Julian Assange: Mambo 10 aliyofichua kupitia wikileaks yaliyomfanya awe mwiba kwa mataifa ya magharibi na makampuni ya kimataifa

Ziggy Sobotka

Member
Feb 13, 2019
19
36
1. RIPOTI YA TRAFIGURA. Mwaka 2009 website ya Wikileaks ilitoa ripoti kuhusu Kampuni kubwa ya mafuta ya Trafigura, wikileaks walifanikiwa kupata ripoti ya mwanasayansi John Minton iliyokuwa inasema uchafu wa kemikali za mafuta ambayo kampuni ya Trafigura imemwaga kwenye pwani ya nchi za Afrika Magharibi (hasa Ivory Cost) ulikuwa na athari kubwa za kiafya kwa wakazi wa nchi hizo kama vile kuungua ngozi, kuharibika kwa macho na hata kupelekea vifo kwa wakazi kutokana na kansa inayosababishwa na kemikali ndani ya maji. Kampuni ya Trafigura ililipeleka gazeti maarufu la Uingereza The Guardian mahakamani ili kuzuia lisichapishe riport hiyo, lakini taarifa zilipoifikia management ya Wikileaks waitafuta data na kuziachia hewani kwenye Website yao. Mwaka 2010 kampuni ya Trafigura ilikuwa matatani na kuamua kumaliza mambo nje ya Mahakama kwa kulipa kiasi cha Dola za kimarekani Millioni 46 kwa wahanga wa tatizo hilo la kimazingira walilolisababisha.

2. Ushirikiano wa kibiashara wa Nchi zilizoko katika Bahari ya Pacific (The Trans-Pasific Partinership). Ushirikiano wa kibiashara unahusisha nchi za Canada, USA, Mexico, Peru, Chile, Japan, Vietnam, Brunei, Malaysia, Singapore,Australia na New Zealand ulisainiwa mwaka 2016 baada ya miaka 7 ya makubaliano ya siri lakini ukiwa bado unasubiliwa kuanza kazi rasmi. Makubaliano bado mkataba bado hayajawekwa wazi lakini Wikileaks ilitoa siri zilizohusu makubaliano ya mkataba huo ambazo hazikuwa nzuri na kuamsha hisia tofauti kwa wakati wa mataifa hayo. Baadhi ya mambo hayo ni kuwakatalia watu maskini haki ya huduma za dawa na mipango ya kubana uhuru wa kujieleza kwa serikali kuwa na uwezo wa taarifa ipi itoke na ipi isitoke kwa umma kama itakuwa ya kuaibisha serikali au kuichafua kwenye nyanja za kiuchumi, kitendo ambacho ni kinyume na katiba za nchi wanachama.

3. Uzuiwaji wa baadhi ya Website huko Australia chini ya mkono wa serikali (The Great Firewall of Australia). Serikali ya Australia mwaka 2009 iliamua kuwa baadhi ya website hazikuwa nzuri machoni mwa wananchi wa Australia walitoa list ya website watakazozifungia milele bahati mbaya kabla hawajafanya hivo, wikileaks walipata taarifa ya website zilizokuwa mbioni kufungiwa na kuzitangaza kwenye website yao kwa wananchi wazione. Bahati mbaya website nyingi zilikuwa hazina athari kama serkali ilivosema mfano website wa makampuni ya usafirishaji, madaktari wa meno na wikipedia zilikuwepo.

4. Skendo ya Chama Cha AKP cha Uturuki. Mwezi Julai 2016 Wikileaks ilizirusha taarifa za mawasilano ya Email kati ya wanachama na viongozi wa juu wa serikali ya Uturuki mara baada ya mapinduzi yaliyoshindikana ikuhusisha taarifa za kuanzia mwaka 2010 zaidi ya barua pepe 3,000 zilizozua mjadala mzito nchini uturuki na duniani kwa ujumla. Zilizokuwa zikitoa maelekezo ya kuwachunguza na kuwaweka vizuizini mamia ya walimu, polisi na majudge waliokuwa kinyume na utawala wa raisi Audegon. Na katika kisa hicho wikileaks walitoa pia adress na mawasiliano ya mamia ya wanawake wa kituruki kitu ambacho kiliwaletea nao kupingwa maana taarifa hizo zilizokuwa kwenye system ya chama zingelea usumbufu dhidi ya wanawake hao.

