#COVID19 Jumanne nitachanjwa ila Rais Samia asinihesabu katika waliomuunga mkono

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,824
35,827
J3 tuna jambo letu. J4 pia tuna jambo letu kulingana na maelekezo ya wizara ya afya.

Hata hivyo wengi wetu tuliipigania hatua hii, wakati SSH na mwendazake wakifanya porojo zao kuhusu ugonjwa huu. Hivyo katu asituhesabu kuwa tutakuwa tumejitokeza kumwunga mkono yeye kwa lolote kuhusiana na hii chanjo.

Ni vizuri pia akafahamu kuwa hata kama asingekuwa kachanjwa sisi tungechanjwa tu.

Vile vile asisahau ukakasi aliotuletea kutokea kwenye kadhia ile ya Mwanza, hapo ndiyo kabisa ametukata stimu!

"J4 nitachanjwa. Ila tafadhali Mama SSH usinihesabu katika list ya watakaokuwa wamejitokeza kuchanjwa eti kwa kuwa umewa 'inspire.' Kwa hakika isingekuwa kwa hali ya huu ugonjwa ilivyo, tungehamasishana dhidi yako."

Niliweke hili wazi, "nilikuunga mkono sana, lakini si baada ya siku zako 100 ofisini, na hasa ulipokuja kutuonyesha rangi zako halisi ulizokuwa bila shaka umezificha."

Nitakuwa mnafiki mno kwa kutokukupa ukweli huo kinagaubaga.

Kumbuka msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.

Habari ndiyo hiyo.
 
Aliyemtoa kafara mzee Ambilikile Mwaisapile:

1. Kwa kumwacha akusanye wagonjwa wa Corona Loliondo pasipo na tahadhari zozote,
2. Kwa kumwacha ashughulike na wagonjwa wa Corona nyumbani kwake bila tahadhari zozote,
3. Kwa kutochukua hatua zozote kuona kifo na mazishi ya mzee huyu yanamalizika salama na kuwa funzo Loliondo na katika nchi nzima,

Hawezi kudai kuwa inspirational figure kwenye chanjo hii. Bora wakae kimya kabisa.

Kwamba bwana alitoa na sasa ametwaa hivyo jina lake lihimidiwe?! Aaah wapi! Kwa kutuona je?

Kwa hakika tutawajibishana tu.

Kwenye siku ile ya kuyasoma majina ya wahanga wote watokanao na ubinafsi wenu, kwa hakika: "jina la Mchungaji Ambilikile Mwaisapile pia litakuwamo."

Kumuunga or kutomuunga mkono ni haki yako. Huwezi ukaongoza watu mil. 60 na ukawafurahisha wote, ndani ya familia tu ya watu wasiozidi 5 kunakuwa na mifarakano. Vilevile eleweni kwamba huyo Mwamba wenu siyo malaika, ukiachilia mbali nafasi yake ya kisiasa, lakini naye ni binadamu kama wewe na anatenda makosa yote ya kibinadamu. Acheni mahakama ifanye kazi yake, Mahakama ile ile iliyomtoa Mdude na kuwarudishia CDM hela zao za faini ndiyo itamuhukumu kwa haki bwana Mwamba, sielewi hizi kelele zote mnazitoa wapi wakati Mwamba yupo katika mchakato wa mahakama unaotambuliwa kikatiba.
 
Nisome vyema. Nimeandika kwa binafsi yangu. Nimempa ya moyoni kwa binafsi yangu kama ninayeipenda tz.

"Hata kama asingechanjwa na hata kama angepiga kampeni tusichanjwe, bado ningechanjwa mimi na washirika wangu."

Haya si maneno matupu. Wanaofahamu hivyo hata humu JF si wachache.

Kamtelekezea janga babu Loliondo. Kawatelekezea janga Loliondo. Bado kama ilivyo ada Babu wa Loliondo kafa kwa umeme wa moyo kukata moto.

Nini alifanya kumlinda babu Loliondo au kuilinda Loliondo dhidi ya ujinga wao na gonjwa hili? Nini anafanya kama funzo Loliondo au nchini?

Kwamba Mbowe kubambikiziwa kesi na sasa tutegemee kuna haki wapi? Haki hiyo kwenye kipindi cha mwendazake ilikuwa wapi? Kwani nini kimebadilika?

Hayo uliyoyataja huko mahakamani angekuwapo yule dhwalimu baba lao si mngesema pia haki ndiyo imetendeka?

Hatutaki haki kwa ridhaa ya mtu na muda anaotaka yeye. Hatutaki haki nusu nusu. Tunataka haki kamili na hiyo ndiyo inayotupa nguvu, uthubutu na utayari wa kuilipa gharama yote inayohitajika ili kuipata:

Haki ni kwa mujibu wa katiba.

Hivi mnatuona je lakini?
 
Kuandika ukiwa umejificha nyuma ya keyboard na fake id ni rahisi sana, ishu inakuja kwenye kutake actions mstari wa mbele, hapo ndipo makamanda huwa wanaanza kusingizia wananchi wa tz wamelala, nyie siyo wananchi? Babu wa loliondo ni kama wafuasi wa "vibwetere" tu, sikio la kufa, hata uwaambie nini hawakuelewi, wameshamezeshwa takataka kwa brain zao.
 
Mmeambiwa chanjo ni HIARI, sasa mambo ya kumuunga mkono Rais Samia yanatoka wapi? Au watu hamjui maana ya neno hiari 🤔

Chanjo ni hiari ndiyo maana niko kwenye kukumbusha kuwa siendi kuchanjwa kwa sababu katokea kuchanjwa hadharani.

