Julia Nyerere: Vitu ambayo vimenisaidia kuishi Tanzania baada ya kuishi Marekani kwa miaka 21

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,432
7,055
IMG_20210530_162448.jpg

Kwa mujibu wa Julia Nyerere, mjukuu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye amekuwa akiishi na kusoma nchini Marekani kwa miaka zaidi ya 20, yafuatayo ni mambo 13 yanayomsaidia kuweza kuishi Tanzania ambako amekuta mambo ni tofauti na alivyozoea huko ughaibuni.

Julia Nyerere:

1. Nimejifunza kubargain. Mtu akikwambia bei Marekani anakwambia bei halisi, TZ watu ambao wanatoa services wamezoea kwamba mtu atataka upunguze so anaanza juu automatically, the trick ni kudivide by 3 alafu unaanza kubargain ili mkutane katikati.

2. Nimepunguza kutoka na kufatana na watu ambao wanatoka kila siku. Sio kila mtu anatumia hela zake anapotoka (machawa) na kuna wengine wanatoka na hawanunui chochote. Ukijaribu kushindana na watu ndio utajuta.

3. Sio kila mtu anaetaka kuhang na wewe ni rafiki yako au yupo genuine, nimejifunza kutofautisha na imenisaidia kua na genuine circle.

4. Invest invest invest, fursa zipo kwenye kila sector. Ushindwe wewe tu!

5. Jiwekee mazingira mazuri nyumbani kwako ili usitamani kutoka mara kwa mara. Kama unapenda kuangalia movies, jiunge na netflix.

6. Jifunze kuomba msaada na ushauri kwa wazoefu, huwezi kujua kila kitu.

7. Usiamini kila kitu unachoambiwa. Hapa ndio wanadiaspora wengi wanapokata tamaa, wanaassume kila mtu atakua mkweli so wanatapeliwa kiurahisi. Hii inaapply kwenye biashara na mahusiano.

8. Subira ni muhimu sana, itachukua muda kuadjust, usifikiri kwamba utazoea kiurahisi.

9. Ukitaka kutumia hela, usiwaze kwa currency ya ulipotoka. Waza kwa shillings, itakusaidia kutumia hela kwa uangalifu zaidi.

10. Usifanye kitu chochote kwa shortcut, mambo yako yote ya nyooke, hata kama mtu akijaribu kukushawishi kwamba ni sawa usikubali. Haijalishi utaspend kiasi gani zaidi kufanya vitu the proper way, cheap is expensive!

11. Enjoy and usijinyime, pale unapoweza jitreat na enjoy kua nyumbani. Kuna sehemu nyingi za kuona na kutembelea nyumbani, pafaidi mpaka wanadiaspora wengine watamani kurudi nyumbani.

12. Mtu asikutishe kwamba hutaweza kusurvive. Bora nyumbani mara ishirini kuliko ugenini. Wapo watu kibao ambao sio watanzania wamehamia huku na wanaishi vizuri tu na wanafaidi mpaka mimi nawaonea wivu kwamba nimechelewa kurudi.

13. Sali sana na sali kila siku, Mungu atakuongoza na hawezi kukubali ufeli.
 
Yaani nyie kwa Mwalimu mngejua robo tu ya uzito wa jina la Babu/ Baba yenu na mkalitumia mngeshangaa sana. Hapo kwenu Mngeweza kulitumia vizuri jina la huyo Mzee kwa kweli mngekua mna nguvu na ushawishi mkubwa sana, Kama Familia ya Kennedy kule US, Lakini basi tena penye miti hakuna wajenzi.
 
Back
Top Bottom