Julius Mtatiro Amewadanganya Waandishi Wa Habari Kuhusu Kupigwa Wanachama CUF!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Julius Mtatiro Amewadanganya Waandishi Wa Habari Kuhusu Kupigwa Wanachama CUF!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KING COBRA, Dec 15, 2011.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Julius Mtatilo , Amewambia Waandishi wa Habari kuwa ,utaratibu wa kuitisha mkutano wa matawi ya Manzese na Mabibo haukufuata na Kwamba katika Mgogorio huo hamadi Rashidi Mohammed alikodi kundi la Wahuni kutoka CCM kuja kuleta Vurugu.
  Ukweli ni Kwamba , Maalimu Seif amekwisha piga marufuku kusifanyike kikao chochote katika ngazi zote kitakacho mhusisha Hamad Rashidi na waraka huo wa kuoiga marufuku upo kwa Mketo unasubiri kusambazwa lakini unatekelezwa kwa Kidikiteta na MTATIRO!!

  Ushahidi uliopatika unaonyesha kuwa Viongozi wa Matawi Husika walifuata taratibu zote za Cuf na barua zote zilipelekwa ofisi ya wilaya kama inavyo onyesha hapa kwenye Attachment!!!


  Kitendo cha Mtatiro kudanganya umma ni aibu kwa kuwa anafanya kazi ya kuwa kibaraka wa Maalimu seif
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Naona kafungu mnalokatiwa na ccm A mnadhulumiana ndiyo maana ya kupigana vikumbo ndani yenu kama chichiemu bi.
  Mhhhhhhh! yetu macho!!!
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,819
  Likes Received: 36,928
  Trophy Points: 280
  siasa za maji ya chooni zinawagharimu CUF
   
 4. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 10,196
  Likes Received: 10,383
  Trophy Points: 280
  [Hamna kuwalipa kwa wakati maana walimu ikifika wakati wa kampeni huwa wanapewa hela za rushwa kisha wanaanza kujichelesha na kusema hakuna chama chenye sera bora kama ccm, vingine vyote ni vya kiukoo na kadini. Serekali ya ccm shikilia hapohapo mpaka tuheshimiane. Walipe mara moja kwa miezi miwili ili wakati wa kura watie akili.
   
 5. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 10,196
  Likes Received: 10,383
  Trophy Points: 280
  Cuf ziiii
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Ukiuwa kwa upanga nawe utakufa kwa upanga tu! unafki wa CUF sasa maji shingoni!!
   
 7. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  THE CIVIC UNITED FRONT
  ‘’CUF - Chama Cha Wananchi
  Office of Ward Secretary
  Manzese, Kinondoni – D.S.M.
  Date 14[SUP]th[/SUP] DEC . 2011
  [​IMG]

  Kumb. Na. CUF/ktb/Mzs- Knd /Vol. 007/2011

  Mhe. Kaimu Kalibu wa CUF,
  Ofisi ya wilaya ya Kinondoni
  Dar – es – salaam.

  YAH: KUTUPATIA WARAKA WA OFISI YA KATIBU MKUU WA CUF UNAOAGIZA NA KUTUZUIA WATENDAJI WA CHAMA TUSITOE USHIRIKIANO KWENYE SHUGHULI ZOTE ZA KICHAMA ZINAZOMUHUSISHA MH. HAMAD RASHID.

  Husika na somo la hapo juu.
  Rejea mazungumzo yetu mimi, wewe na wajumbe wawili niliongozana nao ya tarehe 10/12/2011 nilipokuwa nakukabidhi barua ya taarifa ya ujio wa Mhe. Hamad Rashid katika ofisi yetu ya kata kukabidhi msaada wa viti na meza alioutoa kwa ajili ya shughuli za utendaji za kata, ambapo wewe kaimu Katibu wa Wilaya, Mhe. Kassimu Chogamawano baada ya kufungua na kusoma barua ulinirudishia na kuniambia kuwa limetoka agizo toka ofisi ya Katibu Mkuu wa CUF Taifa linalotutaka watendaji kutotoa ushirikiano kwenye shughuli zote za chama zitakazomuhusisha Mhe. Hamad Rashid.

  Hivyo nakariri ombi langu katika maandishi (barua) juu ya kuiomba ofisi yako itupatie barua yenye maelekezo ya agizo hilo au nakala ya waraka tunaoungelea ambao umesema umekufikia. Sambamba na hilo nimesikitishwa kwa kuvamiwa ofisi yetu ya Kata na ‘’Blue Guard’’ wa Wilaya ya Kinondoni wakiongozwa na Kamanda wao Mwinyipembe Bakari waliongozana na ‘’Blue Guard’’ wa Taifa kuzuia makabidhiano ya msaada wa vifaa alioutoa Mhe. Hamad Rashid kwa ajili ya shughuli za Kata ya Manzese, tendo ambalo limesababisha kuenea kwa watu na kupotea kwa vifaa mbalimbali.
  Ninaomba ungelifanyia haraka kutupatia barua hiyo yenye agizo la kumtenga Mhe. Hamadi Rashid kwani kugoma kupokea taarifa zake kwa ofisi yako bila Kata na Matawi kujulishwa kunasababisha mgongano mkubwa wa kichama.
  Na hapa najiuliza je! Ulikataa taarifa zetu ili ‘’BG’’ hao waje kufanya vurugu hizo? Je kazi BG ni kupiga wanachama au wangesimamia zoezi la makabidhiano liende salama?
  Mbona hawakuthubutu kuzuia mkutano uliohutubiwa na Naibu Katibu Mkuu Mhe. J. Mtatiro siku hiyo hiyo ya tarehe 11/12/2011 majira ya saa kumi alasiri mpaka saa mbili usiku. Kwenye Tawi la Kosovo la Manzese bila sisi Kata na ninyi Wilaya kupewa taarifa? Huu ndio utaratibu?
  Na mbona matukio haya ni mengi sana na hasa kwa Naibu Katibu Mkuu Mhe. Mtatiro ni kinara wa kuvunja hizo taratibu anazosema kwa mifano mingi sana, Mwingine alipoalikwa na kuja Manzese, Mtaa wa Mvuleni kuja kuzindua ‘’CAMP’’ ya Zengwe pasipo tahadhari wala taarifa kwenye chombo chochote na cha ngazi yoyote ya chama hali anajua shughuli hizo za usiku ni hatari kiusalama hili nalo linahitaji darubini ?
  Nashauri haya mambo yasikuzwe na pasitumike vyeo au mamlaka kulazimisha maji yapande mlima, bali zitumike busara sana ili tusigonganishe na kupiganisha wanachama waliojitolea kukujenga chama kwa hali na mali.
  Mwisho nayasubiri majibu na miongozo yenye busara na haki sawa kwa wote.
  Asante
  ‘’HAKI SAWA KWA WOTE’’
  HAMDAN NGURANGWA​
  K/Katibu Kata ya Manzese​
  NAKALA:
  - Katibu Mkuu wa CUF Taifa
  - Mhe. Hamad Rashid (MB) Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF.
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Na msikitikia sana Mtatiro, hawajui wapemba, ni wanafiki, ni wabaguzi na ni vigeu geu, akamuulize James Mapalala atampa ushauri wa bure.
   
 9. K

  KIROJO Senior Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe Huyu Mtatiro ni kijana namshauri awe makini na maneno yake atakuja kujikuta yuko peke yake.
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  mtatiro ni msema hovyo. Mpuuzeni tu. Kwanza atakiwezaje chama cha kiisla?
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Mtatiro kishafahamu Prof Lipumba baada kugombea urais mara 4 na kuambulia patupu anatarjiwa kutogombea uenyekiti wa CUF ktk uchaguzi wao wa ndani ujao. Hivyo Mtatiro kajiona kuwa ni yeye tu ndiyo right person kurithi mikoba ya profesa -- kwani katiba ya chama yasema M'Kiti wa CUF lazima atoke Bara. Na katika azma hii Maalim Seif atamsapoti Mtatiro ili awe mfukoni mwake. Hivyo kisha anza rasmi hiyo kazi ya kulamba viatu.

