Juliana Shonza: Maji bado ni kilio kikubwa licha ya miradi kuwepo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge Juliana Shonza suala la maji limeendelea kuwa kilio kikubwa cha wananchi licha ya Wizara ya Maji kupelekewa fedha nyingi huku vilio vikitoka kwenye maeneo yale yale ambayo Serikali tayari imepeleka miradi mikubwa

Ameeleza hayo Bungeni wakati wa majadiliano ya Bajeti ya Wizara ya Maji na kuongeza kuwa, chanzo cha hayo yote ni kutokuwepo usimamizi wa kutosha kwenye Mikoa, Wilaya na Kata
 
Hakuna wapinzani wa kuwalaumu sasa wameanza kulaumiana wenyewe kwa wenyewe. I am sure enzi zile mbunge wa upinzani angesema hivi bungeni huyu dada angemrukia na kumzodoa kuwa wapinzani wanapinga pinga kila kitu! Na angeipongeza wizara ya maji kwa kazi nzuri chini ya jemedari
 
Yaani ni kama mchezo wa kuigiza, mfano Mbeya vyanzo vya maji ni vingi sana! Lakini mabomba hayatoi maji, mpaka unajiuliza kuna mainjinia kweli!? Tukuyu, Mwakaleli, Suma, Makandana, Ndyonga, Rwangwa, Masoko, Kiwira hata km 30 hazifiki maji kibao! Mabomba hayatoi maji!
 
Back
Top Bottom