Julius Nyerere Intellectual Festival Week: 13 - 17 April 2009 - Nkrumah Hall, UDSM

Petu Hapa said:
Wanakutana kulumbana na kupembua wakiwa na imani maongezi yao na agenda zao zitachangia katika kuendeleza taifa hili.

Petu Hapa,

..miaka yote tumepiga siasa na ndiyo maana tuko nyuma.

..hakuna nchi iliyoendelea kutokana na malumbano ya watu wa aina ya Issa Shivji.

..sasa sisi bado tunawaendekeza hawa kwa kuwapa fedha chungu nzima watumie kuendeleza malumbano yao.
 
Joko Kuu

Jukumu la university mojawapo ni kuhakikisha inachochea mawazo mbalimbali katika jamii. Haiwezekani tukasema tusifikirie na mabadiliko yatakakuja. Mabadiliko yoyote yanakuja kutokana na ideas, which informs actions and the verse versa is true. So, wasomi for ages they have invested their times in ideas. Anyone who can't think for themselves are nothing.

I find Shivji and the crew doing exactly what they claimed to be, and me and you we could define other things, which could be science. Let's move out of this debate! and let do something! I heard the shivji worn the case for BAWATA, which took ten years. So sometime, the struggle take a long path, be patient.

The ways i know shivji, I won't be surprised if their budget was not beyond 10 millions. So, don't worry how much they have spent either!
 
PH nitazidi kuwafikishia ujumbe. Waandaaji wamebanwa sana. Naamini juma lijalo watatinga humu na kutupa dondoo zote. Pia naamini wataufanyia kazi ushauri wako.

JK sina uhakika kama hizo ni hoja au kebehi. Nasema hivi maana hakuna jamii iliyoendelea bila kujadili masuala mazito ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Leo mjadala ni kuhusu zahama ya uchumi duniani ambapo Gavana wa Benki, Prof. Benno Ndulu, atakuwepo kujadili athari zake kwetu na namna ya kukabiliana na zahama hiyo. Kama hiyo ni 'sihasa' tu haya mkuu endelea tu kuenzi hizo nchi za Ulaya na Marekani ambazo unadhani hazijadili siasa. Ila kumbuka maana halisi ya siasa ni suala la mgawanyo wa rasilimali na madaraka. Kama unadhani tutaendelea wakati tunagawia wageni rasilimali zetu hovyo hovyo bila kujadili namna ya kuzuia uporaji huo ambao kina Shivji wanauzungumzia kwenye vitabu vyao na ripoti zao za masuala ya haki za ardhi haya tuwaachie wengine siasa sisi tuwatumikie tu wanasiasa.

"Everything is political" - Anonymous
 
Petu Hapa,

..Cordesia,Mabenki,wafadhili etc hawapaswi kuchangia shughuli zisizokuwa na tija kama makongamano ya kisiasa.

..hii ni karne ya Science and Technology, sasa siyo vizuri kupoteza muda na pesa kujadili siasa, kama hili kongamano la Issa Shivji na wenzake.

JokaKuu:

Kuna kitu kinaitwa social routines. Hawa elites na intelligensia wetu wamezoezwa na mikutano na makongamano ambayo yanabakia kwenye vyumba vya mikutano bila kuwa na impacts yoyote kwa walengwa.

Hii ni sawa na mnugu kuwa na tattoo. Tattoo haiongezi ability ya mtu kufanya mambo, ni good feel factor tu.
 
Jokakuu,

Hapa umeniacha nje mkuu!

OK ngoja nitumie lugha nyingine. Kuna watu wanaojisikia kuwa ni wagonjwa wakati wao ni wazima. Wakienda kwa daktari, wanapewa dummy pills (placebo) na wanapata nafuu.

Mikutano na makongamano kwetu sisi ni Placebo za kuwafanya elites na intelligensia yetu kama kina Companero kujisikia nafuu.
 
JokaKuu:

Kuna kitu kinaitwa social routines. Hawa elites na intelligensia wetu wamezoezwa na mikutano na makongamano ambayo yanabakia kwenye vyumba vya mikutano bila kuwa na impacts yoyote kwa walengwa.

Hii ni sawa na mnugu kuwa na tattoo. Tattoo haiongezi ability ya mtu kufanya mambo, ni good feel factor tu.

