Juma Tomas Zangira: Mtu wa kwanza kutiwa hatiani kwa kosa la ujasusi

Usalama wa Taifa ulimhisi Ndg JTZ kuwa anaunganisha mawasiliano kati ya Oscar K na John W. Barua, zake zilikuwa zikidukuziwa Posta. Alikuwa staff wa Kilimanjaro hotels.
Serikali ilisema jamaa alikuwa jasusi
 
Tushukuru sana yule mzee na usalama wa Taifa. Hawa wakina bibi walishagawana kila kipande na kusahau tuko zaidi ya mil 40. Nina shaka kama walijiandaa kumaliza mida wa kukaa kwenye madaraka. RIP Mwalimu Julius Nyerere
 
Wewe punguani unachoongea ni nini?

Teh teh teh. ...ukiona mtu anakimbilia kutukana fahamu fika ameshaishiwa hoja. Awamu ya nne imeisha na majanga yake pia. Teh teh teh. ...ndio maana tunatufa container kama zimekuwa shindano
 
sio kwamba faizafox habari ya kwenda ikulu kama wanaenda msalani kwa hawamu ya tano ndio imekwisha haaahaaa waanza kuelekea msoga kwa jamaa yao
 
Pia katika kesi hiyo umahili wa wakili Mkude kama sikosei ulijidhihilisha sana kama mwasheria nguli aliyebobea r.i p
 
Miaka ya 1975 na kuendea kuna na kesi ya aliyekuwa mfanyakazi wa Kilimanjaro hotel akiitwa Juma Thomas Zangira. Huyu bwana alishtakiwa kwa kesi ya Ujasusi. Ninaomba anayeijua mwisho wa kesi hiyo na huyu bwana yuko wapi atujuze.

======

JUMA THOMAS ZANGIRA: MTANZANIA WA KWANZA NCHINI KUSHTAKIWA KWA UJASUSI

Moja kati ya kesi kubwa za kihistoria nchini Tanzania ni ile kesi ya UJASUSI (ESPIONAGE) iliyomhusu Bw. JUMA THOMAS ZANGIRA ambayo ilirindima nchini mwaka 1977. Hii ilikuwa ni kesi ya aina yake iliyowaacha wananchi wakiwa hawaamini maskio yao kwani hii ilikuwa ni kesi ya kwanza ya ujasusi nchini.

Siku ya Jumapili, tarehe 25.9.1977, Radio Tanzania Dar Es Salaam, katika taarifa yake ya habari saa mbili usiku, ilieleza kwamba Bw ZANGIRA atapelekwa mahakamani kesho yake, jumatatu. Hata hivyo, RTD haikutaja atapelekwa mahakama ipi. Kwavile wananchi walizoea kwamba washtakiwa wa makosa ya jinai hupelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jumatatu asubuhi watu wengi walijazana mahakamani hapo kujionea wenyewe Mshtakiwa ZANGIRA yukoje na kusikiliza alifanya vipi ujasusi huo.

Hata hivyo, wananchi hao waliula wa chuya kwani kisheria Ujasusi ni kosa kubwa ambalo ni lazma lisikilizwe na Mahakama Kuu na lazma wawepo Wazee wa Baraza kumsaidia Jaji kama yalivyo makosa mengine makubwa kama vile mauaji au uhaini . Ni kwasababu hiyo basi, Bw. ZANGIRA, jumatatu ya tarehe 26.9.1977 alifikishwa Mahakama Kuu, na si Kisutu, toka gereza la Ukonga akiwa amefungwa pingu chini ya ulinzi mkali.

Kutokana na upekee wa kesi hii, ilibidi Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini(DPP) aiendeshe mwenyewe badala ya Mawakili wa Selikali walio chini yake. Aidha, kutokana na ukweli kwamba kesi hiyo ilikuwa ni ya aina yake, ikabidi isikilizwe na Jaji Mkuu, Mh. FRANCIS NYALALI mwenyewe. Mh. NYALALI alisaidiwa na wazee wa Baraza ambao ni Bw. ZUBEIR ALLY, Bw. HUSSEIN ZAMANI na Bw. SIMBA SALUM. Kesi hiyo iliendeshwa kwa kasi ambapo ndani ya siku 10 tu hukumu ikatolewa.

