Jumapili ya Toba: Nani anayeloga wasomi wetu? [Case study: Dr. Bashiru Ally]

guzman_

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,063
2,000
Jumapili hii tuweke kama jumapili ya toba huenda tulimkosea Mungu mpaka kuruhusu wasomi wetu kurogwa na kutojitambua.

Nitumie mfano wa msomi wetu wa siku zote Dr. Bashiru Ally (Katibu mkuu wa CCM). Huyu alipokuwa chuoni alikuwa ni thinker mzuri sana hasa katika masuala ya siasa na maendeleo ya nchi yetu. Huyu alikuwa ni miongoni walioamini katiba mpya na uhuru wa tume ya uchaguzi. Katika kauli zake za hivi karibuni alishawahi kunukuliwa akilalamika kushuka kwa idadi ya watu wanaojitokeza kupiga kura nyakati za uchaguzi. Na sasa tunamsikia akisema atatumia dola kushinda uchaguzi. Hebu sasa tumnyumbulishe

1.Katiba mpya haiepukiki [Nje ya CCM]
2. Kuwa na uchaguzi huru na haki lazima tuwe na tume huru ya uchaguzi [Nje ya CCM],
3. Katiba mpya sio lazima ya sasa inatosha [Ndani ya CCM],
3. Idadi ya wapiga kura inashuka [Ndani ya CCM]
4. Nitatumia dola kushinda na kubaki madarakani 2020 [Ndani ya CCM]
5. Vyama ambavyo viliacha kutumia dola vilishindwa vibaya sana [Ndani ya CCM]
6. Kauli inayofuata...........{Watu wajitokeze kwa wingi kuchagua viongozi wanaowataka}
Haya ni mawazo ya msomi wa Tanzania..(huo ni mfano mmoja tu).

Jumapili ya leo tumwelekee Mwenyezi Mungu kuomba toba juu ya wasomi matumbo kama hawa.
 

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
2,847
2,000
Njaa tu mkuu hakuna kingine.
You can never negotiate properly when you're desperate...
 

Magna Carta

JF-Expert Member
Jul 14, 2014
4,036
2,000
Ukiwa kiongozi kwa ngazi ya Bashiru lazima useme hayo, kumbuka kashaacha utaalamu sasa ni msanii wa Uongozi
 

mkuu wa kijiji

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
757
1,000
Kwanza naamini kwenye siasa ukileta usomi utashindwa,Bashiru Ali kukubali cheo Cha ukatibu ni kuasi usomi , Pili lazima ukubali kujitoa ufahamu ili uweze kuendana na midundo iliyopo. Usisahau watu wanahitaji serikali itimize wajibu wake lakini wewe hutaki kutimiza wajibu wako . Maendeleo yanaanzia kwetu halafu mwisho serikali.
 

Magna Carta

JF-Expert Member
Jul 14, 2014
4,036
2,000
Ukiwa kiongozi kwa ngazi ya Bashiru lazima useme hayo, kumbuka kashaacha utaalamu sasa ni msanii wa Uongozi
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
6,130
2,000
Siasa za watanzania zinaongozwa na njaa wape kitu wanasiasa wetu watafanya chochote utakacho.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom