Julius s. Mtatiro: "Njaa siyo pepo ,haiondoki kwa kukemewa"

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
Rais wetu ashauriwe upya juu ya msimamo wake kuhusu maeneo yenye njaa. Mkoani Mara, baba yangu amekuwa akilima zaidi ya ekari 10 za Mahindi kwa miaka 4 mfululizo, ni hasara tupu. Hakuna mavuno kwa sababu hakuna mvua za kuhimili misimu ya kilimo. Na hata wakulima wakifuata majira ya mvua "wanaingia mkenge", hayafuatiki, hayaeleweki na hayatabiriki.

Gunia la Mahindi mkoani Mara ni wastani wa Shilingi 100,000 kwa sasa. Gunia la Muhogo na Mtama ni wastani wa Shilingi 62,500. Hali hii ina maana Wakuu wa Wilaya hawana miujiza ya kutekeleza amri ya mkuu ya kuondoa njaa kirahisi. Tatizo la ukosefu na upungufu wa chakula linakua kubwa kila uchwao kwa sababu kadhaa;

[HASHTAG]#Mojawapo[/HASHTAG] ni Mvua kutonyesha kwa sababu tumekata miti yote, tunaendelea kuikata na hatuna mpango mahsusi wa kupanda miti.

[HASHTAG]#Sababu[/HASHTAG] ya pili ni kukosekana kwa mipango yoyote ya kukuza kilimo cha umwagiliaji, kama hitaji la kilimo cha umwagiliaji wa kisasa ni asilimia 100, Tanzania tumeweza chini ya asilimia moja.

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG] ni suala la kipaumbele cha kilimo, kilimo kimesahaulika na kutupwa mbali kabisa. Ni mhimili wa maisha kwa asilimia 70 ya Watanzania wote lakini hadi sasa kinachangia asilimia chini ya 3 ya pato la taifa.

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG], serikali ya awamu ya sasa haina kipaumbele cha kitu kiitwacho kilimo, awamu hii ni viwanda ambavyo haieleweki vitaimarishwa namna gani bila kujengwa juu ya msingi wa kilimo.

[HASHTAG]#Tano[/HASHTAG], bado hadi sasa sehemu kubwa ya Wakulima wanatumia jembe la mkono, sawa na enzi za Ujima. Jembe hilo halifui dafu utoshelezaji wa chakula kutokana na ongezeko kubwa la watu.

Rais wetu akumbushwe suala la njaa ni mtambuka na halitatatuliwa kwa amri tu, linahitaji mipango ya muda,mrefu, uwekezaji wa trilioni za shilingi na utashi mkubwa wa kisiasa wa serikali yake na zijazo.
 
Ngoja wananchi wa Chato waandamane kudai chakula labda rais anaweza kuamka usingizini.
Kwa sasa ukitaka rais akurupuke kutatua tatizo lolote lile basi wewe omba hilo tatizo litokee kwanza Chato au Geita.
 
Msimu wa Kilimo wa 2016/17 si mzuri sana kwani maeneo mengi hapa nchini ni makame sana. Mvua hazijanyesha kwa wakati na hata zilikonyesha zimenyesha kidogo sana.
Na kama mvua hazitanyesha kwa kipindi hiki basi tutarajie madhara makubwa zaidi ya haya tunayoyaona sasa.
Tumwombe Mungu atuepushe na hili janga.
 
Ninachokiamini Mimi MUNGU aliwapa hekma wapinzani.walianza na MUNGU wakamaliza na MUNGU,kila likitokea janga ccm wanasema hawajalileta wao ok tunakubali ila AMANI KWENYE NJAA HAIDUMU..
 
Rais wetu ashauriwe upya juu ya msimamo wake kuhusu maeneo yenye njaa. Mkoani Mara, baba yangu amekuwa akilima zaidi ya ekari 10 za Mahindi kwa miaka 4 mfululizo, ni hasara tupu. Hakuna mavuno kwa sababu hakuna mvua za kuhimili misimu ya kilimo. Na hata wakulima wakifuata majira ya mvua "wanaingia mkenge", hayafuatiki, hayaeleweki na hayatabiriki.

Gunia la Mahindi mkoani Mara ni wastani wa Shilingi 100,000 kwa sasa. Gunia la Muhogo na Mtama ni wastani wa Shilingi 62,500. Hali hii ina maana Wakuu wa Wilaya hawana miujiza ya kutekeleza amri ya mkuu ya kuondoa njaa kirahisi. Tatizo la ukosefu na upungufu wa chakula linakua kubwa kila uchwao kwa sababu kadhaa;

[HASHTAG]#Mojawapo[/HASHTAG] ni Mvua kutonyesha kwa sababu tumekata miti yote, tunaendelea kuikata na hatuna mpango mahsusi wa kupanda miti.

[HASHTAG]#Sababu[/HASHTAG] ya pili ni kukosekana kwa mipango yoyote ya kukuza kilimo cha umwagiliaji, kama hitaji la kilimo cha umwagiliaji wa kisasa ni asilimia 100, Tanzania tumeweza chini ya asilimia moja.

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG] ni suala la kipaumbele cha kilimo, kilimo kimesahaulika na kutupwa mbali kabisa. Ni mhimili wa maisha kwa asilimia 70 ya Watanzania wote lakini hadi sasa kinachangia asilimia chini ya 3 ya pato la taifa.

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG], serikali ya awamu ya sasa haina kipaumbele cha kitu kiitwacho kilimo, awamu hii ni viwanda ambavyo haieleweki vitaimarishwa namna gani bila kujengwa juu ya msingi wa kilimo.

[HASHTAG]#Tano[/HASHTAG], bado hadi sasa sehemu kubwa ya Wakulima wanatumia jembe la mkono, sawa na enzi za Ujima. Jembe hilo halifui dafu utoshelezaji wa chakula kutokana na ongezeko kubwa la watu.

Rais wetu akumbushwe suala la njaa ni mtambuka na halitatatuliwa kwa amri tu, linahitaji mipango ya muda,mrefu, uwekezaji wa trilioni za shilingi na utashi mkubwa wa kisiasa wa serikali yake na zijazo.
Sera ya kilimo imekuwaje,mmeona ndege itaokoa nchi,viwanda hewa subirini itaondoa njaa,hiki chama miaka 50 wanajuwa asilimia 65 hadi 70 wanatemea kilimo halafu shule ya msingi watoto hawafundishwi kilimo huku tukijua wengi wao watarudi kiwa wakulima,sasa njaa tutakosa?
 
Vipangaboi vitasafirisha mazao kutoka sehemu yenye Chakula kwenda maeneo yenye njaa
 
mtatiro ni jipu...inakuwaje baba yako analima na wwe una uwezo mkubwa....inaonekana wwe ni selfish....unawezaje kushughulikia matatizo ya watu baki wakati ya kwenu yamekushinda
 
Back
Top Bottom