Julias Mtatiro: CCM inashinda chaguzi kwa kutumia mifumo ilele; rushwa, mabavu, hila, wawakilishi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
NINI KIMETOKEA KWENYE UCHAGUZI WA MARUDIO?

Na. Julius S. Mtatiro (23 Jan 2017).

Goodmorning. Katika uchaguzi huu mdogo CUF ilikuwa inatetea kata 1 ya Kimwani Muleba na CHADEMA ilikuwa inatetea kata 1 ya Duru, Babati. Kata zingine zote zilikuwa za CCM na zilikuwa zinatetewa na CCM.

Matokeo yanaonesha CCM imetetea viti vyake vyote vya udiwani (takribani 20), CUF imenyang'anywa kiti chake kimoja (Kimwani) na CHADEMA imelinda kiti chake kimoja (Duru).

Kwa vyovyote vile vyama mbadala haviwezi kujivunia matokeo haya kwani havikuweza kuishinda CCM, na CCM haina cha kutambia kwani imeongeza kata moja tu. Kwa saa nina mambo kadha ya kuzungumza;

1. Hali halisi inaonesha kuwa kama vyama mbadala vingeshirikiana vingelishinda kata si zaidi ya 7 hivi. Bahati mbaya mashirikiano haya yalikosekana tangu mwanzo baada ya upande wa "CUF ya Msajili na Bwana Yule" kusisitiza kuwa wataweka wagombea nchi nzima na hakuna UKAWA.

2. Lakini pia, hata shajihisho la ushirikiano mkubwa zaidi lililokuja kuzuliwa na kaka yangu Prof. Kitila Mkumbo lilifanywa TOO LATE kwa lengo la kutafuta sababu ya kujificha baada ya matokeo. Niliwahi kusema, kiuzoefu vyama haviwezi kuachiana maeneo wiki moja kabla ya siku ya uchaguzi na kushauri hivyo si kwa nia njema.

3. Baada ya CUF ya Msajili na Bwana Yule kujipanga kuvuruga uchaguzi huu na kushusha spirit ya UKAWA, vyama vya NCCR na CHADEMA pia vilionelea kila kimoja kijipiganie jambo ambalo ni kosa kubwa. Na madhara ya migawanyiko yote yalijulikana.

4. Uzoefu unaonesha kuwa, kuishinda CCM kwenye chaguzi ndogo ni nadra mno. Kuliwahi kuwa na mfululizo wa chaguzi ndogo, Tarime, Busanda, Tunduru, Mbeya Vijijini n.k. na kote huko CCM ilishinda isipokuwa Tarime na baadaye Arumeru. Katika chaguzi ndogo CCM hutawanya rasilimali zake nyingi zikajaa kwenye majimbo au kata hadi POMONI.

5. Mkakati wa DOLA na CCM kuvitumia baadhi ya vyama au baadhi ya viongozi kwenye vyama (mamluki) unaelekea kufanikiwa sana. Lakini, sera za "Self Protectionism" ndani ya vyama mbadala hata kwenye mambo yanayohitaji ushirikiano wa kitaifa zitaendelea kuvigharimu vyama vyetu.

6. Good News kwa ACT Wazalendo kwamba huenda ndicho chama kilichofanikiwa kwenye uchaguzi huu kuliko vyama vyote (CCM inclusive) kwani pamoja na uchanga wake kimevishinda baadhi ya vyama vikongwe kwenye kata chache (kwa idadi ya kura na si ushindi wa jumla). Na hiyo ni alert call kwamba ACT is needed in the UKAWA basket na kwa hiyo ianze ku BEHAVE like a true party wakati UKAWA pia ikiiandalia mazingira kisaikolojia.

7. Bado CCM inashinda chaguzi kwa kutumia mifumo ilele; rushwa, mabavu, hila, wawakilishi wa NEC na NEC yenyewe, uwezo wa uelewa wa wapiga kura (Mfano. CCM imepeleka uandikishaji wa Bima ya Afya kwa wananchi kata ya Nkome, wakati wa uchaguzi = Rushwa).

8. Vyama vya upinzani vinashindwa chaguzi hizi kwa sababu ya kukosa ushirikiano wa kweli baina ya vyama hivyo, maelezo namba 7 hapo juu na sentensi ya kwanza ya maelezo yaliyo namba 5 hapo juu.

9. Kwa hakika, matokeo haya hayana athari zozote za kufaulu kwa Magufuli katika sera zake au kushindwa kwa Magufuli katika sera zake. Yaani, CCM ya Magufuli haijawa na ushawishi wa ziada kwa wapiga kura ili kupata ushindi huu kwenye ngome zake. CCM bado inashinda chaguzi kibabe na kwa mkakati dola zaidi bila kujali nani yuko madarakani.

10. Sijaona connection yoyote kati ya matokeo haya na siasa za 2020. Vyama vyote vinayo fursa ya kuendelea kujipanga na kama tutafanikiwa kuuvunja mfumo dola unaoathiri vyombo vya uchaguzi na uhuru wake, unaoondoa mazingira sawa kwa vyama kufanya siasa n.k, mabadiliko ya kikatiba kwenye NEC na sheria za uchaguzi na mengine mengi, siasa za 2020 zitakuwa mbichi sana.