Siku hiyo ya kwanza saa 3 asubuhi, DPP MEELA alimsomea Bw. ZANGIRA mashtaka 3:

Shtaka la 1 lilikuwa ni kukusanya habari kisha kuzitoa kwa mzungu aishie Uingereza aitwaye JOHN WILSON kwa nia ya kuvuruga usalama wa nchi yetu na kwamba taarifa hizo zingeweza kutumiwa na mataifa ya nje yanayoichukia Tanzania kuvuruga usalama wa nchi. Kosa la 2 ni kumpatia Bw JOHN WILSON habari ambazo zingeharibu jitihada za TANU na vyama vya ukombozi vya SWAPO, FRELIMO, PAC, ANC na ZANU na kosa la 3 ni kutoa taarifa za OAU kwa JOHN WILSON. Mashtaka haya yote matatu yalidaiwa ni kinyume na Kifungu cha 9(1)(a) na 9(2)(1) vya Sheria ya Usalama wa Taifa, 1970.

Mshtakiwa ZANGIRA, aliyekuwa akitetewa na wakili THOMAS MKUDE wa lililokuwa Shirika la Sheria Nchini (TLC), alikana mashtaka yote hayo 3 ambayo ilidaiwa aliyatenda kati ya mwaka 1971 na Julai 1977.

DPP, ambaye aliileza Mahakama kwamba Bw. ZANGIRA ni Afisa Uhusiano wa hoteli ya Kilimanjaro aliyekuwa pia Afisa Usalama wa Taifa, aliita mashahidi 8.

Shahidi wa kwanza alikuwa ni SASP ALI JUMA GUGURU. Kwa ujumla, maelezo ya mashahidi hao 8 yalikuwa ni kwamba tarehe 27.7.1977, Bw GUGURU alipokea habari za ujasusi na akamtuma Sajin ABDALLAH kuchunguza nani anatumia sanduku la posta 3900 DSM. Sajin ABDALLAH akatumia mbinu za medani na kugundua kwamba anayelitumia si mwingine bali ni Bw. ZANGIRA hivyo wakaanza kumfwatilia nyendo zake kwa karibu .

Siku tatu tu baadaye, yaani tarehe 29.7.1977, saa 2 asubuhi, Bw ZANGIRA aliondoka nyumbani kwake akawa anaenda "mdogomdogo" ofisini kwake kwa kupitia posta bila kujua kuwa alikuwa anafanyiwa "surveillance" kali ya nyendo zake!.

Bw. ZANGIRA alipofika posta akafungua sanduku lake la barua na kutoa barua moja aliyoikuta. Kufumba na kufumbua akanyakwa na polisi!

Bw. ZANGIRA alikiri kuwa barua hiyo ni yake na ilipofunguliwa ilikuwa na £ 150. Barua hiyo ilikuwa imeandikwa na JOHN WILSON wa PARKSIDE, DERRY HILLS, CALNE, WITS, UK ikimtaka Bw. ZANGIRA atafute na kumpa habari juu ya namna uhusiano kati ya China na Tanzania unavyoharibu uhusiano wa Tanzania na majirani. Pia ilimtaka aeleze kuhusu vyama vya ukombozi ambavyo makao yake makuu yako Dar Es Salaam. Aidha, ilimtaka kutotumia jina lake halali na kwamba atalipwa £ 150 kwa mwezi na akileta habari zaidi ataongezewa.

Nyumba ya Bw ZANGIRA ilisachiwa na kisha ofisi yake nayo ilisachiwa ambapo zilipatikana barua 33. Barua zote hizo zilipokelewa mahakamani kama vithibiti.

Barua ya kwanza kuandikwa iliandikwa tarehe 29.11.1971 na ikafuatiwa na zingine tarehe 18.2.1972, 29.2.1972, 11.3.1972, 25.3.1972 na 12.4.1972. Barua hizo zilizungumzia mambo mbalimbali ya ujasusi huku zikionesha ZANGIRA alitumiwa £485.

Aidha, baadhi ya barua hizo zilitoa pongezi kwa Bw ZANGIRA kwa kazi nzuri anayofanya na zingine zilimlaumu baada ya kukaa kimya kwa kipindi kirefu. Pia, Bw ZANGIRA alitakiwa kutoa taarifa kuhusu mambo ya OAU na ziliko kambi za wapigania uhuru hapa nchini na kuulizia iwapo Rais NYERERE alikuwa akipendwa na wapigiania uhuru na ni nani nchini angekuja kuchukua nafasi yake.

