Jumatano ya Majivu 2018: Siyo Valentine tu bali Mabadiliko

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Imeandikwa na Pascal Mwanache, Communication TEC

Mtakatifu Valentino ni nani?

Alikuwa Padri wa Roma (Italia) ambaye aliishi kwa kuishuhudia imani ya kikristo kati ya mwaka 197 na 273. Kanisa linamtambua kuwa ni shahidi wa imani kwa kuwa alitoa uhai wake kwa kuilinda, kuitetea na kuitangaza imani ya kikristo.

Aliishi imani ya kikristo nyakati za mfalme Claudio ambaye mara kadhaa alimtesa na kumfunga gerezani na baadaye aliuawa kwa amri ya mfalme Aureliano.

Utakatifu wake

Anatambulika na wengi duniani kwa sababu ya upendo wake kwa watu. Alitumia muda wake mwingi kuwasaidia watu wa ndoa na vijana wachumba kwa kuwafundisha juu ya upendo:
-Upendo ni fadhila kuu ya kikristo na kiutu, kwa hiyo upendo ni kielelezo cha imani na utu
-Uaminifu na umoja ndiyo nguzo za ndoa (ikumbukwe aliishi nyakati ambazo kulishamiri ndoa za mume mmoja na wake wengi)

Mafanikio

Yeye alikemea tabia hii ya wanaume (ikiwemo watawala) kuwa na wake wengi bila kujali mtu yoyote. Polepole watu wakaanza kujirekebisha na upendo ukaanza kurudi ndani ya ndoa. (ndiyo sababu mfalme Claudio alimfunga gerezani).
Aliwakemea vijana wengi walioishi maisha ya unyumba bila ndoa-wengi waliongoka na kufunga ndoa kanisani. Hili lilimkera mfalme kwani vijana wengi waliuingia ukristo.

Aliwatetea vijana waliokuwa jeshini ambao walikatazwa kwa sheria ya mfalme wasifunge ndoa. Alipigania haki ya hao askari na kuwataka watawala waibatilishe sheria hiyo potovu..Katika harakati hzi, alifanikiwa kuwafungisha ndoa wachumba wawili (mmoja mkristo na mwingine mpagani) ambao wazazi wao walikuwa wamewawekea vikwazo. Ikumbukwe mchumba huyu wa kiume alikuwa ni askari.

Tar 14 Februari 273kwa amri ya Mfalme, Valentino aliuawa kwa kukatwa kichwa.

Miaka mitatu aliyofungwa gerezani kabla ya kuuawa alifaulu kumhubiria mkuu wa gereza na kumwongoa. Pia binti mmoja wa mkuu wa gereza ambaye alikuwa kipofu alifanyiwa muujiza na Mt. Valentino akapata kuona. Mkuu wa gereza alibatizwa yeye na familia yake na akafunga ndoa tarehe 14/2/273 siku ya kuuawa kwake. Na siku hiyo aliwaandikia barua watu wengi aliowafungisha ndoa akawasihi wadumu katika upendo, uaminifu na umoja.

Kila barua aliyoiandika mwishoni aliandika “Ndimi Valentino wako”.

Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kubadilika
Kama Mtakatifu huyu alivyotaka kuwabadilisha walimwengu kutoka katika utu na mtazamao wa kale na kuwapeleka katika utu mpya, Jumatano ya majivu inatufungulia kipindi cha kwaresima ambacho nacho kinadai mabadiliko.

Kumbe, Jumatano ya majivu ya mwaka 2018 inakudai sana kwenda Kanisani ukatafakari juu ya nini kinapaswa kufanyiwa mabadiliko katika maisha yako, ili utoke utu wa zamani (uchumba sugu, uzinzi, wizi, ufisadi, uchawi nk) na kuingia katika utu mpya.
 
Back
Top Bottom