"Julius Kambarage Nyerere" Rais Masikini aliyewahi kuiongoza Tanzania

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,485
2,330
Nilikuwa mtoto mdogo na sasa ni mtu mzima sijawahi kusikia tuhuma zinazomuhusu Marehemu Julius K. Nyerere kuhusu kujilimbikizia mali wala kuwapigia chepuo watoto wake wapewe nafasi za juu katika uongozi wa nchi hii kama wengine waliomfuatia.

Nachojiuliza wengine wanashindwa nini kuiga hii roho ya uadilifu iliyokuwemo ndani ya muasisi wa Taifa hili?

Mfano mdogo: Mishahara tu ya hawa wengine si tunaisikia ikitamkwa, hapo hujazungumzia marupurupu mengine na watoto wao katika nyazifa mbalimbali n.k

Najiuliza moyo aliotujengea huyu baba umeenda wapi?

Mzee huyu alitufundisha kukusanya kodi hasa kwa bidhaa za nje (Wageni) ili kulinda bidhaa za ndani (Wazawa) ila leo nchi inaenda kinyume nyume, tunakandamiza ndani tunawalegezea wa nje, kauli mbiu inayotuongoza "TUNAVUTIA WAWEKEZAJI"

KAMA TAIFA, TUJITAFAKARI
 
Nyerere, hakuna wa kufanana nae...

Nyerere aliruhusu sekta binafsi kufanya biashara ya utalii

Nyerere alifunga mpaka wa Bologonja Serengeti - Masai Mara

Nyerere alikaa na wadau wa sekta ya utalii na kusikiliza maoni

Kwa kuweka VAT ghafla bila kutoa muda wa kujiandaa ni Hatari

Bado serikali ina nafasi ya kuahirisha hii kodi kwa mwaka mmoja ili kutoa nafasi kwa watalii kujua na kupanga budget zao
 
Back
Top Bottom