Jumanne Kishimba Mbunge aliyetabiriwa kutokuleta utulivu wa siasa ndani ya Jimbo la Kahama.

Cyangungu

Member
Nov 7, 2019
45
54
Wengi wa Wananchi hasa wenyeji wa Jimbo la Kahama mjini hawakutarajia kabisa endapo ndugu Jumanne Kishimba Mbunge wa Jimbo lile angeleta utulivu wa kisiasa pale Kahama mjini kwasababu ya hali ya kisiasa wakati wa kampeni za Uchaguzi wa mwaka 2015 ilivyokuwa tete.

Leo,Kahama kupo shwari kabisa na Jumanne anao uhakika wa ushindi kwa awamu nyingine hapo mwaka 2020.

Kwa hakika Kahama ambayo ni Manispaa tarajiwa kupo shwari!Siasa za Upinzani hazipo tena.Heko ndugu Jumanne.
 
..bila upinzani chama tawala na wabunge wake watabweteka.

..zama hizi za UTANDAWAZI siyo vema kujisifia kuwa eneo fulani halina siasa za upinzani / ushindani.
 
Kwa upinzani huu wa kina Makongoro Mahanga afadhali tubaki bila upinzani. Hivi ikitoka CCM wakaingia hawa, mwananchi anaweza kupata unafuu upi?!
 
..Makongoro Mahanga alipokuwa CCM wewe ulikuwa upinzani?

..au ulianza kupinga siasa za ushindani baada ya Makongoro Mahanga kuhamia CDM?

..upinzani kama ilivyo kwa CCM kuna watu wabaya na wazuri. Jambo la msingi ni kuwainua wale wazuri.

..kwa uzoefu wangu na siasa za Tz maeneo ambayo hayana USHINDANI wa kisiasa mara nyingi pia huwa nyuma kimaendeleo.

..kuna maeneo hapa Tz yamekuwa na utamaduni wa kubadilisha wabunge kati ya CCM na vyama mbadala. Nadhani tukipata maeneo mengi ya namna hiyo nchi itasonga mbele.
 
Hujajibu swali langu. Nimeuliza, wakitoka CCM wakaingia hawa kina Mahanga ni unafuu gani mwananchi ataupata?! Tungepata unafuu gani kwa mfano Lowasa angekuwa Rais kupitia CHADEMA?!
 
..wakitoka ccm, au wangetoka ccm?

..Do you believe this is the best we can do?
 
kahama inatia aibu kwenye miundombinu,barabala sitendi kuu ya mabasi,wamezidiwa hata na Nzega ,karagwe,Korogwe,utafikili wilaya haina viongozi,ficha aibu yako kuitajataja Kahama ni kuchefuchefu.
 
Wengi wa Wananchi hasa wenyeji wa Jimbo la Kahama mjini hawakutarajia kabisa endapo ndugu Jumanne Kishimba Mbunge wa Jimbo lile angeleta utulivu wa kisiasa pale Kahama mjini kwasababu ya hali ya kisiasa wakati wa kampeni za Uchaguzi wa mwaka 2015 ilivyokuwa tete.

Leo,Kahama kupo shwari kabisa na Jumanne anao uhakika wa ushindi kwa awamu nyingine hapo mwaka 2020.

Kwa hakika Kahama ambayo ni Manispaa tarajiwa kupo shwari!Siasa za Upinzani hazipo tena.Heko ndugu Jumanne.
Kutokuwepo siasa za ushindani na kubaki na NDIOOO limekuwa jambo la kujisifia na kusema heko?
Wacha tuu Marehemu Kenyatta aliye sema nchi yetu ya TZ inao maiti wanaotembea!
 
Kishimba amefanya nini mpaka sasa jama hana hata ushawishi kabisa

Sema pesa zake tu akiwa wazee ( viongozi wa CCM ) wanapamba sana kitu ambacho lembeli alikataa kuwapa hela hao jamaa

Kabla ya mwaka 2015 madiwani wengi walikuwa upinzani tu sema huu uchaguzi wa mwaka 2015 CCM walivuruga uchaguzi pia walikuwa wanasema hata wasipo wachagua wanashinda tu na kweli matokeo ya uchaguzi na rafa zao CCM wakashinda

Madiwani wengi walitoka upinzanj kahama kunamchanganyikowa makabila mengi ushindani upo sana sema Mzee kazuia siasa tu

Nadhani uliona hata uchaguzi ulivyoisha mwaka 2015 CHADEMA walianzia wapi kufanya kampeni wakapigwamabomu hadi kutoboa bati la msikiti
 
Back
Top Bottom