Bw ZANGIRA alitakiwa pia kutoa taarifa kuhusu ofisi zote za ubalozi na maeneo zilipo na ni zipi zinawaunga mkono Wapigania uhuru. Barua hizo pia zilionesha alikuwa akipokea fedha mara kwa mara na aliwahi kumwandikia Bw. JOHN WILSON akimtaka ampe fedha za kujenga nyumba na kununulia gari kwani alikuwa amefanya kazi kubwa ya kupeleka taarifa hizo nyeti na alijibiwa kwamba apeleke "Account No." yake na avute subira. Mwisho, barua zilionesha alisafiri kwenda Kenya (22.7.1974) na Chileke, Malawi(7.4.1976) ambako alitajiwa na JOHN WILSON hoteli za kufikia na watu wa kukutana nao.

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa mfululizo kwa siku 4 na upande wa mashtaka kufunga kesi yao, Ijumaa, tarehe 30.9.1977 ikawa zamu ya Bw ZANGIRA kutoa utetezi wake.

Mh NYALALI alimueleza kwamba anayo haki ya kujitetea baada ya kula kiapo ambapo akimaliza kujitetea ataulizwa maswali au anaweza kuchagua kutoa utetezi bila kuapa ambapo hataulizwa swali na Jaji NYALALI, DPP Meela wala Wazee wa Baraza.

Bw ZANGIRA alichagua kutoa utetezi bila kuapa, hivyo hakuulizwa maswali.

Katika utetezi wake, Bw ZANGIRA alikiri kuwa barua hizo zote ni zake na kwamba ni kweli alikuwa akimpelekea habari Bw JOHN WILSON ila alifanya hivyo kama mwandishi wa habari kwani habari hizo zilikuwa ni za kawaida tu na zilipatikana magazetini. Aidha, alidai kwamba habari alizokuwa akituma zilikuwa za mambo ya biashara tu.

Bw ZANGIRA alieleza zaidi kwamba zamani alikuwa akifanyakazi Subuzani Tours & Safaris, Arusha ambapo kazi yake ilikuwa kuwapeleka watalii mbugani.

Alieleza kuwa mwanzoni mwa 1971 alifanya kazi ya kumpeleka mtalii mmoja aitwae WILTSHIRE mbuga ya Mikumi. Bw WILTSHIRE alimwambia kuwa ana rafiki yake yuko UK anatafuta mwandishi hivyo yeye akasema yuko tayari hivyo akampa Bw WILTSHIRE "Contacts" zake. Baada ya miezi michache ndipo alipoanza kupokea barua toka kwa JOHN WILSON.

Bw ZANGIRA alieleza kwamba alikuwa akilipwa kwa habari zote alizokuwa akizipeleka toka 1971 hadi 1977 na kwamba alipigwa bumbuwazi aliposhtukia anakamatwa asubuhi ya tarehe 29.7.1977 mara tu baada ya kuchukua barua kwenye sanduku lake la posta toka kwa JOHN WILSON.

Baada ya ZANGIRA kutoa utetezi wake, Jaji NYALALI aliwaeleza kwa kifupi wazee wa Baraza mlolongo wote wa kesi hiyo ili waweze kutoa maoni yao. Baada ya hapo, Wazee hao wa Baraza walitoa maoni yao ambapo wawili (SIMBA SALUM na HUSSEIN HAMIS waliona mashtaka yamethibitishwa wakati Mzee ZUBERI ALLY aliona mashtaka hayakuthibitishwa).

Mh NYALALI akaahirisha kesi hiyo na kuahidi kutoa hukumu Jumatano ya tarehe 5.10.1977. Siku hiyo, tofauti na ilivyokuwa siku ya kwanza, umati mkubwa ulifurika Mahakamani hapo kuanzia saa moja asubuhi na ulinzi ulikuwa umeimarishwa vilivyo.

