Jumba hili kwenye eneo la ATC ni la nani? - Picha

Kama connection hiyo ni ya kweli,najiuliza huyu jamaa katulisha nini hata tunamshindwa ilihali katika kila aina ya ufisadi yumo au ana mahusiano nao? mwenye jibu anisaidie maana mie nahisi nimechanganyikiwa

Jamani mpaka sasa ni tuhuma na fununu na wala si uhakika kwamba hilo hekalu ni la RA, kwanini atupiwe lawama, laana na kejeli?.

Tutafute ukweli kwanza kabla ya kuanza kulaumu.

Na jambo lingine jaribuni kuelewa kwamba hata kama RA alifanya ufisadi huko siku za nyuma ukweli ni kwamba haukuufanya peke yake bali ni kundi kubwa la watu lilihusika na pasipo kushikiwa bunduki wala visu. Waliongea na kuelewana na kuamua kufanya waliyoyafanya. Kwanini alaumiwe yeye tu kwa kila jambo?.
 
wadau hii mbona ni kawaida na huwa inakuwaga kweli mara nyingi wizi unapotokea mtaani/kijijini anayeshukiwa kuhusika mara nyingi ni mwizi wa hapo mtaani/kijijini...na huwa asilimia kubwa hizo shutuma huwa za kweli!! so ra hahitaji huruma yetu (at least yangu)!!
 
Kidatu... hata wewe una uhakika kuwa yule mwizi sugu ameshafanya vitu vyake... Ona ulivyojieleza...
Na jambo lingine jaribuni kuelewa kwamba hata kama RA alifanya ufisadi huko siku za nyuma ukweli ni kwamba haukuufanya peke yake bali ni kundi kubwa la watu lilihusika na pasipo kushikiwa bunduki wala visu. Waliongea na kuelewana na kuamua kufanya waliyoyafanya. Kwanini alaumiwe yeye tu kwa kila jambo?.
Lakini kwa sababu unazozijua umeamua kumtetea...
Jamani mpaka sasa ni tuhuma na fununu na wala si uhakika kwamba hilo hekalu ni la RA, kwanini atupiwe lawama, laana na kejeli?.
Tutafute ukweli kwanza kabla ya kuanza kulaumu.
 
ndugu mambo mengine mungu anafanya makusudi watu wamrudie
sasa kwa kuwa wewe umeonyeshwa hiyo nusurobo ya uvamizi ujue kuna mambo mengi makubwa yanachezwa
kwenye wizara na yanabarikiwa na uongozi wa juu;;hapoo nina uhakika hata ukifeatili utamkuta na hati kamili
mpaka saini ya mwenyekiti wa serikali za mitaa...ni wakati wako ama wetu kusali kurudisha mali za nchi yetu zilizoporwa enzi za
RAIS MWINYI;MKAPA;NA HUYU KIKWETE';usiache kuwataja majina kabisa hawa maraisi .....Tunaitaji kurudishiwa mali zetu
hata kama wamechukua mafisadi tunayo haki ya kudai kwenye ulimwengu wa ROHO si leo basi kesho AIBU Itawakuta na
T/did watatuletea wenyewe mikononi wakilia....usikate tamaa wala wasikukatishe tamaaaaa
 
HIYO NI SAINI YA KUONYESHWA NCHI IMEPORWA
NILISHASEMA IKIFKA MIAKA 20 IJAYO AMBAYO MAKAMPUNI MENGI WAKISHIRIKIANA NA RAIS MKAPA
WAMEPEWA MKATABA WA MIAKA 30/20 WATTOTO WATAKAOZALIWA WATAKUTA MASHIMO YAMEJAA
INZI MULE NDANI....SO TUNAITAJI KUOMBA MUNGU ATA MIAKA WAKIMALIZA MKATABA WAO TUYAKUTE
HAYO MADINI;;HII SHERIA ILIOPITISHWA NI UCHAFU WASERIKALI KUONYESHA WAMEKASIRISHWA NA UVAMIZI BAADA YA MUNGU KUQinua watu lakini nakuakikishia MIKATABA MINGI YA MADINI NA BANDARINI IKIWAMO TICTS INA ZAIDI YA MIAKA 30 SO HUU MSWADA UTAWAKUTA
HATA HAWA WANAOPITISHA WOTE WAMEJAZANA PALE KINONDONI CEMENTRY

mungu azdi kuwafungua watanzania tujue jinsi ya kudai mali zetu!!11
 
Kidatu... hata wewe una uhakika kuwa yule mwizi sugu ameshafanya vitu vyake... Ona ulivyojieleza...

Lakini kwa sababu unazozijua umeamua kumtetea...

Nilichotaka ukielewe ni kwamba tuache kumtupia kila lawama RA kwa kila chafu litendwalo hapa Tanzania. Hilo jumba huenda si la kwake na hata kama ni la kwake basi atakuwa na vibali vyote vinavyotakiwa. Sasa kwanini kumtupia lawama RA ambaye hatoi vibali husika?. Kwanini kumlaumu RA katika suala la EPA wakati yeye hakuwa waziri wa fedha, Gavana ama mfanyakazi wa BOT?. Je alitumia bunduki (jambazi) kuchukua pesa za EPA ndani ya BOT?.

Jamani twende mbele lakini tuangalie nyuma ili kupata ukweli wa umbali tuliofikia, hakuna sababu ya kumlaumu RA bali tuwalaumu watendaji tuliowapa madaraka na ofisi, hawa ndiyo sababu na chanzo cha machafu yote. Tusiwe wanafiki na wapiga kelele bila kufikiri, chukua nafasi ya RA uwe ni wewe na dili zinakujia kwa njia ya halali utakataa pesa?. Maana RA si jambazi hakuvunja milango ya BOT kuchukua pesa za EPA bali alilipwa baada ya maidhinisho yote kufanywa na wahusika. Hakuleta Richmond kinguvu na kuwashikia Tanesco bunduki ili wamlipe mamilioni kila siku, bali ni makubaliano halali ya kibiashara kati yake na Tanesco. Sasa kwanini leo atupiwe lawama, laana na kejeli?.
 
Mkuu Kidatu,

I am sorry but are you out of your senses? Kwamba kwa kuwa mtu akutumia bunduki kuiba basi huyo ni halali yake kuachwa aendelee kupeta? Kwamba anayestahili kuitwa mwizi ni huyo anayetumia bunduki tu? Sijui hii definition umeitoa wapi!!! Kwamba hujawahi kusikia wizi wa kutumia kalamu? Kwamba hujawahi kusikia forgery? No naogopa kuamini kwamba haujawa influenced na kitu kusema uliyoyasema!!!!

Tiba
 
yaani nimeiruka hii mada mda mwingi sana kwani sikutaka kujiumiza roho,nasasa nimeisoma roho imeumia tena anyway,kwenye intavyuu ya mama simba wamempa manji kiwanja kajenga na anawalipa kakodi kidogo tu cha kiwanja,mkataba miaka 33.nasasa rostam au somaiya sijui nani sijui utasikia nao mkataba miaka 50,yaani hawa wahindi kweli wamejua kututia vidole vya ******,hakyamungu sasa namuunga mkono idd amin alivyowafurumusha,iko siku nasisi bongo atakujaingia chizi mmoja madarakani watakoma,LAKINI......?SIKU YENYEWE LINI SASA ?AAAAARGH,bora nijiendee zangu kwenye jukwaa la mapenzi na udaku na pilau mie,haya yashanishinda,halafu kesho atakuja mtu analalamika ooh JF siku hizi hamna hoja ya maana,tumechoka na mambo haya bana.
 
Hii nchi hii kuna watu wameamua kujisahau wanafikiri kila mtu anafanana nao. Kila kitu kina matokeo hata hili la kuchezea chezea mambo ya msingi ya uimara wa taifa letu nalo lina matokeo yake
 
Mkuu Kidatu,

I am sorry but are you out of your senses? Kwamba kwa kuwa mtu akutumia bunduki kuiba basi huyo ni halali yake kuachwa aendelee kupeta? Kwamba anayestahili kuitwa mwizi ni huyo anayetumia bunduki tu? Sijui hii definition umeitoa wapi!!! Kwamba hujawahi kusikia wizi wa kutumia kalamu? Kwamba hujawahi kusikia forgery? No naogopa kuamini kwamba haujawa influenced na kitu kusema uliyoyasema!!!!

Tiba

Tiba,
asante kwa mchango wako katika maada hii. Lakini samahani kwa kukuambia kwamba wewe na wengine wengi hapa mnashindwa kuchambua na kuelewa mambo vyema hivyo mnafuata upepo na mkumbo.

Point yangu ni kwamba wapuuzi na wanaotuumiza ni wale tuliowapa madaraka na ofisi kubwa. RA hawezi kufanya hayo yote anayoyafanya kama asingepata msaada na ushirikiano wa wahusika katika ofisi kubwa. Hawa wakuu kama wangeamua kukataa kumpa ushirikiano asingefanya hayo yote, hivyo kwa mtazamo na uelewa wangu wezi na mafisadi ni wale wanaompa ushirikiano na misaada katika kufanikisha machafu hayo. Kwa ufupi ili nikusaidie kuelewa point yangu jiulize hivi RA angelifanya haya machafu enzi za Nyerere?.

Hakuna sababu ya kumlaumu RA bali wakulaumiwa ni wale wanaoruhusu hayo machafu kufanyika.

Kumbuka mbuzi anakula kufuatana na urefu wa kamba uliyomfungia, hivyo maamuzi ya eneo gani na la ukubwa gani mbuzi wako ale ni lako wewe mfugaji. Usimlaumu mbuzi kwa kula eneo kubwa wakati umemfungia kamba ndefu, kama hutaki ale eneo kubwa basi fupisha kamba. Bila shaka umenielewa.
 
