Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imekanusha kuwa na ukata wa fedha na kwamba nchi zote wanachama, zimeanza kulipa ada za uanachama

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,812
4,533
Jumuiya hiyo imesema hakuna nchi yoyote ya Jumuiya hiyo iliyo hatarini kuondolewa uanachama, kwa sababu ya kushindwa kutoa ada za mwaka, isipokuwa upo uwezekano wa kuwekewa vikwazo.

Kwa mujibu wa taarifa ya jumuiya hiyo, hadi kufikia Oktoba mwaka huu, Burundi ilikuwa ikidaiwa Dola za Marekani milioni 13, Tanzania Dola za Marekani milioni tisa, Kenya Dola za Marekani milioni nane, Rwanda Dola za Marekani milioni saba na Uganda Dola za Marekani milioni mbili.

Naibu Katibu Mkuu wa EAC, Steven Mlote, akizungumza na HabariLeo Afrika Mashariki juzi, alisema nchi zote sita wanachama wa jumuiya hiyo, zimetoa michango yao kwa kiwango cha kuridhisha.

Alisema kati ya nchi hizo, Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Sudan Kusini zimetoa michango yao ipasavyo, lakini tathimini kamili kwa mujibu wa sheria itafanyika mwezi ujao kwa mujibu wa taratibu.

“Hivi karibuni kulikuwa na maneno kuhusu baadhi ya nchi kudaiwa kutotoa michango ipasavyo, lakini suala hilo lilibebwa kishabiki zaidi, kwani ndiyo kwanza ilikuwa mwezi Julai na hakukuwa na jukumu la EAC lililokwama kwa sababu ya kutokuwa na fedha.

“Sheria iliyounda jumuiya inabainisha kuwa iwapo nchi mwanachama haijalipa mchango kwa miezi 18 inatakiwa kuwekewa vikwazo kwa mujibu wa viongozi watakavyoona, kama vile kutohudhuria vikao, lakini siyo kuiondoa kwenye jumuiya,” alisema.

Mlote alisema kwa sasa hakuna changamoto ya uhaba wa fedha, kwani fedha zipo. Kuhusu vikao vya Bunge la Afrika Mashariki (EALA), alisema hakuna kikwazo cha fedha na kwamba vikao hivyo vinafanyika kutokana na mipango ya jumuiya kulingana na mtiririko wa fedha.

Mwezi uliopita Bunge hilo lililitaka Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuchukua hatua kali, ikiwamo kuziwekea vikwazo nchi wanachama zisizotimiza wajibu wake wa kutoa mchango wa fedha, kama katiba ya jumuiya hiyo inavyotaka. Bunge hilo lilitaka baraza hilo la mawaziri, kuelezea changamoto ya uhaba wa fedha, unaoikabili sekretarieti ya jumuiya hiyo na kuzihimiza nchi wanachama kutoa michango yao.

Sudan Kusini ilipewa hadi mwisho wa Oktoba mwaka huu, kuwasilisha malimbikizo ya michango yake ya Dola za Marekani milioni 27 na ndiyo sababu ya kupunguza dola milioni tatu. Mjadala huo umefanyika baada ya hivi karibuni Jukwaa la Asasi za Kiraia katika Afrika Mashariki (EACSOF), kutaka kufungua shauri katika mahakama ya jumuiya hiyo, kutaka ufafanuzi wa kisheria kuhusu uhalali wa wanachama wasiolipa ada zao kuendelea na uanachama.

Hivi karibuni ilielezwa kuwa baadhi ya wabunge wa EALA, walipaza sauti zao katika mkutano wa bunge hilo,kulalamikia Sudan Kusini na kutaka iondolewe kwenye jumuiya kutokana na kushindwa kulipa ada ya uanachama. Nchi hiyo iliyopata uhuru wake Julai 2011, ilijiunga na jumuiya hiyo mwaka 2016, inadaiwa haijalipa ipasavyo ada ya uanachama inayotakiwa kila mwaka.

Katibu wa Wizara Viwanda na Biashara wa Sudan Kusini, Mou Mou, amethibitisha kulipwa kwa fedha hizo kupitia wizara ya fedha na uchumi bila kubainisha fedha zilizobaki zitalipwa lini.

Katibu Mkuu wa EAC, Libérat Mfumukeko, alithibitisha kupokewa kwa fedha hizo . Athian alisema limebaki deni la Dola za Marekani milioni 24, lakini hajajua utaratibu wa kumalizia kwa sasa, kwani wizara ya fedha na mipango ya nchi hiyo ndiyo inayoweka mikakati ya kukamilisha kulipa.

Burundi ilisema mwezi uliopita kuwa imedhamiria kulipa madeni inayodaiwa na jumuiya kwa kuanza na Dola za Marekani milioni 1.7. Mpaka Juni mwaka huu nchi hiyo ilikuwa imelipa Dola za Marekani 408,548, ikiwa ni ada ya uanachama sawa na asilimia tano ya ada inayotakiwa kulipa.

Waziri wa EAC wa Burundi, Isabelle Ndahayo, alisema bado wanatakiwa kulipa asilimia mbili ya malimbikizo ili kuanza kulipa mwaka huu wa fedha.
 
Hii ni habari njema na hutokea hata kwenye familia zetu, baba anashinda bar halafu watoto wanaamkia chai kavu ya rangi.

Siri ikifichuka kwa baba anaokunywa nao, lazima atanunua mikate na kupiga nayo selfie atakavyopokelewa na nyumbani na kusema mkate haujawahi kukosekana nyumbani.
P
 
Back
Top Bottom