Nimechokoza mada, tujadiliane.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]; Haya ni maoni yangu binafsi, si ya CUF wala UKAWA.

[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG]@Jan2017.
 
Vyama vya upinzani vinashindwa chaguzi hizi kwa sababu ya kukosa ushirikiano wa kweli baina ya vyama hivyo, maelezo namba 7 hapo juu na sentensi ya kwanza ya maelezo yaliyo namba 5 hapo juu.
 
Jana nimeshuhudia katika kijiji kimoja watu wakifurahi kazi ya Rais, kwa sasa Rais anachukiwa na baadhi ya watu mjini ila anaungwa mkono na kundi kubwa vijijini na lenye maamuzi, Hao akina mtatiro they are after money
 
Mwenyekiti wa chama unashinda mitandaoni kuchokoza mada au huna kazi za kufanya ni mwenyekiti hewa, Mh Magufuli au Mbowe au lipumba wanawweza kuja Mitandaoni kuchokoza mada ili washinde wanajadili hahahaha tanzania ina mambo hiii duuuuh
 
Bwana yule kama ana akili timamu ajue kwamba, CUF hawamtaki, kuanzia viongozi mpaka wanachama na wapiga kura kwa ujumla wao. NAANGALIA ZIRO lol
 
Si wanasema ccm imechokwa inakuwaje wananchi wanaichagua?
Kwa hakika, matokeo haya hayana athari zozote za kufaulu kwa Magufuli katika sera zake au kushindwa kwa Magufuli katika sera zake. Yaani, CCM ya Magufuli haijawa na ushawishi wa ziada kwa wapiga kura ili kupata ushindi huu kwenye ngome zake. CCM bado inashinda chaguzi kibabe na kwa mkakati dola zaidi bila kujali nani yuko madarakani.
 
Tangu 2010 mnaainisha matatizo/kasoro hizo hizo lakini hamfanyi ufumbuzi on-time .

Mnaingiaje kwenye uchaguzi bila ya kudhibiti hila na ghiliba

Mnafanya siasa za upinzani mkiwa mmeridhika utadhani nyie ndio chama tawala, kila siku matamko na maandiko, acheni kututania
 
NINI KIMETOKEA KWENYE UCHAGUZI WA MARUDIO?

Na. Julius S. Mtatiro (23 Jan 2017).

Goodmorning. Katika uchaguzi huu mdogo CUF ilikuwa inatetea kata 1 ya Kimwani Muleba na CHADEMA ilikuwa inatetea kata 1 ya Duru, Babati. Kata zingine zote zilikuwa za CCM na zilikuwa zinatetewa na CCM.

Matokeo yanaonesha CCM imetetea viti vyake vyote vya udiwani (takribani 20), CUF imenyang'anywa kiti chake kimoja (Kimwani) na CHADEMA imelinda kiti chake kimoja (Duru).

Kwa vyovyote vile vyama mbadala haviwezi kujivunia matokeo haya kwani havikuweza kuishinda CCM, na CCM haina cha kutambia kwani imeongeza kata moja tu. Kwa saa nina mambo kadha ya kuzungumza;

1. Hali halisi inaonesha kuwa kama vyama mbadala vingeshirikiana vingelishinda kata si zaidi ya 7 hivi. Bahati mbaya mashirikiano haya yalikosekana tangu mwanzo baada ya upande wa "CUF ya Msajili na Bwana Yule" kusisitiza kuwa wataweka wagombea nchi nzima na hakuna UKAWA.

2. Lakini pia, hata shajihisho la ushirikiano mkubwa zaidi lililokuja kuzuliwa na kaka yangu Prof. Kitila Mkumbo lilifanywa TOO LATE kwa lengo la kutafuta sababu ya kujificha baada ya matokeo. Niliwahi kusema, kiuzoefu vyama haviwezi kuachiana maeneo wiki moja kabla ya siku ya uchaguzi na kushauri hivyo si kwa nia njema.

3. Baada ya CUF ya Msajili na Bwana Yule kujipanga kuvuruga uchaguzi huu na kushusha spirit ya UKAWA, vyama vya NCCR na CHADEMA pia vilionelea kila kimoja kijipiganie jambo ambalo ni kosa kubwa. Na madhara ya migawanyiko yote yalijulikana.

4. Uzoefu unaonesha kuwa, kuishinda CCM kwenye chaguzi ndogo ni nadra mno. Kuliwahi kuwa na mfululizo wa chaguzi ndogo, Tarime, Busanda, Tunduru, Mbeya Vijijini n.k. na kote huko CCM ilishinda isipokuwa Tarime na baadaye Arumeru. Katika chaguzi ndogo CCM hutawanya rasilimali zake nyingi zikajaa kwenye majimbo au kata hadi POMONI.