Mh. NYALALI aliisoma hukumu hiyo ambapo alimtia hatiani Bw ZANGIRA kwa makosa yote 3 aliyoshtakiwa nayo. Mh NYALALI alisema:

"JOHN WILSON alikuwa ni Jasusi aliyekuwa akitumiwa na mataifa fulani ili kuangamiza usalama wa Taifa letu. Utetezi wa Bw ZANGIRA kwamba alikuwa anamtumia WILSON habari za biashara hauna mashiko. Hizo habari hazikuwa za kumfaa Mfanyabiashara yeyote bali Haini SMITH na Kaburu VOSTER wa Afrika ya Kusini. Vilevile, kama ni habari za biashara ni kwanini ZANGIRA atakiwe kutumia jina bandia?. Tanzania ni moja ya nchi zilizo mistari wa mbele Kusini mwa Afrika hivyo kitendo cha ZANGIRA kutoa siri za vyama hivyo na za OAU ni sawa na Uhaini".

Baada ya kutiwa hatiani, DPP MEELA aliiomba Mahakama imwadabishe Bw ZANGIRA kwa kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine hasa ukizingania umuhimu wa Tanzania katika ukombozi kusini mwa Afrika.

Nae MKUDE, wakili wa ZANGIRA, aliiomba Mahakama imuhurumie mteja wake kwani hilo ni kosa lake la kwanza na anategemewa na nduguze.

Mh NYALALI, baada ya kusikiliza "Aggravating & Mitigating factors" hizo, alitafakari kwa kina kisha akamuhukumu Bw ZANGIRA kwenda jela miaka 20.

Huyo ndiye JUMA THOMAS ZANGIRA, Mtanzania wa kwanza kushtakiwa na kutiwa hatiani kwa ujasusi.
 
Huyu Juma Thomas Zangira alikuwa mtu wa intelligence miaka ya mwanzo ya Uhuru wetu wa Bendera, na alikuwa karibu sana na Oscar Kambona. Alikuja kufungwa baadae na alipotoka ndio akawa na kibarua pale Kilimanjaro Hotel enzi hizo.
 
Miaka ya 1975 na kuendea kuna na kesi ya aliyekuwa mfanyakazi wa Kilimanjaro hotel akiitwa Juma Thomas Zangira. Huyu bwana alishtakiwa kwa kesi ya Ujasusi. Ninaomba anayeijua mwisho wa kesi hiyo na huyu bwana yuko wapi atujuze.

Nipo ! Choka mbaya Kilimanjaro hotel nilinyimwa mafao yangu kwa hila, kwa sasa nipo kijijini Mzenga nasota
 
Hivi wakuu maana halisi ya ujasusi huwa ni nini? Ujambazi au uajngiri au ukibaka? Pia tofauti ya jasusi na gaidi.
Jasusi, au mamajusi ni wapelelezi wanaotumwa toka nchi moja kwenda nchi nyingine kwa nia ya kukusanya habari fulani. Kwenye Biblia Herode aliwatuma mamajusi (majasusi) kwenda kuchunguza habari za kuzaliwa yesu (Mathayo 2 kuanzia mstari wa 7 na kuendelea). Mamajusi na majasusi ni neno lenye maana moja ila lahaja ni tofauti. Kwa tafsiri hiyo hapo juu, huyo Zangira hakustahili kuitwa jasusi. Bali alikuwa akishirikiana na jasusi (kama ni kweli lakini). Sababu yeye Zangira alikuwa nchini mwake, hakuwa nchi nyingine.
 
*JUMA THOMAS ZANGIRA: MTANZANIA WA KWANZA NCHINI KUSHTAKIWA KWA UJASUSI!!!*

Moja kati ya kesi kubwa za kihistoria nchini Tanzania ni ile kesi ya UJASUSI(ESPIONAGE) iliyomhusu Bw. JUMA THOMAS ZANGIRA ambayo ilirindima nchini mwaka 1977. Hii ilikuwa ni kesi ya aina yake iliyowaacha wananchi wakiwa hawaamini maskio yao kwani hii ilikuwa ni kesi ya kwanza ya ujasusi nchini.

Siku ya Jumapili, tarehe 25.9.1977, Radio Tanzania Dar Es Salaam, katika taarifa yake ya habari saa mbili usiku, ilieleza kwamba Bw ZANGIRA atapelekwa mahakamani kesho yake, jumatatu. Hata hivyo, RTD haikutaja atapelekwa mahakama ipi. Kwavile wananchi walizoea kwamba washtakiwa wa makosa ya jinai hupelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jumatatu asubuhi watu wengi walijazana mahakamani hapo kujionea wenyewe Mshtakiwa ZANGIRA yukoje na kusikiliza alifanya vipi ujasusi huo.

Hata hivyo, wananchi hao waliula wa chuya kwani kisheria Ujasusi ni kosa kubwa ambalo ni lazma lisikilizwe na Mahakama Kuu na lazma wawepo Wazee wa Baraza kumsaidia Jaji kama yalivyo makosa mengine makubwa kama vile mauaji au uhaini . Ni kwasababu hiyo basi, Bw. ZANGIRA, jumatatu ya tarehe 26.9.1977 alifikishwa Mahakama Kuu, na si Kisutu, toka gereza la Ukonga akiwa amefungwa pingu chini ya ulinzi mkali.

Kutokana na upekee wa kesi hii, ilibidi Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini(DPP) aiendeshe mwenyewe badala ya Mawakili wa Selikali walio chini yake. Aidha, kutokana na ukweli kwamba kesi hiyo ilikuwa ni ya aina yake, ikabidi isikilizwe na Jaji Mkuu, Mh. FRANCIS NYALALI mwenyewe. Mh. NYALALI alisaidiwa na wazee wakati wa Baraza ambao ni Bw. ZUBEIR ALLY, Bw. HUSSEIN ZAMANI na Bw. SIMBA SALUM. Kesi hiyo iliendeshwa kwa kasi ambapo ndani ya siku 10 tu hukumu ikatolewa.

Siku hiyo ya kwanza saa 3 asubuhi, DPP MEELA alimsomea Bw. ZANGIRA mashtaka 3:

Shtaka la 1 lilikuwa ni kukusanya habari kisha kuzitoa kwa mzungu aishie Uingereza aitwaye JOHN WILSON kwa nia ya kuvuruga usalama wa nchi yetu na kwamba taarifa hizo zingeweza kutumiwa na mataifa ya nje yanayoichukia Tanzania kuvuruga usalama wa nchi. Kosa la 2 ni kumpatia Bw JOHN WILSON habari ambazo zingeharibu jitihada za TANU na vyama vya ukombozi vya SWAPO, FRELIMO, PAC, ANC na ZANU na kosa la 3 ni kutoa taarifa za OAU kwa JOHN WILSON. Mashtaka haya yote matatu yalidaiwa ni kinyume na Kifungu cha 9(1)(a) na 9(2)(1) vya Sheria ya Usalama wa Taifa, 1970.

Mshtakiwa ZANGIRA, aliyekuwa akitetewa na wakili THOMAS MKUDE wa lililokuwa Shirika la Sheria Nchini (TLC), alikana mashtaka yote hayo 3 ambayo ilidaiwa aliyatenda kati ya mwaka 1971 na Julai 1977.

DPP, ambaye aliileza Mahakama kwamba Bw. ZANGIRA ni Afisa Uhusiano wa hoteli ya Kilimanjaro aliyekuwa pia Afisa Usalama wa Taifa, aliita mashahidi 8.

Shahidi wa kwanza alikuwa ni SASP ALI JUMA GUGURU. Kwa ujumla, maelezo ya mashahidi hao 8 yalikuwa ni kwamba tarehe 27.7.1977, Bw GUGURU alipokea habari za ujasusi na akamtuma Sajin ABDALLAH kuchunguza nani anatumia sanduku la posta 3900 DSM. Sajin ABDALLAH akatumia mbinu za medani na kugundua kwamba anayelitumia si mwingine bali ni Bw. ZANGIRA hivyo wakaanza kumfwatilia nyendo zake kwa karibu .

Siku tatu tu baadaye, yaani tarehe 29.7.1977, saa 2 asubuhi, Bw ZANGIRA aliondoka nyumbani kwake akawa anaenda "mdogomdogo" ofisini kwake kwa kupitia posta bila kujua kuwa alikuwa anafanyiwa "surveillance" kali ya nyendo zake!.

Bw. ZANGIRA alipofika posta akafungua sanduku lake la barua na kutoa barua moja aliyoikuta. Kufumba na kufumbua akanyakwa na polisi!

Bw. ZANGIRA alikiri kuwa barua hiyo ni yake na ilipofunguliwa ilikuwa na £ 150. Barua hiyo ilikuwa imeandikwa na JOHN WILSON wa PARKSIDE, DERRY HILLS, CALNE, WITS, UK ikimtaka Bw. ZANGIRA atafute na kumpa habari juu ya namna uhusiano kati ya China na Tanzania unavyoharibu uhusiano wa Tanzania na majirani. Pia ilimtaka aeleze kuhusu vyama vya ukombozi ambavyo makao yake makuu yako Dar Es Salaam. Aidha, ilimtaka kutotumia jina lake halali na kwamba atalipwa £ 150 kwa mwezi na akileta habari zaidi ataongezewa.

Nyumba ya Bw ZANGIRA ilisachiwa na kisha ofisi yake nayo ilisachiwa ambapo zilipatikana barua 33. Barua zote hizo zilipokelewa mahakamani kama vithibiti.

Barua ya kwanza kuandikwa iliandikwa tarehe 29.11.1971 na ikafuatiwa na zingine tarehe 18.2.1972, 29.2.1972, 11.3.1972, 25.3.1972 na 12.4.1972. Barua hizo zilizungumzia mambo mbalimbali ya ujasusi huku zikionesha ZANGIRA alitumiwa £485.

Aidha, baadhi ya barua hizo zilitoa pongezi kwa Bw ZANGIRA kwa kazi nzuri anayofanya na zingine zilimlaumu baada ya kukaa kimya kwa kipindi kirefu. Pia, Bw ZANGIRA alitakiwa kutoa taarifa kuhusu mambo ya OAU na ziliko kambi za wapigania uhuru hapa nchini na kuulizia iwapo Rais NYERERE alikuwa akipendwa na wapigiania uhuru na ni nani nchini angekuja kuchukua nafasi yake.

Bw ZANGIRA alitakiwa pia kutoa taarifa kuhusu ofisi zote za ubalozi na maeneo zilipo na ni zipi zinawaunga mkono Wapigania uhuru. Barua hizo pia zilionesha alikuwa akipokea fedha mara kwa mara na aliwahi kumwandikia Bw. JOHN WILSON akimtaka ampe fedha za kujenga nyumba na kununulia gari kwani alikuwa amefanya kazi kubwa ya kupeleka taarifa hizo nyeti na alijibiwa kwamba apeleke "Account No." yake na avute subira. Mwisho, barua zilionesha alisafiri kwenda Kenya (22.7.1974) na Chileke, Malawi(7.4.1976) ambako alitajiwa na JOHN WILSON hoteli za kufikia na watu wa kukutana nao.

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa mfululizo kwa siku 4 na upande wa mashtaka kufunga kesi yao, Ijumaa, tarehe 30.9.1977 ikawa zamu ya Bw ZANGIRA kutoa utetezi wake.

Mh NYALALI alimueleza kwamba anayo haki ya kujitetea baada ya kula kiapo ambapo akimaliza kujitetea ataulizwa maswali au anaweza kuchagua kutoa utetezi bila kuapa ambapo hataulizwa swali na Jaji NYALALI, DPP Meela wala Wazee wa Baraza.

Bw ZANGIRA alichagua kutoa utetezi bila kuapa, hivyo hakuulizwa maswali.

Katika utetezi wake, Bw ZANGIRA alikiri kuwa barua hizo zote ni zake na kwamba ni kweli alikuwa akimpelekea habari Bw JOHN WILSON ila alifanya hivyo kama mwandishi wa habari kwani habari hizo zilikuwa ni za kawaida tu na zilipatikana magazetini. Aidha, alidai kwamba habari alizokuwa akituma zilikuwa za mambo ya biashara tu.

Bw ZANGIRA alieleza zaidi kwamba zamani alikuwa akifanyakazi Subuzani Tours & Safaris, Arusha ambapo kazi yake ilikuwa kuwapeleka watalii mbugani.

Alieleza kuwa mwanzoni mwa 1971 alifanya kazi ya kumpeleka mtalii mmoja aitwae WILTSHIRE mbuga ya Mikumi. Bw WILTSHIRE alimwambia kuwa ana rafiki yake yuko UK anatafuta mwandishi hivyo yeye akasema yuko tayari hivyo akampa Bw WILTSHIRE "Contacts" zake. Baada ya miezi michache ndipo alipoanza kupokea barua toka kwa JOHN WILSON.

