Juma Duni Aunguruma:Ahoji Kila Wananchi Wakiwa Masikini Zaidi Ndiyo Wachaguwe CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Juma Duni Aunguruma:Ahoji Kila Wananchi Wakiwa Masikini Zaidi Ndiyo Wachaguwe CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Sep 30, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Akiongea na BBC Juma Duni Haji "Babu" amesema wameshinikiza tume huru ya uchaguzi na katiba mpya kwa kuwa iliyopo inafanya kazi kama kamati ya CCM kwa kukipendelea chama hicho kikongwe.
  Duni akiongea kwa "points" amesema kuwa hata katiba ya nchi iliyopo sasa bado inaegeamea mfumo wa kizamani wa chama kimoja.
  "...tume iliyopo sasa haikidhi matakwa ya mfumo wa vyama vingi kwa kushindwa kusimamia majukumu yake kwa uadilifu..." alisema Duni.
  Aliongeza kuwa katika chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibu kumekuwa na dosari kubwa hasa idadi ya wananchi wanaojitokeza katika kupiga kura ni tofauti na ile ya wale walioandikishwa kwa kutofikia hata nusu.
  "...hii inaonyesha udhaifu mkubwa kwa tume ya uchaguzi... na sisi tukiomba tuonyeshwe daftari tume haitaki kwa kudai kuwa ni kazi zao, tukiwauliza kwa nini idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ni chini ya nusu ya walioandikishwa tume haiotoi jibu.." alihoji "babu" Duni.
  Naye Katibu Mwenezi wa chama cha Mapinduzi, Capt. John Chiligati amesema kuwa wapinzani wasitafute mchawi bali watumie muda huu kufanya mambo ya maana zaidi kujiimarisha.
  "...ningekuwa mimi ndo Rais Kikwete ningewaingiza wapinzani wote katika tume ya uchaguzi na bado CCM ingeshinda tu..." alisema Chiligati kwa kujilabu.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mimi nahisi watanzania labda wana matatizo ya afya ya akili au umasikini umedumaza fikra zao kiasi kuwa hata wakionewa vipi wao ni amani tu, hata wakiibiwa shilingi ngapi poa tu, hata wakidharauliwa vipi wao kidumu tu, hata wakidanganywa vipi wao wanachukuwa wanaweka waaaaa, mradi watanzania wapenda amani tuuu hata ukiwanajisi na kuwa chezea chezea nanihii zao o.k yaani watanzania ni watu wa ajabu hakuna mfano wao popote duniani. Hongereni sana wachache kati yenu wanafikiri kama ninavyofikiri mimi kuwa CCM si chama chenye matumaini yoyote nasema tena yoyote nasisitiza yoyote kwa mtu masikini wa nchi hii, anaekataa na akatae huo ndo ukweli.
   
 3. L

  Lampart Senior Member

  #3
  Oct 1, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nd. Junius,
  >Hongereni sana wachache kati yenu wanafikiri kama ninavyofikiri mimi
  <

  Hakuna hata mmoja kati yetu anaefikiri kama wewe. Sasa unatueleza nini hapa juu? Zaidi naona unalaumu tu. Kulaumu kila mtu anaweza.
  Hao unaowategemea wote walikuwa CCM na wote ni wasaliti kama alivyotueleza Nd. Wazanganyika, lakini walipoona kula yao imekatwa ndio wakapiga kambi kwengine.
  Don't underestimate Tanzanians. Umeona walifanya nini tarehe 12 January, 1964? That was the first people's revolution in Africa!
   
 4. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tueleze yakhe!!! ni chama kipi..............usemacho wewe kina matumini? zaidi ya CCM- Tutakupa hoja hapa jamvini.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ahsante Chiligati inafaa ugombee Uraisi yaani hapo umeshampiku Kikwete na inaonyesha umahiri wako na kujiamini na vilevile unaonyesha ushujaa wa kujiamini jambo ambalo ndilo haswa linalotafutwa .kila Chama kijiamini kikamilifu ,ili uwekwe uchaguzi wa aina yake hapa duniani.

  Yaani kama ni mtaji wa kiutawala basi Chiligati huo wako umetimia kabisa na hauna kasoro hata chembe ,nasema huko ni kujiamini kunakotakiwa kwa Chama Tawala ,kwa maana hiyo kama Tume ya uchaguzi itasoma maoni yako basi itabidi ijiuzulu mara moja ,ili kutekeleza hilo analolidai Chiligati ,tuone na kujua lipi bichi na lipi limeiva.
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mm nafikiri hivi ili tupige hatua moja mbele ya matumaini basi tunahitaji mabadiliko ya mfumo wa utawala (system) ambao kama utabakia hivi ulivyo sasa basi "maisha bora" yatakuwa kwa "wanene" tu "wenda miayo" tutabaki kujitafuna ulimi mpaka tufe.
  Hayo ya 12 Jan, ni mizugo ya akili uliyozugwa ukiamini kuwa ilifanywa kukusaidia ww nambie umefika wapi mpaka sasa, nani anamaisha bora kati ya hao waliofanya hayo na ww? mara ngapi wameshakufanya ww ngazi ya kupandia madarakani na kujineemesha wao na watu wao wakikubakisha ww ndo mkanda wa kurekodia uwongo wao wanaouita sera kila baada ya miaka mitano, nawe hujijuwi bila ya kujali yaliyopita yametekelezwa au la unakubali ahadi mpya mpya kila chaguzi, ndgu haya unayafikiria au ndo na kidumu tu kwa shibe zao na shida zako ww basi si lazima!
  Ukimuona mtu anaepuka matatizo ujuwe ndo hayataki na yeshamchosha ndiyo maana hao waliohama CCM kwenda upinzani si jengine kwa sbabu ya mabadiliko tu na hilo ni jambo la kawaida si lazima kuwa waje watu kutoka sayari nyengine wafanye upinzani.Upo.
  Iwapo utanambia ni matumaini yepi watanzania tuwenayo au tusubiri yatazaa matunda baada ya miaka 45 ya kila kitu kutoka CCM ambayo tusitegemee kutoka chama chengine chochote isipokuwa CCM?
   
Loading...