Jumuiya ya Afrika Mashariki yasaini mkataba wa Mamilioni na Umoja wa nchi za Ulaya

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)imesaini mkataba wa EURO milioni 10 na umoja wa nchi za Ulaya kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi uanachama wa jumuiya hiyo.

Mkataba huo umesainiwa mapema leo katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo na Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki ,Liberat Mfumukeko na Balozi wa umoja wa nchi za Ulaya nchini Tanzania, Manfredo Fanti.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo ,Katibu mkuu wa EAC ,amesema kuwa, fedha hizo zimetolewa na jumuiya ya umoja huo ili kuziwezesha nchi wanachama kukabiliana na changamoto ya usalama ambayo imekuwa na kikwazo katika maendeleo katika nchi hizo.

Mfumukeko ameshukuru jumuiya hiyo ya umoja wa ulaya kwa msaada huo ambao umekuja muda muafaka na kuongeza kuwa, jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana kwa ukaribu Sana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Hata hivyo ,Mfumukeko amesema kuwa,jumuiya hiyo ya nchi za Ulaya wamekuwa washirikiana kwa muda mrefu na jumuiya hiyo ambapo katika kipindi cha miaka mitano wamekwisha kutoa kiasi Cha EURO milioni 85 .

Kwa upande wake, Balozi wa jumuiya ya umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Manfredo Fanti amesema kuwa, wataendelea kusaidia jumuiya hiyo katika maswala mbalimbali ya maendeleo .

"Tumekuwa tukisaidia jumuiya ya Afrika Mashariki katika miradi mbalimbali tangu mwaka 2007 ambayo imeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo na kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili."amesema Balozi huyo.


Ends


IMG-20191128-WA0005.jpeg
IMG-20191128-WA0003.jpeg
 
Hizo pesa ni sawa na na MTU mwenye milioni 100 halafu akakutana na ombaomba mtaani kisha akaamua kumpa ombaomba buku moja (1,000/=)!!
Kiukweli msaada wa buku Kwa ombaomba kutoka Kwa MTU mwenye milioni 100 ni matusi ya hadharani!!!!
Tufike mahala tuamue kulinda heshima yetu!! Euro milioni 10 kila mwanachama anaambulia chini ya euro milioni 2 halafu mtoa msaada anayemiliki matrilioni ya euro anategemea kuambiwa asante!!! No way!!
 
Back
Top Bottom