Julius Mtatiro na Zitto Kabwe ni vijana watakaohamia CCM siku moja

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,034
28,201
Nawasikitikia sana hawa vijana kwa kushindwa kuchanga karata zao vyema kwani wangeweza kwa umri walionao kuwa sehemu ya baraza la mawaziri.

Tatizo lao walishindwa kuchanga karata zao vyema na sasa mbongo zao zimesimama kufikiria maendeleo ya nchi.

Zitto na Julius Mtatiro ni wasomi wanasiasa wazuri kutoka UDSM na walikuwa na fursa ya kuchagua upande sahihi kisiasa ili waweze kufikia hatua nzuri za kiuongozi badala yake uzwazwa au majivuni viliwatawala katika maamuzi yao.

Naamini iko siku watajifunza na kuelewa ni maamuzi yapi ya kisiasa ni sahihi kwayo.

Wako vijana wengi nyuma yao ambao walichanga karata zao vyema na sasa wamewazidi katika vyeo vya kisiasa.

Naamini bado hawajachelewa na watajirekebisha na hatimaye kuhamia chama kubwa la Ukombozi barani Afrika.

UPDATES:
Tarehe 11 August 2018...ndugu Julius Mtatiro atangaza kuhamia CCM.
 
Kumbe wewe unaangalia vyeo vya kisiasa kuna wengine hawaangalii vyeo wanaangalia maslahi mapana ya taifa hata bila vyeo wako tayari kulitumikia taifa lao.
Wameangalia maslahi ya Taifa kwa jicho chongo na hivyo kupoteza fursa adimu ya kulitumikia Taifa.
 
Fisiemu mnawaza vyeo tu.

Nape alikuwa kwenye baraza la mawaziri, leo yuko wapi?

Nyalandu alikuwa kwenye baraza la mawaziri, leo anatukanwa hadi na panya wadogo wa Lumumba.

Hayo mavyeo unayoyataja kama faida ambazo wangepata Zitto na Mtatiro kama wangekuwa CCM ni akili za fisi maji.
 
kitu kama hicho amezungumza Mh Makinda leo kwenye kongqmano la JKN. kuna vijana Wanauwezo hata wa kuendelea lkn wanakwamishwa na siasa za vuruguvurugu, fujofujo na mambo kama hayo.
ZZK Sifahamu ila Mtatiro akipitia njia sahihi anaweza kuwa mtu mkubwa sana. enzi za utawala wake DRS alikuwa na ushawishi kuliko hata rais wake Deo.
 
Mtoa mada ana maanisha Kitila mkumbo na juliana Shonza walichanga kalata zao vizuri.

Hivyo zito na wanasiasa wengine waige mfano huo
 
do you think every politician is living for higher appointments? what is good kupata vyeo na kuwasaliti wanyonge?
acha kuwaza vyeo wewe mtu mweusi.
Tell me one politician who would not want to be ina a high political profile.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom