Juma mkambi-general afariki dunia

Mshambuliaji mahiri wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa Stars Juma Mkambi 'Jenerali' amefariki alfajiri ya leo...Marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo kwa takribani wiki mbili sasa na atazikwa katika hospitali ya Tumbi Kibaha kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.....Habari zadi juu ya mazishi yake tutajuzana....R.I.P Jenerali JUMA MKAMBI
R. I. P jenerali, hii ni habari ya kusikitisha sana, hapo kwenye nyekundu bado sijaelewa, nadhani umekusudia aliugulia hospitali ya Tumbi na baadae kuhamishiwa Muhimbili ila wapi mazishi bado hauna habari, ama sivyo Mkuu?
 
Mshambuliaji mahiri wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa Stars Juma Mkambi 'Jenerali' amefariki alfajiri ya leo...Marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo kwa takribani wiki mbili sasa na atazikwa katika hospitali ya Tumbi Kibaha kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.....Habari zadi juu ya mazishi yake tutajuzana....R.I.P Jenerali JUMA MKAMBI
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
Surely we belong to Allah and to Him shall we return

Marehemu Juma Mkambi (wa kwanza shoto waliochuchumaa) akiwa na
kikosi cha Yanga wakati wa fainali za Super Cup mwaka 1981.

Nimehuzunika kupata habari za kifo cha J. Mkambi "HOMA YA JIJI". Pamoja na kwamba umri wa kucheza ulishapita lakini wapenzi wasoka walikuwa bado wanamhitaji kwani alikuwa na hazina ya utaalamu katika soka. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amen
 
Oh! sorry nimekosea yeye hakuwa HOMA ya JIJI, nimemchanganya na Makumbi juma. Samahani kwa usumbufu. Yeye alikuwa akijulikana kwa "GENERALI".
 
Mazishi yake yatafanyika leo katika makaburi ya Kisutu mjini Dar es Salaam.

'Jenerali' Juma Mkambi tutamkumbuka kama kiungo katika kikosi pekee cha Taifa Stars katika historia ya Tanzania kupata kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (then, Kombe la Mataifa Huru ya Afrika) nchini Nigeria mwaka 1980.

Amefariki akiwa na miaka 55.
 
bado naukumbuka ule usemi maarufu wa juma mkambi

juma mkambi is very fantastic, agenda musix agenda mueight, juma mkambi agenda agenda na kushuti gooooooooooooooo

msemo maarufu wa kumtambulisha kiungo mahiri wa watani

kumbuka amecheza miaka yote young africans tangu kids, yanga b hadi wakubwa, utaratibu mzuri kabisa ulioanzishwa na tambwe leya, then victor stanculescu lakini ambao umetoweka siku hizi
 
Back
Top Bottom