Bw ZANGIRA alieleza kwamba alikuwa akilipwa kwa habari zote alizokuwa akizipeleka toka 1971 hadi 1977 na kwamba alipigwa bumbuwazi aliposhtukia anakamatwa asubuhi ya tarehe 29.7.1977 mara tu baada ya kuchukua barua kwenye sanduku lake la posta toka kwa JOHN WILSON.

Baada ya ZANGIRA kutoa utetezi wake, Jaji NYALALI aliwaeleza kwa kifupi wazee wa Baraza mlolongo wote wa kesi hiyo ili waweze kutoa maoni yao. Baada ya hapo, Wazee hao wa Baraza walitoa maoni yao ambapo wawili (SIMBA SALUM na HUSSEIN HAMIS waliona mashtaka yamethibitishwa wakati Mzee ZUBERI ALLY aliona mashtaka hayakuthibitishwa).

Mh NYALALI akahairisha kesi hiyo na kuahidi kutoa hukumu Jumatano ya tarehe 5.10.1977. Siku hiyo, tofauti na ilivyokuwa siku ya kwanza, umati mkubwa ulifurika Mahakamani hapo kuanzia saa moja asubuhi na ulinzi ulikuwa umeimarishwa vilivyo.

Mh. NYALALI aliisoma hukumu hiyo ambapo alimtia hatiani Bw ZANGIRA kwa makosa yote 3 aliyoshtakiwa nayo. Mh NYALALI alisema:

*"JOHN WILSON alikuwa ni Jasusi aliyekuwa akitumiwa na mataifa fulani ili kuangamiza usalama wa Taifa letu. Utetezi wa Bw ZANGIRA kwamba alikuwa anamtumia WILSON habari za biashara hauna mashiko. Hizo habari hazikuwa za kumfaa Mfanyabiashara yeyote bali Haini SMITH na Kaburu VOSTER wa Afrika ya Kusini. Vilevile, kama ni habari za biashara ni kwanini ZANGIRA atakiwe kutumia jina bandia?. Tanzania ni moja ya nchi zilizo mistari wa mbele Kusini mwa Afrika hivyo kitendo cha ZANGIRA kutoa siri za vyama hivyo na za OAU ni sawa na Uhaini"*.

Baada ya kutiwa hatiani, DPP MEELA aliiomba Mahakama imwadabishe Bw ZANGIRA kwa kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine hasa ukizingania umuhimu wa Tanzania katika ukombozi kusini mwa Afrika.

Nae MKUDE, wakili wa ZANGIRA, aliiomba Mahakama imuhurumie mteja wake kwani hilo ni kosa lake la kwanza na anategemewa na nduguze.

Mh NYALALI, baada ya kusikiliza "Aggravating & Mitigating factors" hizo, alitafakari kwa kina kisha akamuhukumu Bw ZANGIRA kwenda jela miaka 20.

Huyo ndiye JUMA THOMAS ZANGIRA, Mtanzania wa kwanza kushtakiwa na kutiwa hatiani kwa ujasusi.
 
Miaka ya 1975 na kuendea kuna na kesi ya aliyekuwa mfanyakazi wa Kilimanjaro hotel akiitwa Juma Thomas Zangira. Huyu bwana alishtakiwa kwa kesi ya Ujasusi. Ninaomba anayeijua mwisho wa kesi hiyo na huyu bwana yuko wapi atujuze.
Mayalla kama ulikuwa unapendelea kufuatilia kesi unikumbushe kesi ya MTU mmoja anaitwa
(1) Thomas Nzangira alikamatwa kwa kesi ya uhaini kama sio ujasusi nimesahau
(2) dereva taxi muhando aliyewachomekea kesi kina maghee alikuwa anapaki taxi yake Kilimanjaro hotel
Yes nilikuwa napenda kufuatilia kesi, hiyo kesi ya uhaini ya Juma Thomas Zangira pia niliifuatilia.
Ilizungumzwa hapa na humu kuna nyuzi nyingi tuu za kesi hii,
Pamoja Na Ufisadi Wake Wote, Chenge is One of Best Brains Kwenye Bunge Full of Ignorants - JamiiForums

Kesi yenyewe kamili imeripotiwa hapa
Juma Thomas Zangira: Mtanzania wa kwanza kushitakiwa kwa ujasusi - JamiiForums

P
 
Back
Top Bottom