Jumong ndiye muanzilishi wa himaya ya Goguryeo

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Habari zenu wakuu.

Kabla ya kufanya research kama kuna kitu kilikuwa kinanichanganya wakati naangalia series za Korea ni hizi kingdoms.

Unakuta series hii wameigiza kipindi cha GORYEO , nyingine GOGURYEO hujakaa vizuri kuna series nyingine imeigiziwa JOSEON

Sasa nikawa napata mkanganyiko which is which na kwanini zina majina tofauti , leo naomba tuwe pamoja ili tuweze kuelewa Goryeo na Joseon zina utofauti gani ili unapoangalia series kali za kikorea uweze uweze kuelewa.

Sasa huwezi ukazungumzia Goryeo na Joseon bila kuongelea nchi ya Goguryeo maana hiyo ndio kama Taifa mama. Kabla ya Goryeo na Joseon kuwepo kulikuwa na taifa la Goguryeo.

Kimpangilio inaanza himaya ya Goguryeo ambayo ilianza mwaka 37 B.C na kuishia 668 AD.

JUMONG ndiye muanzilishi wa himaya ya Goguryeo, hivyo basi ile series ya JUMONG iliyokuwa inaoneshwa ITV inaelezea kinaga ubaga jinsi ambavyo Goguryeo ilianza.

Baada ya Goguryeo kuanguka ikaingia himaya nyingine Ya GORYEO. Hili neno Korea linalotumika sasa hivi limetokana na neno hilo linalotamkwa "Koryeo".

Goryeo ilianzishwa na mfalme Taejo. Na kiukweli tu Goryeo ilikua sana hasa kijeshi na kiuchumi lakini kutokana na udhaifu wa viongozi wa ndani ya nchi ya mwaka 1392 GENERAL YI SEONGGYE alimpindua mfalme GONGYANG na yeye akawa mfalme. Huo ukawa ni mwisho wa Goguryeo.

Baada ya kuwa mfalme General Yi Seonggye kumpindua Gongyang na yeye kuwa mfalme alitaka kuanza Upya. Hivyo basi alibadilisha viongozi karibu wote kwenye serikali, akaweka sheria mpya na hata jina la himaya AKAIBADILISHA badala ya Goryeo nchi akaipa Jina La JOSEON. Hii ilikuwa ni mwaka 1392.

Ukiangalia series ya SIX FLYING DRAGONS au ile DEEP ROOTED TREE ya mwaka 2011 zinaongelea jinsi ambavyo GORYEO ILIBADILIKA IKAWA JOSEON.

Kwa hiyo kimpangilio Ukiangalia series za kikorea usije kuchanganya tena kimpangilio inaanza

GOGURYEO >>>>> GORYEO >>>> JOSEON

Of course pia ukiangalia series kama
QUEEN SEONDEOK kuna falme kama SILLA au kama umeona series kama THE KINGDOM OF THE WINDS kuna BUYEO na BAEKJE zote hizi ni kingdoms za kipindi hicho huko Korea.

Hivyo kulingana na story ilivyo directors wanamuu stori itaigiziwa kipindi gani aidha kioindi cha Joseon, Goryeo au Goguryeo. Inategemea na Stori au matakwa ya director.

Nilitaka niweke hapa kwa undani utofauti wa hizi kingdoms lakini nimeona uzi utakuwa mrefu zaidi.
Naomba niishie hapa.

Wasalaaam!
jumong-1.jpg
maxresdefault.jpg
1391656-0-q80.jpg
45875.jpg
Screenshot_20210506-162514.jpg
10012019_seoulbeats_rookiehistoriangoohaeryung_0.jpg
 
Shukrani kwa maelezo mazuri. Nami niongezee machache!

Kumbukumbu za kihistoria zinautaja Ufalme wa Joseon mara mbili. Yaani palikuwa na Falme mbili za Joseon katika nyakati mbili tofauti. Kabla ya Joseon ya Taejo palikuwa na Joseon nyingine kabla ya Falme Tatu (Three Kingdoms). Hiyo Joseon nyingine inafahamika kwa jina la "Gojoseon" ama "Joseon ya kale".

Pia palikuwa na Ufalme mwingine maarufu uliofahamika kama Buyeo ambao mwanzilishi wake anatajwa kwa jina la Hae Mo-su. Huyu jamaa ni maarufu sana sababu ndiye baba mzazi wa Jumong wa Goguryeo. Huu Ufalme ya Buyeo ulitokana na "Joseon ya kale" niliyoitaja awali, almaarufu Gojoseon.
 
Shukrani kwa maelezo mazuri. Nami niongezee machache!

Kumbukumbu za kihistoria zinautaja Ufalme wa Joseon mara mbili. Yaani palikuwa na Falme mbili za Joseon katika nyakati mbili tofauti. Kabla ya Joseon ya Taejo palikuwa na Joseon nyingine kabla ya Falme Tatu (Three Kingdoms). Hiyo Joseon nyingine inafahamika kwa jina la "Gojoseon" ama "Joseon ya kale".

Pia palikuwa na Ufalme mwingine maarufu uliofahamika kama Buyeo ambao mwanzilishi wake anatajwa kwa jina la Hae Mo-su. Huyu jamaa ni maarufu sana sababu ndiye baba mzazi wa Jumong wa Goguryeo. Huu Ufalme ya Buyeo ulitokana na "Joseon ya kale" niliyoitaja awali, almaarufu Gojoseon.
Big up Boss KWA kujazia nyama
 
Nilisikia kutengana kwa Buyeo na Gugureyo ndo maana tuna North korea na South korea kwamba ni kitambo tu hawapatani
 
Write your reply...kumbe mo pol no ana mchango mkubwa Ku establish state,mzee mfua vyuma,mapanga take yalikua hatari.iron smith
 
ila six flying dragons ilikua ni fire.Pambano la yule dogo muyoul ( cjui ndo linaandikwa hvyo 😳 ) na yule pacha alie bakia gilisomi, lilikua pambano hatar sana.
 
Back
Top Bottom