Katokea hadharani ku inspire watu kuchanjwa. Hiyo ni kwa maneno yake. Labda kama unataka kuurekebisha usemi wake 😂😂!

Jiridhishe kuwa usiyeelewa maana ya hiari hii ni wewe.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kuandika ukiwa umejificha nyuma ya keyboard na fake id ni rahisi sana, ishu inakuja kwenye kutake actions mstari wa mbele, hapo ndipo makamanda huwa wanaanza kusingizia wananchi wa tz wamelala, nyie siyo wananchi? Babu wa loliondo ni kama wafuasi wa "vibwetere" tu, sikio la kufa, hata uwaambie nini hawakuelewi, wameshamezeshwa takataka kwa brain zao.

Umemchanganya babu wa Loliondo na kibwetere sikio la kufa wa kanisa la ufufuo kamili?

Kwani Babu wa Loliondo hata alionywa au kupewa angalizo tu na nani kuhusiana na hatari iliyokuwa ikimuelekea kutokana ujinga wake?

Je serikali ilichukua hatua gani kumlinda yeye au kuilinda Loliondo?

Hivi waziri Mkuu na vigogo wizara ya afya wangalipo ofisini pamoja na kadhia hii ya babu na Corona? Bado unathubutu kumwita huyu babu kuwa ni kibwetere? Kibwetere atakuwa yeye au hawa waliokolea huku serikalini?

Kwamba fake ID nyuma ya keyboard? Zama tofauti sana hizi. Si, jiwe alitubatiza kwa moto?

Au wewe umesahau jombi?

Tunayo nafasi ya kuyasimamisha yasiyo ya haki yasitokee tena. Hayo ni kama haya mnayotaka kumvisha nayo Mheshimiwa Mbowe.

Nafasi hiyo tutaitumia kikamilifu Inshallah!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kumuunga or kutomuunga mkono ni haki yako. Huwezi ukaongoza watu mil. 60 na ukawafurahisha wote, ndani ya familia tu ya watu wasiozidi 5 kunakuwa na mifarakano. Vilevile eleweni kwamba huyo Mwamba wenu siyo malaika, ukiachilia mbali nafasi yake ya kisiasa, lakini naye ni binadamu kama wewe na anatenda makosa yote ya kibinadamu. Acheni mahakama ifanye kazi yake, Mahakama ile ile iliyomtoa Mdude na kuwarudishia CDM hela zao za faini ndiyo itamuhukumu kwa haki bwana Mwamba, sielewi hizi kelele zote mnazitoa wapi wakati Mwamba yupo katika mchakato wa mahakama unaotambuliwa kikatiba.
Wewe unaamini Tanzania tuna mahakama katika maana ya mahakama? Mahakama gani inayofanya kazi kwa kuelekezwa na Rais?

Magufuli alisema, funga hawa, na walifungwa. Samia akasema, watoeni, wakawatoa. Hiyo utasema ni mahakama?
 
Tz kwa nini watu watumie feki ID???
Rais ajiulize kwa nini watu wanaogopa kusema ukweli Tz??? Jambo baya sana!! Yeye alimwogopa Magufuli ndiyo maana hakujiusulu!! Majaliwa naye aliogopa!! Spika naye aliogopa ndiyo maana sasa kidogo anageuka!! Legislature iliogopa!!! Waandishi wa habari waliogopa!!!
Ndiyo maana nchi imekwenda kombo!!!
 
Hawezi kujiuliza kwa maana wanaweka maslahi ya matumbo yao mbele.
 
J3 tuna jambo letu. J4 pia tuna jambo letu kulingana na maelekezo ya wizara ya afya.

Hata hivyo wengi wetu tuliipigania hatua hii, wakati SSH na mwendazake wakifanya porojo zao kuhusu ugonjwa huu. Hivyo katu asituhesabu kuwa tutakuwa tumejitokeza kumwunga mkono yeye kwa lolote kuhusiana na hii chanjo.

Ni vizuri pia akafahamu kuwa hata kama asingekuwa kachanjwa sisi tungechanjwa tu.

Vile vile asisahau ukakasi aliotuletea kutokea kwenye kadhia ile ya Mwanza, hapo ndiyo kabisa ametukata stimu!

"J4 nitachanjwa. Ila tafadhali Mama SSH usinihesabu katika list ya watakaokuwa wamejitokeza kuchanjwa eti kwa kuwa umewa 'inspire.' Kwa hakika isingekuwa kwa hali ya huu ugonjwa ilivyo, tungehamasishana dhidi yako."

Niliweke hili wazi, "nilikuunga mkono sana, lakini si baada ya siku zako 100 ofisini, na hasa ulipokuja kutuonyesha rangi zako halisi ulizokuwa bila shaka umezificha."

Nitakuwa mnafiki mno kwa kutokukupa ukweli huo kinagaubaga.

Kumbuka msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.

Habari ndiyo hiyo.
Safi kabisa unakuwa inspired na science behind vaccine siyo haya matakatakà
 
Kuandika ukiwa umejificha nyuma ya keyboard na fake id ni rahisi sana, ishu inakuja kwenye kutake actions mstari wa mbele, hapo ndipo makamanda huwa wanaanza kusingizia wananchi wa tz wamelala, nyie siyo wananchi? Babu wa loliondo ni kama wafuasi wa "vibwetere" tu, sikio la kufa, hata uwaambie nini hawakuelewi, wameshamezeshwa takataka kwa brain zao.
Stupid wewe uko wapi
 
Safi kabisa unakuwa inspired na science behind vaccine siyo haya matakatakà

Hawa watu wanatuona sisi ni wajinga kuliko wao. Wanadhani bila wao sisi hatuna maamuzi. Bure kabisa!
 
Back
Top Bottom