Jumamosi ya Usafi: Kuna uonevu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali

inyele

JF-Expert Member
Aug 8, 2017
1,645
1,258
Wakuu salaam!

Kama ambavyo iliasisiwa na Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dr JPM kwamba kila siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi itumiwe na wananchi kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo yao yanayowazunguka.

Awali siku hii ya usafi ilizingatiwa na kupewa umuhimu mkubwa na usafi ulifanyika kwa usimamizi wa viongozi wa serikali za mitaa. Usafi ulifanyika kwa utaratibu mzuri kwa wananchi wote kushiriki na asiyeshiriki aliadhibiwa na heshima ikajengeka kwa kiasi kikubwa ndani ya siku hii ya usafi wa kitaifa.

Bila shaka pengine muasisi wa siku ya Jumamosi ya usafi alikuwa na nia njema kabisa ya kuhakikisha mazingira ya nchi yetu yanakuwa katika hali nzuri kiusafi na kwa ustawi wa afya ya jamii ya Tanzania. Kadri muda ulivyoenda mbele zaidi hata kipindi cha uhai wa JPM mambo yalianza kubadilika kutokana na watu kuanza kuipuuza hii siku ya usafi. Watu walianza kufanya usafi kwa kujiamulia tu. Yaani ukifanya usafi au usifanye vyote ni sawa tu na hakuna atakayefuatilia.

Tatizo linakuja hivi wakuu:-
Kuna baadhi ya maeneo hapa nchini/mitaani mwetu haki haitendeki. Naona jamii imegawanyika katika makundi makuu mawili ambapo kuna watu ambao wao ni lazima wafanye usafi ndani ya siku hii ya jumamosi ya mwisho wa mwezi na lingine limeachwa huru. Wapo wafanyabiashara/wajasiriamali wenye ofisi zao za kudumu ambao hulazimika kutofungua ofisi zao hadi saa nne asubuhi muda ambao inasemekana ndio unatosha kuwa ishara ya usafi kufanyika na kuruhusu mambo mengine kufanyika. Ikitokea mwenye ofisi mfano duka kafungua kabla ya muda huo basi lolote linaweza kutokea la kuvuruga amani kwa kuvamiwa na uongozi wa serikali ya mtaa kwa kushirikiana na jeshi la polisi, kuna mtu kupigwa faini bila huruma na kupelekwa kituo cha polisi na kupatiwa adhabu kali.

Wakati hayo yote yanaendelea kwa wafanyabiashara kuna watu wameamka saa kumi alfajiri wako mitaani wanazunguka huku na huko wakitafuta riziki nakadhalika. Mfano watu wa usafirishaji boda boda, dereva taxi n.k. Hawa watu wao ni ruksa kufanya biashara yao na hakuna mtu wa kuwauliza kama wamefanya usafi au la. Na hao abiria wao wamefanya usafi au la. Hakuna wa kuwafuatilia watu wanaozurura asubuhi ya siku ya jumamosi ya usafi hata kama muda ulioruhusiwa kufanya mambo mengine tofauti na usafi haujafika.

Binafsi naona huu ni uonevu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wetu. Yaani mtu mwenye leseni ya biashara anayelipa kodi kwa serikali bila chenga ndiye anayebanwa kuliko wengine. Naomba wajuvi wa mambo haya mjitokeza na mtupe mwongozo katika vipengele vifuatavyo:-

(1) Je, suala la usafi kila siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi lipo kisheria?

(2) Je, ni nani aliyekusudiwa kufanya usafi ndani ya siku hii ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi?

(3) Je, muda sahihi wa kumalizika usafi ni saa ngapi?

(4) Je, asiyefanya usafi anatakiwa kuwajibishwa vipi?

(5) Je, ni upi msimamo na mwongozo wa serikali yetu ya sasa juu ya siku ya jumamosi ya usafi?

N.B. Wakuu nawaomba pia mlete uzoefu wenu wa kinachoendelea kwenye mitaa yenu ili tupate picha kamili ya hali iliyopo nchini kwa sasa na mitazamo ya jamii yetu juu ya suala la usafi katika siku hii ya jumamosi ya mwisho wa mwezi!

Nawasilisha
 
Hivi kwa mfano KARIAKOO kuna kampuni ya Usafi KAJENJERE kila Duka linalipa 40,000 kwa Mwezi

Hiyo jumamosi wafanyabiashara wanafanya usafi gani?!

Serikali imefikiria inapoteza mapato kiasi gani kwa kufunga biashara kwa masaa matatu kwa ajili ya usafi ambao kiuhalisia haupo?!!
 
Hivi kwa mfano KARIAKOO kuna kampuni ya Usafi KAJENJERE kila Duka linalipa 40,000 kwa Mwezi

Hiyo jumamosi wafanyabiashara wanafanya usafi gani?!

Serikali imefikiria inapoteza mapato kiasi gani kwa kufunga biashara kwa masaa matatu kwa ajili ya usafi ambao kiuhalisia haupo?!!
Kuna tatizo sehemu juu ya hili cha ajabu hakuna mwongozo sahihi kutoka serikalini
 
Ni upuuzi mtupu na kupotezeana muda , maeneo kama Kariakoo Usafi ufanyike usiku tu kila siku.

Hii ya kutofungua maduka hadI saa 4 jumamosi ya kila mwisho wa mwezi ni kupotezeana muda, hata Usafi wenyewe wala haufanyiki
 
Nakumbuka wenye maduka walikuwa wanangojea saa nne ipite ndio wafungue, waanze biashara
 
Ni upuuzi mtupu na kupotezeana muda , maeneo Kama Kariakoo Usafi ufanyike usiku tu kila siku
Hii ya kutofungua maduka hadI saa 4 jumamosi ya kila mwisho wa mwezi ni kupotezeana muda, hata Usafi wenyewe wala haufanyiki
Ngoja tusubiri waje
 
Kwa hiyo siku hizi hakuna huo utaratibu
Huo utaratibu ulianza kwa kasi sana lakini kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele ulilegalega na hatimaye ukaondoka na mwendazake, taasisi imara ni muhimu kuliko kiongozi imara
 
Kwa hiyo hamtaki kufanya usafi? Mnatakiwa mtandikwe fimbo za shingoni "salasini na sita" kila mmoja hadi adabu kwa sirikali iwajae. Mnahoji agizo la sirikali? Huu ari yuuu bai zi wei?
 
Mkuu hakuna haja ya kuleta utani ,, lete mwongozo wa hiyo serikali
 
Back
Top Bottom