5. Taarifa ya kanisa la Scientology (Church of Scientology). Wikileaks walichapicha taarifa katika website yao kuhusu makusanyo ya vipande vya biblia ya siri ya Dini ya Scientology inayowahusisha mastaa wa Hollywood kama John Travolta na Tom Cruz. Kupata data zaidi kuhusu dini hii pitia mtandaoni kuna machapisho mengi kuhusu.

6. Meseji kutoka USA STATE DEPARTMENT (CABLE GATE). Mwaka 2010 walichapisha meseji nyingi kutoka USA State Department zilizoibwa na Mwanajeshi wa marekani Bradley Manning kuhusu mambo mengi ikiwemo taarifa kutoka Balozi za Marekani duniani kote kuhusu viongozi wa mataifa mengine duniani. Kama taarifa kuhusu raisi wa Ufaransa Sarkozy na nguvu ya Putin Russia na hata Skendo ya hapa Tanzania ya Mkurugenzi wa Takukuru Hosea kumuita Kikwete dhaifu kufatilia mashtaka ya rushwa alipokuwa akipiga story na Balozi wa Marekani na viongozi kibao wa kiafrica. Hapa ndipo Marekani ilipoingia kwa nguvu zote kumfungulia Mwanzilishi wa Wikileaks Julian Assange mashtka ya kuhatarisha usalama wa taifa la Marekani. Hii pia ilipelekea makampuni kama Visa, Paypal na Apple kuacha kufanya kazi na Website ya Wikileaks.

7. Taarifa kuhusu gereza maarufu la Guantanamo. (The Guantanamo Bay Paper). Ripoti kuhusu mateso na uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa katika Gereza maarufu la Guantano linalo washikiria wahalifu wengi wa matendo ya Kigaidi uliamsha hisia kwa watetezi wa haki za binadamu duniani kote kuhusu uchafu unaofanywa na serikali ya marekani kwa watuhumiwa walioko huko gerezani Guantanomo Bay Cuba.

8. Meseji za 9/11 siku ya tukio la kulipuliwa kwa majengo pacha ya World Trade Centre na jengo la wizara ya ulinzi Washington. Kuanzia saa 1 kabla ya kulipuliwa majengo na baada ya masaa 24. Meseji zilizotunzwa kutoka Pentagon, FBIA, FEMA na NYPD zilichapishwa ili angalau kuwapa picha wananchi wa marekani kuhusu nini kilikuwa kinaendelea siku ya matukio hayo ambayo yalileta taharuki kwa ulimwengu na raia wa Marekani kwa ujumla. Zilikuwa ni meseji za watu wa kawaida wakijaribu kuulizana kuhusu nini kinaendelea katika siku ya matukio hayo ya kusikitisha zaidi ya meseji milioni moja zilichapishwa.

9. Kuvuja kwa taarifa juu ya uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2016. Kuvuta kwa meseji za siri kutoka kambi ya Democratic na mgombea wao Hilary Clinton na taarifa za wachangia wakubwa wa uchaguzi kwa kambi ya Democratic na jinsi chama kilivyomuunga mkono Hillary Clinton dhidi hujuma kwa mpinzani wake ndani ya chama Beny Sanders. Na speech ya Hillary Clinton kwa wafanyabiashara Wallstreet iliyoonesha anachoongea na wafanyabiashara ni tofauti anachowaambia wananchi wa kawaida. Watu wengi walitegemea Hilary Clinton kushinda lakini tofauti akashinda Trump watu wanajiuliza je uvujaji wa hizo data ulimsaidia kiasi gani Rais Trump kushinda.

10. Mauaji ya kinyama huko Iraq yanayofanya na majeshi ya marekani. Mwezi wa 4/5/2010 Wikileaks iliachia video zinazionesha ndege ya kijeshi ikiwapiga risasi raia huku marubani wakicheka kama wanacheza Video Game na cha ajabu zaidi baada ya kufanya mauaji hayo gari iliyokuja kubeba maiti na watu waliokuwa wakisaidia kubeba miili walipigwa risasi bila huruma na kuua pia mtoto aliyekuwa ndani ya gari. Ulimwengu ulishtushwa na yaliyokuwa yanafanywa na wanajeshi hao ambao ni uhalifu wa kivita na je mangapi tusiyoyaona yanayoendelea na kuleta hofu juu ya ubabe wa marekani kuvamia mataifa mengine na kuua bila sababu.

NB: Kutolewa kwa taarifa hizo kimmemfanya Julian Assange kuishi mafichoni ndani ya ubalozi wa nchi moja ya amerika kusini kwa muda mrefu mpaka alivitolewa kwa nguvu kutoka ubalozini baada ya ubalozi huo kumwambia aondoke kutoka na kuvunja baadhi ya utaratibu wa kukaa ndani ya ubalozi huo. Je mtu kama huyu inatakiwa apongezwe au atiwe kizuizini kama alivofanyiwa.
View attachment 1077703View attachment 1077704

The absence of evidence is not the evidence of absence.
 
taarifa zake zimenufaisha mamilioni lakini malipo anayabeba yeye binafsi. ukweli alipaswa kusanehewa maana kauanika ukweli. na kupitia ukweli huo wengi wamepona, hasa pwani ya ivory coast, australia na sakata la kufungiwa mitandao, unyama wa majeshi ya marekani nchini iraq
 
Tusisahau kuwa kuna mashtaka yanayomkabili ya ubakaji. Tusikimbilie kusema amebambikiwa kesi wakati hata yeye kuna wakati alielekea kukiri kufanya non consensual sex na bidada yule. Kufanya kwake mema kusijustify na mabaya aliyoyafanya
 
hivi washampeleka us? Na vipi yule trans woman elizabeth manning ambaye ndio chanzo cha yote, nae yupo ndani
 
Mkuu ukipata muda Download Documentary moja kumhusu amehojiwa huyo mwanamke na Assange mwenyewe, utaona kabisa ishu ilikuwa ya kusukwa flani ila jamaa ndio kawa victim. Hawa majasusi wa huu ulimwengu waache tuu wako tayari kuziba siri zao kwa namna yoyote ile. Nilivoicheki ile documentary nilibadili mawazo yangu kuhusu kesi yake hiyo ya ubakaji.
 
6. Meseji kutoka USA STATE DEPARTMENT (CABLE GATE). Mwaka 2010 walichapisha meseji nyingi kutoka USA State Department zilizoibwa na Mwanajeshi wa marekani Bradley Manning kuhusu mambo mengi ikiwemo taarifa kutoka Balozi za Marekani duniani kote kuhusu viongozi wa mataifa mengine duniani. Kama taarifa kuhusu raisi wa Ufaransa Sarkozy na nguvu ya Putin Russia na hata Skendo ya hapa Tanzania ya Mkurugenzi wa Takukuru Hosea kumuita Kikwete dhaifu kufatilia mashtaka ya rushwa alipokuwa akipiga story na Balozi wa Marekani na viongozi kibao wa kiafrica.
The absence of evidence is not the evidence of absence.
Kama kawaida hili neno halikosekani!...
Ila mtu aliyevumbua Panama Papers namheshimu sana!, kaitendea dunia heshima kubwa sana!...
 
hivi washampeleka us? Na vipi yule trans woman elizabeth manning ambaye ndio chanzo cha yote, nae yupo ndani

Assange naona bado anashikiliwa na vyombo vya usalama vya Uingereza. Manning alipunguziwa miaka ya gerezani na serikali ya Obama ila mwezi wa 3 mwaka huu alikamatwa tena sababu ya kukataa kumsnitch Assange kwenye Mahakama kuu ya Marekani.
 
Tusisahau kuwa kuna mashtaka yanayomkabili ya ubakaji. Tusikimbilie kusema amebambikiwa kesi wakati hata yeye kuna wakati alielekea kukiri kufanya non consensual sex na bidada yule. Kufanya kwake mema kusijustify na mabaya aliyoyafanya
Hiyo ilikuwa nchini Sweden na walimfutia mashtaka na sasa wameibua mashtaka upya.
 
Kama kawaida hili neno halikosekani!...
Ila mtu aliyevumbua Panama Papers namheshimu sana!, kaitendea dunia heshima kubwa sana!...

Hahhaaaa Kikwete hakukoroma alipotezea kiutuzima naona Ndugai yeye hataki kabisa kuitwa hivo. Jamaa wa Panama nae alicheza sana huu ulimwengu unasiri nzito sana nyingi sana ukipata hata nafasi ya kuzijua 1/10 tuu utashangaa sana jinsi Dunia inayoendeshwa na kikundi cha watu wengine tunaishi kwa kufata order zao bila kujua kuanzia mavazi, kula, burudani, magonjwa, vita na kila kitu kilichopo.
 
1. RIPOTI YA TRAFIGURA. Mwaka 2009 website ya Wikileaks ilitoa ripoti kuhusu Kampuni kubwa ya mafuta ya Trafigura, wikileaks walifanikiwa kupata ripoti ya mwanasayansi John Minton iliyokuwa inasema uchafu wa kemikali za mafuta ambayo kampuni ya Trafigura imemwaga kwenye pwani ya nchi za Afrika Magharibi (hasa Ivory Cost) ulikuwa na athari kubwa za kiafya kwa wakazi wa nchi hizo kama vile kuungua ngozi, kuharibika kwa macho na hata kupelekea vifo kwa wakazi kutokana na kansa inayosababishwa na kemikali ndani ya maji. Kampuni ya Trafigura ililipeleka gazeti maarufu la Uingereza The Guardian mahakamani ili kuzuia lisichapishe riport hiyo, lakini taarifa zilipoifikia management ya Wikileaks waitafuta data na kuziachia hewani kwenye Website yao. Mwaka 2010 kampuni ya Trafigura ilikuwa matatani na kuamua kumaliza mambo nje ya Mahakama kwa kulipa kiasi cha Dola za kimarekani Millioni 46 kwa wahanga wa tatizo hilo la kimazingira walilolisababisha.
2. Ushirikiano wa kibiashara wa Nchi zilizoko katika Bahari ya Pacific (The Trans-Pasific Partinership). Ushirikiano wa kibiashara unahusisha nchi za Canada, USA, Mexico, Peru, Chile, Japan, Vietnam, Brunei, Malaysia, Singapore,Australia na New Zealand ulisainiwa mwaka 2016 baada ya miaka 7 ya makubaliano ya siri lakini ukiwa bado unasubiliwa kuanza kazi rasmi. Makubaliano bado mkataba bado hayajawekwa wazi lakini Wikileaks ilitoa siri zilizohusu makubaliano ya mkataba huo ambazo hazikuwa nzuri na kuamsha hisia tofauti kwa wakati wa mataifa hayo. Baadhi ya mambo hayo ni kuwakatalia watu maskini haki ya huduma za dawa na mipango ya kubana uhuru wa kujieleza kwa serikali kuwa na uwezo wa taarifa ipi itoke na ipi isitoke kwa umma kama itakuwa ya kuaibisha serikali au kuichafua kwenye nyanja za kiuchumi, kitendo ambacho ni kinyume na katiba za nchi wanachama.
3. Uzuiwaji wa baadhi ya Website huko Australia chini ya mkono wa serikali (The Great Firewall of Australia). Serikali ya Australia mwaka 2009 iliamua kuwa baadhi ya website hazikuwa nzuri machoni mwa wananchi wa Australia walitoa list ya website watakazozifungia milele bahati mbaya kabla hawajafanya hivo, wikileaks walipata taarifa ya website zilizokuwa mbioni kufungiwa na kuzitangaza kwenye website yao kwa wananchi wazione. Bahati mbaya website nyingi zilikuwa hazina athari kama serkali ilivosema mfano website wa makampuni ya usafirishaji, madaktari wa meno na wikipedia zilikuwepo.
4. Skendo ya Chama Cha AKP cha Uturuki. Mwezi Julai 2016 Wikileaks ilizirusha taarifa za mawasilano ya Email kati ya wanachama na viongozi wa juu wa serikali ya Uturuki mara baada ya mapinduzi yaliyoshindikana ikuhusisha taarifa za kuanzia mwaka 2010 zaidi ya barua pepe 3,000 zilizozua mjadala mzito nchini uturuki na duniani kwa ujumla. Zilizokuwa zikitoa maelekezo ya kuwachunguza na kuwaweka vizuizini mamia ya walimu, polisi na majudge waliokuwa kinyume na utawala wa raisi Audegon. Na katika kisa hicho wikileaks walitoa pia adress na mawasiliano ya mamia ya wanawake wa kituruki kitu ambacho kiliwaletea nao kupingwa maana taarifa hizo zilizokuwa kwenye system ya chama zingelea usumbufu dhidi ya wanawake hao.
5. Taarifa ya kanisa la Scientology (Church of Scientology). Wikileaks walichapicha taarifa katika website yao kuhusu makusanyo ya vipande vya biblia ya siri ya Dini ya Scientology inayowahusisha mastaa wa Hollywood kama John Travolta na Tom Cruz. Kupata data zaidi kuhusu dini hii pitia mtandaoni kuna machapisho mengi kuhusu.
