Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,300
- 33,913
Katika hili naomba nitofautiane nawe kidogo. Ni kweli wananchi wanakatisha tamaa, lakini ni kwa nini wanakatisha tamaa?Wananchi ndio wameshika usukani wa kukatisha tamaa mlio mstari wa mbele. Haiwezekani mtu anatandikwa risasi mchana kweupe halafu tupo kimya tu
Kwa mtazamo wangu urafiki hauji wakati wa shida bali wakati wa raha na kwenye shida ni kusaidiana. Tatizo kuna watu wanataka kuwa wao ndiyo "wakombozi" na si viongozi wa ukombozi.
Kama tunataka kuwa na kundi kubwa nyuma yetu la watu wasiokata tamaa ni lazima wawe marafiki zetu wakati sisi tuna raha na wao wana shida. Kwa mfano Watu hawapandishwi madaraja, hawaongezwi mishahara, wamefukuzwa kazi mikono mitupu baada ya kufanya utumishi wa umma kwa zaidi ya miaka Kumi ama Ishirini, hao "wakombozi" walifanya nini?