Uchaguzi 2020 Juliana Shonza: Kwetu sisi wewe ni Rais, Oktoba 28 tuepuke matapeli wa kisiasa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Leo Rais Magufuli amefika Vwawa mkoani Songwe katika mkutano wa kampeni, pamoja na mambo mengine Rais Magufuli aliongelea Songwe kama sehemu ya mwisho kupewa hadhi ya mkoa hivyo ataujali kama mtoto wa Mwisho kwenye familia. Pia alimkaribisha Juliana Shonza kuongea na wananchi ambae anamaliza muda wake kama naibu waziri wa Michezo, naye alinena yafuatayo,

Juliana Shonza: Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, DKT. John Magufuli, sisi wananchi wa mkoa wa Songwe tutakuwa tunafanya makosa sana na hatukutendei haki iwapo tukisema leo umekuja kufanya kampeni kwa sababu kazi ambazo umefanya kwenye mkoa wetu wa Songwe ni kampeni tosha, kwa hiyo kwetu sisi wananchi wa Songwe wewe ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Niwaombe sana wananchi wenzangu wa mkoa wa Songwe, siku ya tarehe 28 mwezi wa kumi tukatae matepeli, tuepuke matapeli wa kisiasa, kura zote tupeleke kwa Dr. John Pombe Magufuli na kura zote kwa wabunge sita ya majimbo ya mkoa wa Songwe na madiwani wa mkoa wa Songwe.
 
Hiyo misifa ndio imempumbaza jiwe akawasahau wanyonge wapiga kura sasa wanamiminika kwa #NiYeye
 
Huyu si aliunga juhudi mkono,atakuwa anatafuta kacheo .

Tatizo Mkuu itategemea ameamkaje.
 
Back
Top Bottom