Julius Mtatiro: Ikiwa mahakama itamtangaza Lipumba kuwa Mwenyekiti halali, CUF itakufa kuanzia hapo

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Aliyekuwa kada wa Chama Cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro amedai chama chake cha zamani huenda kikapoteza mwelekeo zaidi endapo Mwenyekiti wake anayetambuliwa na Msajili, Profesa Ibrahim Lipumba atakabidhiwa mamlaka na mahakama.

lipumbaaa.jpg


Mtatiro ambaye alihudumu kwenye chama hicho kwa zaidi ya miaka 10 amesema kuwa endapo chama hicho kitaendelea kuwa mikononi mwa Lipumba kina hatihati ya kupoteza idadi kubwa ya wabunge wake na madiwani hasa upande wa Tanzania bara.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mtatiro ameandika, "kwa miaka takribani 20 Lipumba amekuwa Mwenyekiti wa CUF asiye na mafanikio kabisa, amekuwa mgombea urais kupitia CUF kwenye chaguzi za 1995, 2000, 2005 na 2010 na kila uchaguzi kura zake zikishuka kama ndege iangukavyo kutoka angani".

Aidha Mtatiro amesema kuwa Lipumba amekosa ushawishi miongoni mwa makundi muhimu na hakuwahi kuthubutu kujenga ushawishi kwa taasisi za kijamii, hata kama kusingelikuwa na mgogoro katika CUF.

"Ikiwa Lipumba atatangazwa kuwa Mwenyekiti halali wa CUF, CUF itakufa kuanzia hapo, itakufa kwa maana ya kubakia chama kama vile vyama vya kina Kiraracha na wengine, haitakuwa na mashiko Bara wala Zanzibar", ameongeza Mtatiro.
 
Hao cuf wafe tu ' imekosa viongozi wenye vision chama kimechakaa hakina sera chanya limekuwa kama gari la mkaa ..mbaya zaidi huyo lipumba ni kibaraka mkubwa sana wa ccm anatumika miaka na miaka kuwahadaa wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ni fikra zake tu na siyo lazima iwe hivyo. Professa ni very pragmatic politician atawashangaza wengi iwapo hukumu ya mahakama itakuwa upande wake ila asahau kabisa kura za Pemba kwani kule Maalim amewafunga kamba vizuri sana.
 
asa mtatiro na lipumba wanatofauti ipi?

sema mtatiro anatakiwa tokea tokea fend fod ili mkuu amkumbuke maana ni muda kasahaulika
 
Cuf ikifa, chadema itanawili Zanzibar, kuna hatarii kubwa ya chadema kutawala siasa za Zanzibar 2020. Chadema itapata nguvu sana zanzibar
 
Msaliti hana rangi, Mtatiro na yeye amekimbia vita uwanjani naona uteuzi hadi sasa bado hajapewa au anaendelea kumungunyua lile donge nono?
 
Back
Top Bottom