Most thinkers don't act, kwahiyo sitaraji wasomi wetu watachukua hatua za kiutendaji. Kutegemea kwamba watakuwa watendaji wanachoyasema ni ndoto - kwani kazi yao ni kuchochea fikira - za wanafunzi na jamii - na ndicho kinachofanyika.

Lakini, swala lako la pili ni la msingi kwamba mijadala hiyo iwekwe kwenye utaratibu ambao watendaji mbalimbali wanaweza kuyatumia maongezi hayo.
 
companero said:
Leo mjadala ni kuhusu zahama ya uchumi duniani ambapo Gavana wa Benki, Prof. Benno Ndulu, atakuwepo kujadili athari zake kwetu na namna ya kukabiliana na zahama hiyo

..sasa Dr.Ndulu anakwenda kuwahadithia Prof.Shivji na Prof.Soyinka kuhusu mtikisiko wa uchumi duniani ili wafanye nini haswa?

..taifa letu halijitoshelezi kwa chakula, tena katika mashule yetu wanafunzi hawana waalimu wa kutosha, vitabu, na madawati,maabara, etc.

..sasa kama hali yetu ndiyo hiyo, hamuoni kwamba makongamano ya ku-theorize kama hili ni matumizi mabaya ya kidogo tulichonacho?
 
Most thinkers don't act, kwahiyo sitaraji wasomi wetu watachukua hatua za kiutendaji. Kutegemea kwamba watakuwa watendaji wanachoyasema ni ndoto - kwani kazi yao ni kuchochea fikira - za wanafunzi na jamii - na ndicho kinachofanyika.

Lakini, swala lako la pili ni la msingi kwamba mijadala hiyo iwekwe kwenye utaratibu ambao watendaji mbalimbali wanaweza kuyatumia maongezi hayo.

What you mean when you say "Most thinkers don't act". The essense of their existance is to act.

Watu wanachochewa na incentives. Mfano watapeli wa DECI walianzisha fictitious incentives ambazo ziliwafanya watu waweke pesa zao huko, kuliko kumsikiliza Shivji.
 
naposema thinkers don't act, mara nyingi wanachochea fikira za mabadiliko - wanafundisha, wanahamasisha, wanachambua, na kujenga ideas ambavyo vyote kwa namna moja ama nyingine zinainform action. Wale thinkers wenye firkra za kimapinduzi ndio unaweza kuwakuta kwenye mapambano - chachage, shivji, fanon, rodney, karl marx, nyerere, - wakitaka kuleta mabadiliko kwa kushiriki katika hali halisi ya maisha ya watu - wengine wanakuwa observants, later analysts and critics.
 
Zakumi,Petu Hapa,Companero,

..navutiwa zaidi na wataalamu wanaojielekeza ktk kubadili hali za wananchi kwa namna ambayo tunaweza kupima matokeo ya kazi zao.

..hii habari hapa chini imenivutia sana. tunahitaji kusikia wataalamu wengi zaidi wakiachana na makongamano na kwenda vijijini kusaidia juhudi za wakulima kuboresha maisha yao.

..hii habari toka gazeti la Raia Mwema has really touched me.

Raia Mwema said:
Kidumba anasimulia akibainisha tofauti ya tija kati ya huko walikotoka na waliko sasa akisema: "Nilianza kulima kwenye skimu hiyo mwaka 1986, tulilima kienyeji, hatukuwa na utaalamu wowote, lakini baadaye skimu yetu iliboreshwa, tukapata utalaamu kupitia mabwana shamba, shamba darasa na mzungu mmoja aliyekuja hapa kijijini kwetu.

"Nimeongeza uzalishaji wa mpunga, sasa navuna gunia kati ya 25 hadi 30 za mpunga kwa ekari moja, huko nyuma nilivuna kati ya gunia saba hadi kumi. Mwaka jana nilivuna gunia 31 katika ekari yangu moja niliyolima, niliuza gunia 15 na kubakiza 16 kwa ajili ya chakula na mbegu.

"Hapa ni kulima mwaka mzima, tunaita hakuna kulala, mpunga nalima mara moja kwa mwaka, halafu kuna vitunguu nalima mara mbili kwa mwaka, mwaka jana nililima ekari mbili na kuvuna gunia 80 kila ekari, lakini nikienda vizuri navuna hadi gunia 100 kwa ekari.

"Kwa mfano Julai mwaka jana nilivuna gunia 100 kwa kila ekari, safari ya pili nilivuna gunia 107, na safari ya tatu nilivuna gunia 96, bei ya Januari huwa ni shilingi 50,000 kwa gunia la vitunguu, lakini baada ya Januari huongezeka hadi kufikia shilingi 70,000."

bonyeza hapa kusoma habari nzima
 
Hadithi nzuri kwa hamasa! Safi sana. Lakini kunasiri ya mafanikio zaidi ya elimu ya mtaalamu na umwagiliaji. Lazima kunamsukumo wa ndani wa nafsi, uliotambua umuhimu wa kazi katika kuleta mabadiliko. Tunahitaji kujua wananchi wanafanya nini pia, fikira zao zinabadilika vipi wanaposhiriki katika uzalishaji mali. Sio tu katika kujenga nyumba mpaya, pia kutika kufanya upembuzi wa mazingira yao.
 
naposema thinkers don't act, mara nyingi wanachochea fikira za mabadiliko - wanafundisha, wanahamasisha, wanachambua, na kujenga ideas ambavyo vyote kwa namna moja ama nyingine zinainform action. Wale thinkers wenye firkra za kimapinduzi ndio unaweza kuwakuta kwenye mapambano - chachage, shivji, fanon, rodney, karl marx, nyerere, - wakitaka kuleta mabadiliko kwa kushiriki katika hali halisi ya maisha ya watu - wengine wanakuwa observants, later analysts and critics.

Sio kuwa nakataa shughuli walizofanya. Kama wanazifanya shughuli hizo as a part of academic rituals, which they should do, sina matata.

Lakini kusema kuwa wanayofanya yanaleta chachu za maendeleo ni kuwa irresponsible. Majority ya watanzania ambao wako responsible kuleta maendeleo wana-respond na vitu vingine kabisa na sio yanayotokea UDSM.
 
agree to disagree.
 
..sasa Dr.Ndulu anakwenda kuwahadithia Prof.Shivji na Prof.Soyinka kuhusu mtikisiko wa uchumi duniani ili wafanye nini haswa?

..taifa letu halijitoshelezi kwa chakula, tena katika mashule yetu wanafunzi hawana waalimu wa kutosha, vitabu, na madawati,maabara, etc.

..sasa kama hali yetu ndiyo hiyo, hamuoni kwamba makongamano ya ku-theorize kama hili ni matumizi mabaya ya kidogo tulichonacho?

Kumbuka pale ni Chuo Kikuu. Pale ndipo walipo wanafunzi wetu ambao wakihitimu wanaenda kufanya kazi kwenye mabenki, mawizara na kwenye taasisi mbalimbali. Hivyo fursa kama hizi ni muhimu kwao ili wajue nini kinaendelea nchini na duniani. Vyuo vyote vikubwa duniani vinafanya hivyo. Vinaleta wataalamu kutoa mihadhara ya Umma ili kuwajenga wanafunzi wao watakaokuwa watunga sera na watekelezaji wa mipango yao ya uchumi na maendeleo. Noam Chomsky, Jeffrey Sachs, Joseph Stigltz, Amatya Sen wote hao huwa wanatoa mihadhara na kuwa na mijadala mikubwa katika vyuo vyao vikuu na mijadala hiyo ndio inatoa chachu ya kufikiria na kuvumbua mipango ya maendeleo. Sasa unataka wanafunzi wetu wasipate fursa za kuwasikia vinara wetu ambao wameshika hatamu za ufahamu na ujuzi wa mambo? Au unadhani kazi ya chuo ni kutoa to vyetu?

"Elimu Sio Cheti Ni Ujuzi" - HAKIELIMU
 
Companero:

Intellectual pikiniki yenu imekwisha. Nina uhakika mwakani mtarudia yaleyale na kusahau kuwa miaka iliyopita mlishayajadili.
 
Companero:

Intellectual pikiniki yenu imekwisha. Nina uhakika mwakani mtarudia yaleyale na kusahau kuwa miaka iliyopita mlishayajadili.

Be part of it the coming october and you will see the difference. Zakumi, this was the first conference of Mwalimu chair, don't generalize with other conferences you have been part of. Being a good critic you need to be observant as well. For me, i see a bit of progress - this festival has managed to launch first a bulletin after many years of not having one, and they are going to produce another one in october. Second, they launch Nyerere's documentary, which tool significant organization.
 
Back
Top Bottom