Jumba la Makumbusho ya Kasri la Kifalme la Hong Kong kufunguliwa mwezi Julai

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
VCG111384852857.jpg

Mei 29, 2022, Jumba la Makumbusho ya Kasri la Kifalme la Hong Kong

Jumba la Makumbusho ya Kasri la Kifalme la Hong Kong lililoko magharibi mwa wilaya ya kitamaduni ya Kowloon Magharibi, litafunguliwa mwezi Julai mwaka huu na kuonyesha vitu vya kale kutoka kwa Jumba la Makumbusho ya Kasri la Kifalme la Beijing na kote duniani.

Jumba hilo lililoanza kujengwa mwaka 2018 na kumalizika mwaka huu, litaonyesha vitu vya kale vinavyohifadhiwa katika Jumba la Makumbusho ya Kasri la Kifalme la Beijing, ambavyo vingi vitaoneshwa hadharani kwa mara ya kwanza mkoani Hong Kong. Jumba hilo pia huandaa mara kwa mara maonyesho maalum kuhusu utamaduni na sanaa ya China, pamoja na hazina za sanaa kutoka duniani kote.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom