hizo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), Mhashamu Severin Watson Mang’ana amemkabidhi askofu huyo mpya nguvu kuu ishara za mamlaka na madaraka ya uaskofu ikiwamo Biblia, Katiba ya KMT, Cheti cha Uaskofu na vitabu vya taratibu ya kuendesha ibada za Kanisa hilo na nyimbo.

  Kanisa la Mennonite lililoanzishwa duniani mwaka 525 na Mchungaji Menno Simon mjini Zurich, Uswisi, liliingia nchini miaka 77 iliyopita mwaka 1934 na liko katika maeneo yote ya Tanzania isipokuwa Zanzibar, Ruvuma na Pwani. Kanisa hilo lina makao yake mkoani Mara.

  Source: Maganga One.: VIONGOZI WA DINI NA TAASISI SAIDIENI SERIKALI KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA - JAKAYA KIKWETE
   
 14. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh mimi ni silent observer. Wote hapo juu mmeongea vitu vizito (kasoro FF) na nakubaliana na hoja zenu wakuu
   
 15. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni baada ya kuwaonya viongozi wa madhebu mbalimbali ya dini hapa nchini kuacha tabia ya kushiriki kuuza madawa ya kulevya! Wanasema awataje wanaojihusisha na kuuza madawa ..'ASIOGOPE'!!

  Huyo ndo JK ..bingwa wa kufulia!!

  Source: ITV news!!
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kusema huko nyuma nadhani hata wanaJf wengi wamelisemea hili - tena kwa nia njema kabisa, kwamba Magogoni kuna upungufu mkubwa kwenye safu wa washauri. Inawezekana kabisa kuwa Kikwete ni mtu wa kuangalia vyeti kwa hiyo mtu akija na list ya vyeti yeye anailainika. Si uchumi, si siasa, mambo ni shagalabagala. Ni hii inaenda hata kwa watoto wake hasa huyu aliyeko UVCCM na Mama na WAMA yake. waangalie hili maana hawezi kushindana na maaskofu. These people are not your average leaders. wamekwenda shule, wanasoma falsafa na wako karibu na jamii. wrong enemy!

  Na kama Taifa hatutafaidi chochote kwa ofisi ya rais -kama taasisi kuwa na mgororo na viongozi wa madhehebu ya dini. (iwe waislama au wakristo). Mbaya zaidi Kikwete anataka kulumbuna na wakristo ambao ndio wanaongoza kutoa huduma za jamii baada ya serikali kulegea? shule, hospitali, maji!
   
 17. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Tukiwaambieni Jakaya Mrisho Kikwete Mdini watu humu jamvini mnaona kama tunamwonea,this fool has ****ed this country and now is looking for a scapegoat na kwa akili yake ndogo anafikiri atawasaidi au kuwavutia Waislam kwa kuwabagua Wakristo anajilisha upepo sababu Waislam na Wakristo wa leo hawawezi pumbazwa na siasa muflisi za kiongozi aliyechoka kiafya na kiakili kama yeye ambaye hata hajui kwanini aliutaka urais wala hajui kwanini nchi na wananchi wake ni maskini.
   
 18. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  kadharau kanisa ,he must name them, yeye ni mkuu wa nchi hatakiwi kuhisihisi kama mtoto wa kike,unles kanisa limsusie asialikwe kwenye mikutano yao na anajipendekeza sana huko church!anafikiri kanisani ni kwenye vikao vya kahawa na soga! In church we are hungry of facts and prøof
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
 20. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Swadaktaaaa!! Taja mheshimiwa hata kama ni Sheikh, Padri, Askofu,kadhi,maalim,ustaadh,alhaj imam,walii,towashi,mtawa,mwinjilisti,katekista,bradha, sista etc sisi tutakuunga mkono hatutaki biashara hii kharamu nchini kwetu!

  Nategemea mkuu wangu utawataja wiki hii bila kificho kwani unawajua, vunja ukimya!
   
Loading...