kapotolo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2010
- 3,727
- 2,214
Wazir wa Afya (siha) wa Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar ndugu Juma Duni Haji akihojiwa katika kipindi cha Saa ya Hamza Kasongo (Hamza Kasongo Hour) cha channel 10 alisema mkutano wa 8 wa CCM huko Dodoma ulikuwa na lengo moja la kuwaunganisha wana CCM kwa lengo la kushinda Uchaguzi wa 2015 lakini si kujenga chama cha kutumikia wananchi.
Alisema wamegundua kwa mgawanyiko uliopo ndani ya chama hawataweza kushinda uchaguzi. Hawana nia ya dhati ya kutumikia wananchi, na hizi ziara zao mikoani ni danganya toto ndio maana hata baadhi ya mawaziri wameanza kuzikwepa.
Ndugu Duni alitumia fursa hiyo pia kuzungumzia uhuru wa Zanzibar na kuwaomba wazanzibar waliopewa vyeo wasikubali kuwa na akili za samaki kwani hivyo vyeo ni chambo kitakachowanasa kwenye mtego wa kushindwa kuitetea Zanzibar yao.
Pia alikanusha vikali CUF kuhusishwa na uamsho na akamtetea pia Rais mstaafu Amani Abeid Karume kuhusu kuhusishwa kwake na uamsho na akatoa tafsiri tano za nini alikimaanisha Rais Karume alipowaambia wanzanzibari wasiwe na akili kama za samaki.
Moja ya tafsiri hizo ni kukubali kumeza chambo na ndoana za vyeo kwenye serikali ya muungano na kushindwa kutetea Uzanzibari.