Julius Nyerere: Siwezi kuacha nchi yangu iangukie mikononi mwa mbwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Julius Nyerere: Siwezi kuacha nchi yangu iangukie mikononi mwa mbwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, Apr 20, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwaka 1995 mwalimu Nyerere alisema, "I can't let my country go to the dogs, akimaanisha Augustine Mrema na NCCR-Mageuzi wakati ule.

  Maskini Nyerere hakujua kuwa nyumbani kwake walikuwa wamejaa mbwa tena kusiri!

  Miaka zaidi ya kumi tangu Nyerere ang'ake. Je Tanzania haikwenda kwa hao mbwa ambao wengi wao wamegeuka kuwa hata mchwa wakitafuna kila kitu hata takataka?

  Akina Benjamin Mkapa, Daniel Yona, Basil Mramba, Nazir Karamagi, Edward Lowassa, Mstapha Mkulo, Idd Simba, Ibrahim Msabaha, Cyril Chami, William Lukuvi, Anna Makinda, Samuel Sitta, Juma Ngatunga, Jakaya Kikwete, Ali Hassan Mwinyi ni nani jamani?

  Should we let our country fall in the hands of dogs or do something?
   
 2. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 3. E

  Emmanuel_mtui Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni muda, angekuwepo leo angekiri udhaifu, kwani kama hata hao aliowaona watu wakati huo leo wako wapi na wanfanya nini? Tumsamehe mzee yule alishazeeka tukomae na yetu,
   
 4. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MKUBHWA,

  NYERERE hakuwa anamaanisha MREMA peke yake. MWL alikuwa akimaanisha 'mbwa na vijiumbwa' ndani na nje ya CCM: REJEA (1) KITABU 'UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA'; (2) HOTUBA YA YAKE MEI 1, 2005; NA (3) HOTUBA KWA NEC CCM NA MKUTANO MKUU TAIFA CCM. MWL ALIHAKIKISHA WANATUTAWALA SASA NA WALIO NJE KAMA KINA JOHN SIGWEYAMISI ANAWATEKEKTEZA KISIASA.

  NI KWELI LAKINI, AKIFUFUKA ATAJILAUMU KWA KUTOA KAULI ILE KWANI ATAGUNGUA KUWA HATA WALE ALIOAMINI KUWA SI MBWA, KUMBE NDO MAMBWAMWITU!
   
 5. LOWE89

  LOWE89 Senior Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mbwa wanaosahau hata kunyonyesha watoto wao
   
 6. s

  shikulaushinye JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2015
  Joined: Aug 29, 2014
  Messages: 829
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 60
  'I cannot let my country go to the dogs' Hii ni kauli ambayo iliyowahi kutolewa na Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere mwaka 1995.

  Kesho tukienda kuadhimisha miaka 16 tangu atangulie mbele ya haki Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere.(R.I.P) Pia tukiwa na siku 12 kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, Ningependa tujadiri kauli hiyo hapo juu. Lakini pia tukumbuke Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayapata nje ya CCM.

  Pamoja na ushuri huu wa Baba wa taifa kwa CCM bado haikulichukulia jambo hili la mabadiriko kujisahihisha. Katika uchaguzi wa mwaka huu muungano wa vyama vya upinzani UKAWA umeibeba agenda hii ya mabadiliko na kujizolea wafuasi wengi, Baada ya kuona agenda hii itawasumbua viongozi wa CCM nao wamekimbia kuibebea juu kwa juu agenda hii, kiukweli haikuwa agenda ya CCM kwa sababu hata mikakati ya mabadiliko ndiyo wanaitafuta. Kama wangemsiliza muasisi wa CHAMA wasingepata shida wanazopata kwa sasa, tunamwonea huruma Mh. Magufuri shida anayopata kupambana na UKAWA wakiongozwa na Mheshimiwa LOWASSA ambaye awali alikuwa CCM. Kiukweli CCM wamejitakia wenyewe kwa kujiona wao ndiyo kila kitu kutosikia ushauri wa kiongozi na muasisi wa chama.

  CCM ILIKUWA NA NAFASI KUJISAHIHISHA NDANI YA MIAKA 10 LKN MAZOEA YALIWAATHIRI. MOJA YA KATI MAMBO YALIYO WATIA DOA NI HAYA HAPA:-
  · KASHFA YA EPA: watuhumiwa waliambiwa warudishe pesa badala ya sheria
  kuchukua mkondo wake.
  · UFISADI WA RICHMOND: watumiwa kuachiwa bila kuchukuliwa hatua
  stahiki, na mwenyekiti kusema eti kujiithuru kwa waziri mkuu Mh. LOWASSA
  ilikuwa ni ajari ya kisiasa.
  · UFISADI MEREMETA: Serikali ilisema ni jambo linalohusu usalama wan chi
  hivyo hairusiwi kuchunguzwa.
  · Kauri za baadhi ya viongozi kama zile za Mh. CHENGE kukutwa na bilioni moja
  nje ya nchi na kujibu eti ni vijisenti tu, Kauri ya Prof. Tibaijuka kuwa bilioni moja
  ilikuwa ni pesa ya mboga.
  · Kutojishughurisha na walioweka pesa nje ya nchi
  · Baadhi ya viongozi kujisahau na kujiona wao ni Miungu watu kuliko wananchi,
  utamwona kiongozi alikuwa wa kawaida tu lakini baada ya muda mfupi utaona
  mfumo wake wa maisha kubadirika ikiwa ni pamoja na gari la kifahari
  likining'iniza suti ndani km vile ndiyo makabati ya nyumbani.
  · KASHFA YA ESCROW: Rais aililichukulia powa tu jambo hili kwa kulichukulia
  kiitikadi zaidi badala ya kitaifa.

  Iwapo Rais Kikwete angeacha kufanya kazi kwa mazoea (BUSINESS AS USSUAL) akawafukuza kazi mara moja na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria basi CCM wasingepata upinzani wanaoupata sasa hivi.

  Ukweli ni kwamba serikali ya CCM ilijisahau sana, matokeo yake wananchi wana hasira sana lolote na liwe na sasa wanataka kuwakabidhi nchi MBWA au MBWEHA. Kwa kauli ya baba wa taifa mbwa ni nini, na wapo? Kama wapo ni akina nani?

  Kwa uelewa wangu mbwa ni wala rushwa, wapiga deal, wakola, wezi, wahuni, wanaopenda kujilimbikia mali, waroho na wenye uchu wa madaraka.
  R.I.P BABA WA TAIFA HAYATI MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE.
   
 7. MSHINO

  MSHINO JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2015
  Joined: Jul 26, 2013
  Messages: 856
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mkuu asante kwa post.
   
 8. MeinKempf

  MeinKempf JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2015
  Joined: Jun 11, 2013
  Messages: 11,027
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Hivi huu uzi kweli utapendwa na watawala ..?
  maana una choma choma kama miba flani hivi.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2015
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CCM hawana kizuri hata kimoja !
   
 10. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2015
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,431
  Likes Received: 81,504
  Trophy Points: 280
  Ngumu kumesa ngumu kutema ngumu kumumunya... Ccm moja haikai mbili haisomi
   
 11. MSHINO

  MSHINO JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2015
  Joined: Jul 26, 2013
  Messages: 856
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Inabidi kumeza tu.
   
 12. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2015
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  kifo cha Mende Chaaalliiiiiiiiii!!!!
   
 13. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2015
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,431
  Likes Received: 81,504
  Trophy Points: 280
  Ya moto sana
   
 14. maonomakuu

  maonomakuu JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2015
  Joined: Jul 24, 2015
  Messages: 2,511
  Likes Received: 967
  Trophy Points: 280
  MBWA Mkubwa ni CCM ndiyo mlezi wa MAUMBWA
   
 15. P

  PLEASE JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2015
  Joined: Nov 6, 2013
  Messages: 570
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  asante mtoa mada...mbwa wanataka kuchukua nchi kwa kisingizio cha mabadiliko....ccm mlaaniwe sana
   
 16. MSHINO

  MSHINO JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2015
  Joined: Jul 26, 2013
  Messages: 856
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hadi inatia hasira.
   
 17. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2015
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,100
  Likes Received: 11,251
  Trophy Points: 280
  CCM ndo "mbwa" aliokuwa anawaongelea Mwl. Nyerere.
   
 18. a

  aiai654 JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2015
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,861
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Mleta mada ni dalili nzuri umeanza kukubali kuwa nchi inakwenda. Na kwa usahihi ni kuwa mbwa wanawekwa kando
   
 19. Bwai

  Bwai JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2015
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 467
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 60
  Inasikitisha Sana, mtaani watu wanasema liwalo na liwe, viongozi acheni KIBURI.
   
 20. TL. Marandu

  TL. Marandu JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2017
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 3,561
  Likes Received: 5,508
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi wa Kwanza wa Vyama Vingi Tanzania 1995 Mwalimu Nyerere, alienda Dodoma kuhakiki zoezi la Kupatikana Mgombea wa Chama, Mwalimu Nyererealivyohojiwa na Waaandishi hasa ni Kwanini amejiyosa huko! Alijibu, ,"Siwezi kwenda Butiama Kulala Usingizi huku niache nchi yangu Ikichukuliwa na Mbwa!"

  Watu kwa makusudi walioyajua Mwenyewe wakadai ati Mwalimu Nyerere alimaanisha Wapinzani ni Mbwa! Wapinzani haikuwa sababu ya Mwalimu Kujitosa, Ila aliogopa Nchi kuangukia Mikononi mwa watu wenye Kiburi na Udictator! Mtu ambaye alimsema wazi ni anageuka mbogo anapohojiwa au Kushauriwa alikuwa ni John Samwel Malecela na Nyerere alimlazimisha aondoe jina lake kwenye list.

  Majina mengine galiondolewa kwa kuwa Nyerere alihisi walipingana sana na siasa ya Ujamaa, na Akahisi walikuwa na Tamaa ya Utajiri. Ingawa hawakuwa na hatia, Nyerere alihofia wakishinda watawasahau Masikini, Nao ni Msuya na Lowassa.

  Ila Sirudii kutaja Majina hapa! Mbwa kwa Nyerere alimaanisha Wenye hulka za Udictator na Kiburi. Mmoja alipoambiwa aondoe jina akawa Mjanja akanyamaza, hakubishana na Nyerere, Mwingine akabishana sana, akidai, "Nyerere ni Kiumbe na Mimi ni Kiumbe" Na baada ya Uchaguzi akaendelea Kusema, "CCM haina Dira wala Mwelekeo" Ingawa alikuwa ni Mtu Jasiri asiye na hofu, Akaitwa kuhojiwa ati mahojiano yale yakamtisha na kumpa mshituko wa moyo! Hatuko naye Tena!

  Je hofu ya Nyerere imekuja Kutimia yeye akiwa hayupo tena nasi?
   
Loading...