  Pili itakuwa ni wasaa wa CUF kuwa na kiongozi wa dini nyingine.

  Ni mtazamo wangu
   
 12. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Mbona tarehe imeandikwa kwa kalamu ya wino? Hii haitii shaka kwamba barua ya maombi ya makabidhiano imeandikwa baada ya makabidhiano yenyewe? Iweje uandike barua kwa kutype maandishi katika tarakilishi (computer), halafu ushindwe kuandika tarehe kwa kutumia hiyo hiyo computer hadi uje uandike kwa mkono/wino, haitii shaka kuwa hii barua imeandikwa baada ya tukio?
   
 13. K

  KIROJO Senior Member

  #13
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo nalo Neno mKUUU
   
 14. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  :eyebrows:
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  dhambi ya kuwasaliti wanainchi bungeni itawagharimu sana CUF
   
 16. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45

  Kwani hata ikiandikwa kwa tarakishi na tarehe pia hiyo itakuaminisha kuwa iliandikwa katika muda husika? Hapa ilitakiwa ionekane kuwa barua iliwafikia wahusika na kupokelewa, tunahitaji jina, saini na tarehe iliyopokelewa.

  Lakini pia inaonyesha barua haikupokelewa kwa maagizo ya ofisi ya katibu mkuu hili ndilo linaloleta wasiwasi na sasa tunawataka kina Mtatiro walitolee maelezo.
   
 17. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawawezi kukubali kamwe kuwa na kiongozi (Mwenyekiti) KAFIR...
   
 18. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Namlilia kijana wetu Julius Mtatiro!!
   
 19. m

  malai the son New Member

  #19
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza inasikitisha pili ni jambo la aibu na ni kuonyesha ni jinsi gani tunavyo kurupuka na kuonyesha mioyo yetu na akilizetu zinafikiri nakutaka nini tofauti nayale tunayo yaweka mbele ya jamii husika . ni aibu sana kwa mtu kama mtatiro kutamka mbele ya vyombo vya habari kwakujiamini inhali akijua fika kuwa anayo wakilisha ni uwongo. na akijua fika kuwa uwongo mwisho wake ni mfupi. kuna wakati niliwai kumfananisha na wapiganaji wa chadema lakini nimegundua hanatofauti na madungayembe wengine
   
 20. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Taarifa zilizonifikia Punde zinaonyesha kuwa Julius Mtatilo ni Kundi la Maalimu seif na aliye mshawishi Kuingia CUF ni Ismail Jussa!!!

  ismail Jussa alitumwa na Maalimu seif kumutafuta Julius Mtatilo Wakati yupo UDSM kama maandalizi ya kumupata Mkristo wa Kumurithi Wilfred Lwakatare wakati Njama za Kumuondoa zimekamilika Kupitia Blueguds.

  Maalim Seif amemuweka Mtatilo hapo Kama Kinga kwani anajua Waislamu CUF hawawezi kumushambulia Kuogopa UDINI!!!

  Hata hivyo zipo taarifa kuwa maandamano ya kumtaka Mtatiro ajiuzulu yamepamba Moto na Jumatatu ijayo fika Makao Makuu ya CUF uone mapambano mapya !!!

  Maalimu seif amepanga kuongea n a Wana CUF mkoa wa DSM siku ya Jumapili katika Hotel StarLight ambapo Wakristo wengi watakuwa Makanisani na Ukumbi huo ni Mdogo kiasi cha kuzuia wengine wasiingie!!!

  Hofu yote hiyo ni kuzuia kundi la Hamad Rashid!!
   
Loading...