Jumatano ya Majivu: Wakatoliki kupakwa majivu bila kuguswa ili kuepuka Corona

Ndio,ubovu wa Mambo ya Mungu kuingiliwa na mwanadamu,mnaacha kufuata anayoamlisha Mungu,tunamfuata mwanadamu ambaye akifa atahukumiwa kama sisi
 
Ni jambo jema!

Hata ubatizo wa watoto wachungaji wa KKKT wanatumia jagi kummwagia maji mtoto kichwani badala ya mikono.

Leo askofu mkuu Dr Shoo ameendesha ibada mjini Tabora akiwa amevalia barakoa lakini 95% ya waumini akiwemo RC na DC hawakuvaa barakoa.
Pale kiongozi anapojali madaraka kuliko uhai.
 
maji ya baraka vipi yanaendelewa kuchovywa na kila mtu kufanya ishara ya msalaba? padre mgawa sakrament atakuwa anavaa gloves ? vipi kuhusu kubusu pete ya askofu na papa marufuku?

vipi kuhusu ijumaa kuu kubusu msalaba haiwezi ambukiza corona ? kanisa limeelekeza nini?
Maji ya baraka hayapo tena plus kubusu msalaba hakutakuwepo zaidi ya kuinamia tu... cha msingi ni kuonyesha ishara na kuwa na moyo wa kumpenda Yesu wa msalaba
 
Ni jambo jema!

Hata ubatizo wa watoto wachungaji wa KKKT wanatumia jagi kummwagia maji mtoto kichwani badala ya mikono.

Leo askofu mkuu Dr Shoo ameendesha ibada mjini Tabora akiwa amevalia barakoa lakini 95% ya waumini akiwemo RC na DC hawakuvaa barakoa.
Huyo Shoo nae ana kiherehere kama yule Bagonza tu
 
Wewe ni hopless sana, una kisirani cha kijinga kwasababu wakatoliki walikuwa wa kwanza kuwataka waumini wao wachukue tahadhari kujikinga na Corona, ulitaka wadanganywe waendelee kufa na kuugua Nimonia?

Wacha upumbavu, hao waumini wakienda kuungama watavaa barakoa.
Mbona una hasira sana?

Kama wakatoliki wako serious kwanini wasizuie mikusanyiko zikiwemo ibada kabisa?
 
Ndio,ubovu wa Mambo ya Mungu kuingiliwa na mwanadamu,mnaacha kufuata anayoamlisha Mungu,tunamfuata mwanadamu ambaye akifa atahukumiwa kama sisi
Uko sahihi Yesu aliposema ya kaisari aachiwe kaisari alikuwa hatanii
sayansi na dini tofauti sayansi haijawahi amini dini hata siku moja ndio maana maaskofu katoliki huamini Yesu alikufa na kufufuka sayansi haikubali Katoliki wanasema Maria mama Wa Yesu ni bikira pamoja na kuwa alimzaa Yesu sayansi haikubali pia Katoliki huamini Maria Mama wa Yesu alipaa sayansi haiamini!!!!

Leo hii Papa na maaskofu wa katoliki na mapadri wamegeuka wahubiri wa sayansi!!! Yesu aliwatuma kuhubiri injili sio sayansi au wanasayansi wanasemaje?

serious kuna tatizo masskofu na mapadri na papa hawamjui Mungu wanayemsingizia kuwa kwaita!! Vinginevyo wange stick kwenye kwenye dini isemacho sio ku twist twist kwa kuangalia dunia au corona inasemaje

corona imekuja kupepeta imani ili waamini Mungu halisi wajulikane na matapeli wajulikane wawe mapapa au maaskofu

Raisi Magufuli kama Mlei muumini wa kawaida aliposema tufunge siku tatu kuomba alibezwa na hadi masskofu waliokomaa kuwa wanasayansi wasikilizwe !!! Lakini kile ndio kilikuwa kipimo chao cha uaskofu kama ni watumishi wa Mungu au wanasayansi au wa Corona
 
hivyo vyote vinafuatwa vyema kabisa
kwa hiyo mnajikinga kanisani sababu mnamtuhumu Mungu kuwa aweza kuwa kidudu cha corona kuwaambukiza?

kuwa mkiwa busy kumuabudu yeye atakuwa busy kuwagawia Corona?

