Jumuiya ya Kikristo Nchini yatoa wito wa Serikali kutoingilia Mahakama

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Ikitoa maoni kwa Tume ya Haki Jinai katikakuboresha mfumo wa Haki nchini, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), imeshauri maeneo manne yanayohusisha mfumo wa huduma za magereza, utendaji wa Jeshi la Polisi na mhimili wa mahakama chini ya msingi wa biblia, kitabu cha Isaya sura ya 32:17-18 kinachoelekeza habari ya kutenda haki ili amani na utulivu vitawale katika jamii.

CCT inayounganisha makanisa 12 na taasisi 14 zinazoendesha huduma mbalimbali za kiroho, ilishauri kuweka misingi itakayoweka huru mhimili wa mahakama.

Askofu Nelson Makori, mwenyekiti wa Kamati ya Sera, Fedha na Programu wa CCT alisema, “tunataka tuone mahakama ikiwa huru kwa asilimia 100 bila kuingiliwa na chombo chochote, itoe haki bila kupendelea, sawa na sheria za nchi.

“Kwa hiyo kuna mapendekezo kuhakikisha mahakama haiingiliwi na chombo chochote, mtu yeyote,” alisema.

“Pili, mahabusu walindwe, hawajahukumiwa. Sasa wanataabika, wanarundikana huko, maisha ya kibinadamu hayapo na inadhalilisha utu wao, kwa hiyo tumeshauri kushughulikia hilo,” alisema Askofu Makori.

Mengine yaliyomo kwenye mapendekezo yao ni pamoja na kuboreshwa kwa mfumo wa mafunzo utakaosaidia mfungwa kurekebishika tabia na kuweka misingi itakayowezesha Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yao kisheria badala ya kusikiliza maelekezo ya watu wengine.

Chanzo: Mwananchi
 
Ndio maana tunasisitiza tupate katiba mpya. Kama wakuu wa hivyo vyombo vya haki wataendelea kupatikana kwa kuteuliwa na raisi, hakuna kitakacho badilika. Hiyo tume ni kama inatafuna kodi zetu bure tu.
 
Ikitoa maoni kwa Tume ya Haki Jinai katikakuboresha mfumo wa Haki nchini, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), imeshauri maeneo manne yanayohusisha mfumo wa huduma za magereza, utendaji wa Jeshi la Polisi na mhimili wa mahakama chini ya msingi wa biblia, kitabu cha Isaya sura ya 32:17-18 kinachoelekeza habari ya kutenda haki ili amani na utulivu vitawale katika jamii.

CCT inayounganisha makanisa 12 na taasisi 14 zinazoendesha huduma mbalimbali za kiroho, ilishauri kuweka misingi itakayoweka huru mhimili wa mahakama.

Askofu Nelson Makori, mwenyekiti wa Kamati ya Sera, Fedha na Programu wa CCT alisema, “tunataka tuone mahakama ikiwa huru kwa asilimia 100 bila kuingiliwa na chombo chochote, itoe haki bila kupendelea, sawa na sheria za nchi.

“Kwa hiyo kuna mapendekezo kuhakikisha mahakama haiingiliwi na chombo chochote, mtu yeyote,” alisema.

“Pili, mahabusu walindwe, hawajahukumiwa. Sasa wanataabika, wanarundikana huko, maisha ya kibinadamu hayapo na inadhalilisha utu wao, kwa hiyo tumeshauri kushughulikia hilo,” alisema Askofu Makori.

Mengine yaliyomo kwenye mapendekezo yao ni pamoja na kuboreshwa kwa mfumo wa mafunzo utakaosaidia mfungwa kurekebishika tabia na kuweka misingi itakayowezesha Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yao kisheria badala ya kusikiliza maelekezo ya watu wengine.

Chanzo: Mwananchi
Wateule wa mahakama ngazi za juu hupangwa na nani tuanzie hapo?
 
Vizuri. Kwa kusema hivyo ina maana Yule Mwamba wa Kesi ya Ugaidi angeachwa tu aendelee na Kesi aprove u innocent wake.
 
Back
Top Bottom