Julius Mtatiro: Ndugu zangu watanzania, hakuna aliye salama

Julius Mtatiro

Verified Member
Joined
Jun 20, 2009
Messages
45
Points
125

Julius Mtatiro

Verified Member
Joined Jun 20, 2009
45 125
UJUMBE WANGU WA LEO KWENU.

Ndugu zangu watanzania hakuna aliye salama, hayupo! Si mwanasiasa wa upinzani, si mfanyakazi, si mkulima, si bodaboda, si tajiri wala masikini, siyo kiongozi wa dini au wa kijamii, si aliyeko mjini au kijijini.

Pona pona yetu ya peke yake ni kutumia haki zetu za kikatiba kupinga udhalimu, uonevu, ukoloni, ubwana, unyanyasaji, matumizi mabaya ya madaraka na kila aina ya uovu.

Yes, wapo wale wenzangu na mimi watakaotuponda usiku na mchana, lakini kazi ya kupigania haki za nchi yetu itawafaa hao watuchekao na vizazi vyao. Usimsikilize mtu anayekuponda na kukucheka kwa kupigania demokrasia, utawala wa kikatiba na kisheria kwenye nchi yetun

Uhuru wetu tulioupata mwaka 1961 ulipiganiwa ili wazungu wasituonee, wasitunyanyase, wasitukoloni, wasitudhulumu, wasitumie madaraka yao vibaya juu yetu na wasitukataze kulinda utu wetu.

Kama ni maendeleo wakoloni pia waliyaleta, walijenga reli, barabara, viwanda, shule, maofisi n.k. Wakoloni waliyafanya hayo si kwa sababu walikuwa wanatupa hisani, NO! ilikuwa ni kazi yao na jukumu lao. Walikuwa hawatoi pesa zao mifukoni, zilikuwa ni kodi zetu.

Pamoja na yale yote wakoloni waliyofanya wakasema ni maendeleo, bado tuliwatoa madarakani, tukasema tujitawale. Kujitawala kwetu kuna maana kusiwe na mtu anayetudhulumu, kutudhalimu, kutuonea, kutunyanyasa, kututishia jela, kutuzuia tusiseme, kutuua n.k.

Kujitawala kwetu kuwe na maana ya kulinda utu, haki, usawa, demokrasia, utawala bora, utii wa sheria na katiba na mgawanyo wa madaraka kati ya serikali, bunge na mahakama.

Ikija serikali yoyote hata kama ingalijenga viwanda vikubwa 1000 vyenye mtaji na hadhi ya kiwanda cha Dangote Mtwara (Tshs Trilioni 1), viwanda hivyo visingalikuwa na maana, ufahari, umuhimu wala tija yoyote kwenye maisha yetu ikiwa uhuru na haki zetu vinakanyagwa hadharani

Katika maisha hakuna EXCUSE yoyote ya "nakuua kwa sababu nakujengea viwanda", "sitaki ukusanyike, ufanye mkutano au uandamane kwa sababu natoa elimu bure", "sitaki uwe na uhuru wa kumsema Rais kwa sababu yeye anapambana na ufisadi...." There is no any excuse when WE THE PEOPLE are exercising our constitutional rights... There is no any excuse, I repeat!

Ndiyo maana nataka kuwaambia kuwa mapambano ya kudai haki za kikatiba katika nchi yetu ni endelevu, hayatajali kama Mbowe yuko jela au kwake, hayatajali ikiwa Maalim Seif yuko madarakani au ameporwa ushindi, hayatajali ikiwa Zitto yuko salama au yuko hatarini. Mapambano haya hayajali chochote.

Mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika hayakujali kama Nyerere angalikuwepo au asingalikuwepo. Mapambano ya kuwafikisha wana wa Israel nchi ya ahadi hayakujali kama Musa atakuwepo au hatakuwepo...hata bila uwepo wa Musa wana wa Israel walivuka vizingiti vyote na kufika kwenye nchi ya ahadi.

Hadi sasa sijaona ni nini au nini nani atakayewazuia watanzania kulifanya taifa lao kuwa la haki, usawa, utu, demokrasia, utawala bora, ukuu wa katiba na sheria na kila aina ya ndoto za watanzania wenye nia njema.

Jela si kikwazo, Kutekwa si kikwazo, kuuawa si kikwazo, kufunga vyama vyote vya upinzani au kuviua kwa maguvu na mikono ya dola si kikwazo..sioni kikwazo.

Kwa kadri viongozi wanavyoswekwa rumande na jela kwa sababu za kimakusudi ndivyo taifa letu linavyozidi kuwa imara, ndivyo wapigania mabadiliko wanazidi kupata ari mpya na nguvu kubwa na ndivyo hata waliokuwa wanatucheka wanakuja kuungana nasi.

Nataka kuwaambia kuwa safari inaweza kuwa ndefu lakini lazima tufike. Na tutafika ikiwezekana hata kama walioianzisha watakuwa magerezani na makaburini na haitajalisha nani atakuwepo. Tutakwenda mbele!

Mtatiro J
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi,
The Civic United Front,
29 Machi 2018.
 