5. Mkakati wa DOLA na CCM kuvitumia baadhi ya vyama au baadhi ya viongozi kwenye vyama (mamluki) unaelekea kufanikiwa sana. Lakini, sera za "Self Protectionism" ndani ya vyama mbadala hata kwenye mambo yanayohitaji ushirikiano wa kitaifa zitaendelea kuvigharimu vyama vyetu.

6. Good News kwa ACT Wazalendo kwamba huenda ndicho chama kilichofanikiwa kwenye uchaguzi huu kuliko vyama vyote (CCM inclusive) kwani pamoja na uchanga wake kimevishinda baadhi ya vyama vikongwe kwenye kata chache (kwa idadi ya kura na si ushindi wa jumla). Na hiyo ni alert call kwamba ACT is needed in the UKAWA basket na kwa hiyo ianze ku BEHAVE like a true party wakati UKAWA pia ikiiandalia mazingira kisaikolojia.

7. Bado CCM inashinda chaguzi kwa kutumia mifumo ilele; rushwa, mabavu, hila, wawakilishi wa NEC na NEC yenyewe, uwezo wa uelewa wa wapiga kura (Mfano. CCM imepeleka uandikishaji wa Bima ya Afya kwa wananchi kata ya Nkome, wakati wa uchaguzi = Rushwa).

8. Vyama vya upinzani vinashindwa chaguzi hizi kwa sababu ya kukosa ushirikiano wa kweli baina ya vyama hivyo, maelezo namba 7 hapo juu na sentensi ya kwanza ya maelezo yaliyo namba 5 hapo juu.

9. Kwa hakika, matokeo haya hayana athari zozote za kufaulu kwa Magufuli katika sera zake au kushindwa kwa Magufuli katika sera zake. Yaani, CCM ya Magufuli haijawa na ushawishi wa ziada kwa wapiga kura ili kupata ushindi huu kwenye ngome zake. CCM bado inashinda chaguzi kibabe na kwa mkakati dola zaidi bila kujali nani yuko madarakani.

10. Sijaona connection yoyote kati ya matokeo haya na siasa za 2020. Vyama vyote vinayo fursa ya kuendelea kujipanga na kama tutafanikiwa kuuvunja mfumo dola unaoathiri vyombo vya uchaguzi na uhuru wake, unaoondoa mazingira sawa kwa vyama kufanya siasa n.k, mabadiliko ya kikatiba kwenye NEC na sheria za uchaguzi na mengine mengi, siasa za 2020 zitakuwa mbichi sana.

Nimechokoza mada, tujadiliane.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]; Haya ni maoni yangu binafsi, si ya CUF wala UKAWA.

[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG]@Jan2017.
Ni pigo kwa wapenda mabadiliko lakini kama kuna mtu anayeangalia mambo kwa makini hili lilitegemewa.
Hivi kweli pamoja na kuwa ni jimbo moja tu CCM watakubali Dimani liende upinzani?Nini ingekuwa matokeo ya jimbo kwenda CUF?
Uchaguzi mdogo huu unadhihirisha jambo moja kubwa ambalo ni kuwa USIMUAMINI MTANZANIA asilimia mia kwani msimamo wake unayumba.
La pili ni kuwa kwa vijana iangalieni siasa ya Tanzania kwa macho mawili kwani majority ya Watanzania hawajawa tayari kwa mabadiliko ya kimfumo (msitumie nguvu kubwa kupita kiasi wakati wale ambao unaona wanaumia hawajatambua kama wanaumia).
Uchaguzi mdogo umepita,maisha yaendelee.
 
Yaani Hawa Viongozi Wa Upinzani Kama Na Familia Zao Wanaziendesha Hivi Basi Kuna Tatizo Kubwa.

- Unapata Tatizo Nyumbani Kwako Badala Ya Kukaa Ujue Namna Ya Kulitatua Wewe Unakimbilia Kutukana Na Kuwalaumu Majirani

- Huyo Mtatiro Tangu Apigwe Sunna Akili Imemruka Kabisa Halafu Hata Huwa Haoni Aibu Kabisa, Na Kibaya Zaidi Huwa Anajiona Mjuvii

- Huwa Nakereka Sana Unanunua Gazeti La Mwananchi 1,000 Then Unakuta Kurasa Tano Makala Za Mtatiro, Patrick Elias, Elias Msuya, Malissa G, Saanani. Siku Hizi Nimeacha Kabisa Kuharibu Buku Yangu Bora Ninywe Soda
 
Kama mmeshindwa kaa kushoto kama mnajua sisiemu ni wezi kwann mnasimamisha wagombea hatutaki ujinga hapa uwo utitili wa mavyama ndio msumali wenu na utaendelea kuwachoma mpaka mtakapo jitambua
Wambie mkuu hawa wagonjwa wa akili
 
Jana nimeshuhudia katika kijiji kimoja watu wakifurahi kazi ya Rais, kwa sasa Rais anachukiwa na baadhi ya watu mjini ila anaungwa mkono na kundi kubwa vijijini na lenye maamuzi, Hao akina mtatiro they are after money
Sahihi kabisa mkuu wangu umeongea vitu vya maana sana kupata ujumbe
 
Back
Top Bottom