Julius mtatiro: Bora cuf tubadilike tuwe kama chadema.

Mtatiro ni naibu katibu mkuu wa CUF ambaye ni kiongozi pekee aliyeamua kuwashauri viongozi wa CUF kubadilika na kufuata misingi ya utawala bora, Mtatilo aliamua kuwashauri wabunge na viongozi wa CUF kuamua kumfuata Rais KIKWETE ili aweze kuruhusu mabadiliko ya sheria ya ya ktunga katiba,

Mtatilo aligundua kuwa kile walichokiamua wabunge wa CUF bungeni kwa kupitisha huu mswaada wa sheria ya kutunga katiba ni kwa sababu hawakuona madhara yake kwa baadaye nahapo ndoo akaamua kuitisha kikao na viongozi wenzake wa CUF ili warudi nyuma japo walikosea, Mtatilo alisema kuwa ''KUFANYA KOSA SI KURUDIA KOSA, TUFANYE KAMA WALIVYOFANYA WENZETU CHADEMA ILI TUJINUSURU NA HII KASHFA YA KUITWA CCM B,"

Kiujumla simpingi Mtatilo kwani wabunge wake hawakukaa na kutafakali kwanza kitu ambacho kiliwafanya wapitishe maamzi yasiyokuwa na tija kwa taifa, kiufupi nawapongeza CUF kwa kugungua kosa jambo ambalo limenifanya nikiamini tena hiki chama changu,

CUF NGANGALI

Haya ndio mambo tunayotaka kusikia sio wapinzani kupingana pingana tuuu kila kukicha,jamaa walichemka tumepiga kelele wenzetu mnakosea wametusikia wamekifanyia kazi kilio chetu sasa tuwapongeze na kusonga mbele tuache kejeli,ndizo zinazofanya vyama vya upinzani visizungumze lugha moja,afterall cdm na cuf ni ndugu moja kwa vijana msiojua,waliwahi kufunga ndoa na cdm,na hiyo ni hostoria ya pekee ambayo haiwezi kufutika!
 
Back
Top Bottom