Kwa hiyo shetani wa Corona yuko hadi kanisani na ana nguvu ya kueneza Corona kuliko nguvu ya Mungu kulinda waumini wasipate Corona wakiwa wanaabudu? NANI MWENYE NGUVU IBADANI KATI YA MUNGU NA SHETANI? INAONYESHA WAZI KWA WAKATOLIKI SHETANI NI TISHIO
 
Mimi huwa nawaza yale matoleo hasa sadaka,zile pesa tunazishika na wao pia. Kwa kifupi huu ugonjwa umetushika pabaya
pesa hawajasema zivalishwe barakoa na watoa sadaka wavae gloves? Pesa hazitakiwi kuvalishwa barakoa? Maaskofu wanasemaje kuhusu pesa kuvalishwa barakoa? ukitilia maanani kuwa mtoa sadaka aweza kuwa anatoka mijasho viganjani au kaipata pesa kwa jasho au kapokea kwa mtoka jasho la corona eg kwenye daladala nk?
 
Tuendelee kunawa na maji tiririka
na hela za sadaka noti na coins zioshwe maji tiririka au?
Maji ya baraka hayapo tena plus kubusu msalaba hakutakuwepo zaidi ya kuinamia tu... cha msingi ni kuonyesha ishara na kuwa na moyo wa kumpenda Yesu wa msalaba
Kwa dini katoliki sasa inategemea hali ya hewa na dunia ? haiko static inategemea dunia inaendaje sio imani ya mitume na mababa wa kanisa isiyobadilika inasemaje? inaenda na fashion ya dunia na haki ya dunia au?
 
Ndio,ubovu wa Mambo ya Mungu kuingiliwa na mwanadamu,mnaacha kufuata anayoamlisha Mungu,tunamfuata mwanadamu ambaye akifa atahukumiwa kama sisi
wewe ulitakiwa upewe upapa kanisa katoliki badala ya huyu Papa Francis aliyepo asiyejielewa
 
na hela za sadaka noti na coins zioshwe maji tiririka au?

Kwa dini katoliki sasa inategemea hali ya hewa na dunia ? haiko static inategemea dunia inaendaje sio imani ya mitume na mababa wa kanisa isiyobadilika inasemaje? inaenda na fashion ya dunia na haki ya dunia au?

Acha mawazo mgando,nazungumzia mikono yetu baada ya kushika vyote hivyo.
 
kwa hiyo mnajikinga kanisani sababu mnamtuhumu Mungu kuwa aweza kuwa kidudu cha corona kuwaambukiza?

kuwa mkiwa busy kumuabudu yeye atakuwa busy kuwagawia Corona?

Kwa hiyo shetani wa Corona yuko hadi kanisani na ana nguvu ya kueneza Corona kuliko nguvu ya Mungu kulinda waumini wasipate Corona wakiwa wanaabudu? NANI MWENYE NGUVU IBADANI KATI YA MUNGU NA SHETANI? INAONYESHA WAZI KWA WAKATOLIKI SHETANI NI TISHIO
Mambo mengine inahitaji ujifikiri ndipo useme hayo yote ngoja nikuambie Mungu ni mkuu kuliko wote na vyote hivyo amekupa/ametupa akili au uwezo wa kutambua mema na mabaya.

Hivyo basi kama unajua kwamba ugonjwa unaenezwa kwanjia ya hewa,kutonawa mikono,majimaji mfano jasho, n.k na wakati huo unajua namna ya kujikinga kwahiyo ukaacha kujinga ukitarajia Mungu aje akukinge wakati huo wewe mwenyewe hutaki kujikinga Usiwe kama wagalatia.

Hivyo ishi na kumtumaini Kristo ili uje upate thawabu
 
kwa hiyo mambo yote ya kuchovya maji wakati ukiingia kanisani na kufanya ishara ya msalaba na ukitoka,kubusu msalaba au pete ya askofu ,kupaka majivu kwenye paji la uso ni nk ni mafundisho ya kibinadamu yasiyo na uhusiano na Mungu yasiyo na maana yeyote? Sio Mungu aliagiza ni mambo ya kidunia ya kujitungia ambayo yaweza badilishwa muda wowote ?
 
aliyekuambia Ishara ya msalaba haipigwi nani?
Ishara inapigwa kama kawaida.

Haina haja ya kuendelea kubishana na wewe maana sikuelewi unarudia kitu unachoelekezwa
Usiwe sawa na Mpinga kristo
 
Back
Top Bottom