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Messages
7,306
Points
2,000

Francis12

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2016
7,306 2,000
-
Hadi sasa sijaona ni nini au nini nani atakayewazuia watanzania kulifanya taifa lao kuwa la haki, usawa, utu, demokrasia, utawala bora, ukuu wa katiba na sheria na kila aina ya ndoto za watanzania wenye nia njema.

Jela si kikwazo, Kutekwa si kikwazo, kuuawa si kikwazo, kufunga vyama vyote vya upinzani au kuviua kwa maguvu na mikono ya dola si kikwazo..sioni kikwazo.
 

KIBST

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2017
Messages
511
Points
1,000

KIBST

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2017
511 1,000
Kwa kadri viongozi wanavyoswekwa rumande na jela kwa sababu za kimakusudi ndivyo taifa letu linavyozidi kuwa imara, ndivyo wapigania mabadiliko wanazidi kupata ari mpya na nguvu kubwa na ndivyo hata waliokuwa wanatucheka wanakuja kuungana nasi.
Mbona yeye hatumuoni kwenye UHARAKATI kama wenzake....?
 

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
33,148
Points
2,000

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
33,148 2,000
Heheee hee maneno mujarabu sana haya"" hata kina lugalo mkwawa ..na kinjekile ngwale "" walipokuwa wanapigana na wakoloni kwaajili ya uhuru wa mtanganyika "" wapo watangjanyika waliokuwa wanawabeza "" lakini hawakuona woga wakuziweka roho zao rehani ili vijukuu na vitukuu vyao vije kuishi kwenye nchi isiyo na mabeberu wa kikoloni""" ijpokuwa walifikwa na mauti kwaajili ya kuipigania haki "" lakini walijua kuwa wanaondoka huku wakiwa wamepandikiza mbegu za ukombovu kwa vijana wazalendo wa wakati huo""" baada ya miaka kadhaa tangu wafikwe na mauti ndoto zao zinakuja kutimia kwakupitia harakati za vijana kama mwalimu nyerere ""waliorithi mbegu hizo nakuhkikirsha wanamtoa mkoloni""

IPO siku tu wakati utaongea na kutoa hukumu YAKE """ hakuna marefu yasiyo na ukingo """
 

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Messages
2,395
Points
2,000

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
Joined May 16, 2011
2,395 2,000
"Kama ni maendeleo wakoloni pia waliyaleta, walijenga reli, barabara, viwanda, shule, maofisi n.k. Wakoloni waliyafanya hayo si kwa sababu walikuwa wanatupa hisani, NO! ilikuwa ni kazi yao na jukumu lao. Walikuwa hawatoi pesa zao mifukoni, zilikuwa ni kodi zetu."
Hii nimeipenda na ikanikumbusha hii reli ya kati ambayo hadi leo hii tunaitumia. Ilianza kujengwa na wakoloni wa kiDachi na ikakamilishwa na wakoloni wa Kiingereza. Sasa kama walitujengea reli ambayo hapana shaka ni 'maendeleo' (kwa mujibu wa maendeleo hayana vyama), kwa nini tulipigana kuwaondoa madarakani - ambacho kitu tunakiita tulipigania uhuru?
 

KIBST

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2017
Messages
511
Points
1,000

KIBST

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2017
511 1,000
Naomba niwe mkweli kwenye hili...kati ya Wabunge niliokuwa nawaamini ni wajasiri mbele ya Jeshi la POLISI ni LEMA....ila leo kaniacha mdomo wazi...kwanini kanishtua...

Leo nilikuwa nategemea jamaa angekuwa mstari wa mbele pale kisutu kuwapa makamanda moyo...Lakini cha ajabu BAADA YA KUSIKIA ETI ANATAFUTWA KUUNGANISHWA NA KINA MBOWE jamaa akalala mbele sasa ili kuonyesha unafiki wake kwa makamanda waliopo uraiani aka ORGANIZE mpango wa kuomba kwenda kukutanisha wabunge wa UPINZANI kwenye ofisi za EU.....

Sasa hapa tujiulize kama LEMA tu tunaemuona ni KAKSI ndani ya CHADEMA kalikimbia JESHI LA POLISI tena kwa KUHISI anatafutwa JE NYIE WA..APUZI humu mna sapoti 26/04...Vpi mkikutana na POLISI siku hiyo?....ISIKIENI TU MAHABUSU hata KINA MBOWE wakitoka huko wanaweza wasiwavuje moyo makamnda lakini ndani ya NAFSI zao kamwe hawata taka thubutu kurudi huko ambapo juzi mpaka hyo tarehe 3 watakuwa wanaonja UCHUNGU WA MAHABUSU makusudi kabsa...NDIO MAANA LEMA amekuwa na heshima siku hizi mbele ya JESHI LA POLISI mmana hata kwa hisia tu huyo UVUNGUNI mwa EU...

Nawashauri tu wale marofa wenzangu msidanganywe na hawa kina LEMA leo wamewadhihilishia ya kuwa WAKIHARIBU wao wana sehemu pa kujifichia KWA WAZUNGU WAO..vipi kuhusu nyie mtajificha wapi?...Bila shaka mtakuwa na hiyo sehemu maalumu mkijilaumu....
 

Forum statistics

Threads 1,355,842
Members 518,774
Posts 33,121,354
Top