Kama connection hiyo ni ya kweli,najiuliza huyu jamaa katulisha nini hata tunamshindwa ilihali katika kila aina ya ufisadi yumo au ana mahusiano nao? mwenye jibu anisaidie maana mie nahisi nimechanganyikiwa

Rostam Aziz ndo jina lake...jua maana ake halisi kwa kutumia kamusi za mafisadi mkuu....
 
mwenye uweza wa kunipa bomu la kuweza maliza mafisadi wote naomba anipe mie ntajitoa mhanga kwa faida ya Watanzania wote maana sina maana tena....
 
Kinachonichekesha ni kwamba miaka si mingi iliyopita washua wakipandishwa vyeo basi watoto wanajua pamoja na mambo mengine lakini yeeees obey hiyo! Kuhamia oysterbay ilikuwa ni motivation kubwa kwa watumishi wa serikali na familia zao. Leo hii hali si hivyo, tumeshindwa kabisa kupanua au kuanzisha obey yetu zaidi ya ile ya mkoloni na kinachotokea ndio mambo kama haya. Every tycoon anataka akabanane O'bay na Masaki kwa namna yeyote ile.

Funny enough less than a km (Msasani uswahilini) kuna abject poverty ambayo huwezi kuamini wala kufikiri. For all these years Msasani, Kinondoni, Mwananyamala and possibly Manzese zingeweza kuwekwa infrastructure safi na sustainable kuipanua O'bay na Masaki.

Angalia suburb kama Chang'ombe ndiyo imejifia hivyo....................Mbezi beach barara mbovu, access ya kwenda mjini ni mainly thru barabara 2 tu, one way lane. Bahari beach is just so minute! Na all in all si kila mtu lazima akae kando ya bahari. Mipangilio imgekuwa mizuri hata ukikaa mtaa wa ishirini kutoka baharini bado ingekuwa bomba tu. Just kama ilivyo huku ughaibuni.

Sehemu kama Mbweni, "Boko" and Bunju at least kuna mipangilio lakini barabara za vumbi na ni vilane vile vile kama huku kwa zamani. By the main road ndiyo usiseme ni takataka tu kama vile Manzese. Kimara no mipango miji no maji and the list goes on and on and on..............
 
Tiba,
asante kwa mchango wako katika maada hii. Lakini samahani kwa kukuambia kwamba wewe na wengine wengi hapa mnashindwa kuchambua na kuelewa mambo vyema hivyo mnafuata upepo na mkumbo.

Point yangu ni kwamba wapuuzi na wanaotuumiza ni wale tuliowapa madaraka na ofisi kubwa. RA hawezi kufanya hayo yote anayoyafanya kama asingepata msaada na ushirikiano wa wahusika katika ofisi kubwa. Hawa wakuu kama wangeamua kukataa kumpa ushirikiano asingefanya hayo yote, hivyo kwa mtazamo na uelewa wangu wezi na mafisadi ni wale wanaompa ushirikiano na misaada katika kufanikisha machafu hayo. Kwa ufupi ili nikusaidie kuelewa point yangu jiulize hivi RA angelifanya haya machafu enzi za Nyerere?.

Hakuna sababu ya kumlaumu RA bali wakulaumiwa ni wale wanaoruhusu hayo machafu kufanyika.

Kumbuka mbuzi anakula kufuatana na urefu wa kamba uliyomfungia, hivyo maamuzi ya eneo gani na la ukubwa gani mbuzi wako ale ni lako wewe mfugaji. Usimlaumu mbuzi kwa kula eneo kubwa wakati umemfungia kamba ndefu, kama hutaki ale eneo kubwa basi fupisha kamba. Bila shaka umenielewa.

Hivi hujui kama Kikwete kawekwa mfukoni na RA kwa kumfadhili katika uchaguzi wa 2005? Kama singekuwa kawekwa mfukoni huyu RA angekuwa jela kwa uharamia mkubwa alioufanya dhidi ya nchi yetu, lakini hata kuchunguzwa tu hachunguzwi kwa sababu Kikwete anamuogopa anaweza. Kafanya uharamia mbali mbali wa kuiba mabilioni ya fedha na juzi juzi karuhusiwa kuuza mtambo wa Richmond katika mazingira ya kutatanisha pamoja na Mahakama kumzuia kufanya hivyo mpaka alipe deni lake la mabilioni kwa shirika la umeme. Huyaoni tu hayo? Anajua anaogopwa na yeye anatumia kuogopwa huko kuendelea kuifisadi nchi.
 
Kwani hawa Wadosi Rostam Aziz na Tanil Somaiya ni bullet proof? Wanaweza kuwa na "bullet-proof wallets" lakini risasi moja tu utosini kila moja kwshnei wao na ufisadi wao. Nyambaaf!
 
Sielewi hii Story,sioni link yeyote ya nyumba na pesa za serikali au ofisa wa serikali,kama ni Rostam hakuna cha ajabu hapo jamaa ni billionea na hakuna ajabu kwa mtu kama yeye kujenga nyumba kama hii,mpaka mje na story kamili lakini hii ni majungu tuu na hakuna cha ajabu kwa mtanzania kujenga nyumba kama hiyo
 
Back
Top Bottom