6. Meseji kutoka USA STATE DEPARTMENT (CABLE GATE). Mwaka 2010 walichapisha meseji nyingi kutoka USA State Department zilizoibwa na Mwanajeshi wa marekani Bradley Manning kuhusu mambo mengi ikiwemo taarifa kutoka Balozi za Marekani duniani kote kuhusu viongozi wa mataifa mengine duniani. Kama taarifa kuhusu raisi wa Ufaransa Sarkozy na nguvu ya Putin Russia na hata Skendo ya hapa Tanzania ya Mkurugenzi wa Takukuru Hosea kumuita Kikwete dhaifu kufatilia mashtaka ya rushwa alipokuwa akipiga story na Balozi wa Marekani na viongozi kibao wa kiafrica. Hapa ndipo Marekani ilipoingia kwa nguvu zote kumfungulia Mwanzilishi wa Wikileaks Julian Assange mashtka ya kuhatarisha usalama wa taifa la Marekani. Hii pia ilipelekea makampuni kama Visa, Paypal na Apple kuacha kufanya kazi na Website ya Wikileaks.
7. Taarifa kuhusu gereza maarufu la Guantanamo. (The Guantanamo Bay Paper). Ripoti kuhusu mateso na uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa katika Gereza maarufu la Guantano linalo washikiria wahalifu wengi wa matendo ya Kigaidi uliamsha hisia kwa watetezi wa haki za binadamu duniani kote kuhusu uchafu unaofanywa na serikali ya marekani kwa watuhumiwa walioko huko gerezani Guantanomo Bay Cuba.
8. Meseji za 9/11 siku ya tukio la kulipuliwa kwa majengo pacha ya World Trade Centre na jengo la wizara ya ulinzi Washington. Kuanzia saa 1 kabla ya kulipuliwa majengo na baada ya masaa 24. Meseji zilizotunzwa kutoka Pentagon, FBIA, FEMA na NYPD zilichapishwa ili angalau kuwapa picha wananchi wa marekani kuhusu nini kilikuwa kinaendelea siku ya matukio hayo ambayo yalileta taharuki kwa ulimwengu na raia wa Marekani kwa ujumla. Zilikuwa ni meseji za watu wa kawaida wakijaribu kuulizana kuhusu nini kinaendelea katika siku ya matukio hayo ya kusikitisha zaidi ya meseji milioni moja zilichapishwa.
9. Kuvuja kwa taarifa juu ya uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2016. Kuvuta kwa meseji za siri kutoka kambi ya Democratic na mgombea wao Hilary Clinton na taarifa za wachangia wakubwa wa uchaguzi kwa kambi ya Democratic na jinsi chama kilivyomuunga mkono Hillary Clinton dhidi hujuma kwa mpinzani wake ndani ya chama Beny Sanders. Na speech ya Hillary Clinton kwa wafanyabiashara Wallstreet iliyoonesha anachoongea na wafanyabiashara ni tofauti anachowaambia wananchi wa kawaida. Watu wengi walitegemea Hilary Clinton kushinda lakini tofauti akashinda Trump watu wanajiuliza je uvujaji wa hizo data ulimsaidia kiasi gani Rais Trump kushinda.
10. Mauaji ya kinyama huko Iraq yanayofanya na majeshi ya marekani. Mwezi wa 4/5/2010 Wikileaks iliachia video zinazionesha ndege ya kijeshi ikiwapiga risasi raia huku marubani wakicheka kama wanacheza Video Game na cha ajabu zaidi baada ya kufanya mauaji hayo gari iliyokuja kubeba maiti na watu waliokuwa wakisaidia kubeba miili walipigwa risasi bila huruma na kuua pia mtoto aliyekuwa ndani ya gari. Ulimwengu ulishtushwa na yaliyokuwa yanafanywa na wanajeshi hao ambao ni uhalifu wa kivita na je mangapi tusiyoyaona yanayoendelea na kuleta hofu juu ya ubabe wa marekani kuvamia mataifa mengine na kuua bila sababu.
NB: Kutolewa kwa taarifa hizo kimmemfanya Julian Assange kuishi mafichoni ndani ya ubalozi wa nchi moja ya amerika kusini kwa muda mrefu mpaka alivitolewa kwa nguvu kutoka ubalozini baada ya ubalozi huo kumwambia aondoke kutoka na kuvunja baadhi ya utaratibu wa kukaa ndani ya ubalozi huo. Je mtu kama huyu inatakiwa apongezwe au atiwe kizuizini kama alivofanyiwa.
View attachment 1077703View attachment 1077704
The absence of evidence is not the evidence of absence.

Nimeupenda huu msemo wa mwisho
 
Back
Top Bottom