Julai Mosi Ni Sikukuu Ya Mabenki-tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Julai Mosi Ni Sikukuu Ya Mabenki-tanzania

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mbangaizaji, Jun 27, 2008.

 1. M

  Mbangaizaji Senior Member

  #1
  Jun 27, 2008
  Joined: Jul 23, 2007
  Messages: 121
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Wakuu,

  Jumanne tarehe 1 Julai, imetangazwa kuwa itakuwa ni sikukuu ya mabenki(bank holiday) Tanzania na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania.Kwahiyo mabenki hayatafanya kazi siku hiyo, wenye shida ya kupata huduma za kibenki inabidi wapate huduma hizo jumatatu tu.Jumanne mabenki yote yatakuwa yamefungwa.

  Hamna sababu maalum iliyotolewa juu ya sikukuu hii maana hii si public holiday and all other industry will be working apart from banking. My question is is appropriate to have a holiday for only financial industry on a normal working day? Naomba tujadili maana hizi sikukuu naona zimekuwa nyingi sasa.

  Asante
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Bongo sikukuu ni kama kazi. Lakini haya mabenki yenyewe kimeo. Kutoa huduma ya mikopo kwa watanzania weusi ni kazi kweli. Hata sioni sababu ya mabenki yao haya. Mi nadhani watuache tuendelee kukopeshana kwenye tu saccos twetu vijisenti hivi vitatutosha. Mabenki yarudi ulaya yaendelee kuwakopesha waasia wao!
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Jamani, Sie Akina Mang'enya Hali Mbaya, Ukikopa Hata Tumilioni Tutatu Na Kubadili Ajira Wiki Hiyohiyo Unakuta Wanatutreat Kama Defaulters, Sijui Wenzangu Lakini Banking System Yetu Mbaya Na Hasa Kwa Wa Chini. Bahati Mbaya Zaidi Ni Hata Hao Loan Officers (no Disrespct) Ambao Hali Zao Ni Chovu Kama Zetu, Huanza Kuonyesha Attitude Kwa Mkopaji

  Sijui Tufanyaje Jamani, Mambo Mengine Tunayaleta Wenyewe
   
 6. H

  Haika JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  hii sikukuu ni ya kimataifa au Tanzania tu?
   
 7. K

  Kungurumweupe JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 317
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hii ni hujuma nyingine ya uchumi wetu. Malipo ya biashara kubwa kubwa hapa nchini hayakamiliki bila kulipa pesa bank. Kwa mfano makampuni makubwa ya mafuta hayawezi kuwapa wateja wao mafuta mpaka walipe pesa bank na zionekane kwenye account za hayo makampuni. Sasa wakifunga inamaana wamehujumu mapato ya hayo makampuni, na hujuma hii ina-reflect kwenye uchumi wa nchi.

  Nakwanini wafunge wakati kesho ni siku ya kazi?! Kuna kitu! HUU NIUFISADI MWINGINE!
   
 8. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Haya Masikukuu Ni Mengi Mno! Kesho Pia Ni Local Government Day! Nilidhani Kwa Kuwa Benki Hazifanyi Kazi, Nikafanye Site Inspection Kwenye Halmashauri Moja Mkoani Kilimanjaro. Nimeambiwa Wako Busy Kuandaa Maandamano Ya Local Govrnment Day! Jana Ilikuwa Siku Ya Cooperative Day! Hapa Moshi Mjini Niklikwama Kwa One Hour Kwa Ajili Ya Maandamano Ya Wanaushirika, Bado Wakulima Day! Law Day! Engineer Day! Surveyor Day! Eheeeeeeeeeeeeeee
   
 9. M

  Mbangaizaji Senior Member

  #9
  Jun 30, 2008
  Joined: Jul 23, 2007
  Messages: 121
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Sikukuu hii ni Tanzania tu.na givernor ametumia banking act ya 2006 kudeclare sikukuu kwa mara ya kwanza.Lakini sector zingine zote zinafanya kazi.Kwahiyo kesho kama unafedha za mauzo ziweke uchagoni mpaka jumatano
   
 10. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Swali ni kwamba kwa nini tarehe 1 yaani when people need access to their money, kwa nini ghafla kwa notisi ya masaa 24? Pia mtu wangu alipiga simu benki aliambiwa kwamba wafanyakazi wa benki wanakwenda kazini kama kawaida lakini hawata-deal na customers. Jamani tutafutieni data na sisi tutazidi kutafuta SOMETHING IS WRONG!!!!
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  MTM haya ya mabenki yetu yanatia aibu.
  Viongozi wetu kwa kuwa wao wana access ya kukopa bila maswali nakwambia hakuna anayejali nini kinaendelea kwetu.
  Ukienda benki nakwambia mlolongo mrefu wa mambo ya kufanya. Hiyo si kitu lakini unaomba millioni 30 unapewa 5 tayari malengo na mwelekeo wa shughuli yako imeharibika.
  Kibaya zaidi siku hizi wanakupa mkopo na kukudai urudishe mwaka huo huo yaani zaidi ya mwaka mmoja hawataki.
  sasa hiyo biashara ya kupewa mkopo leo ukaanza kulipa mwisho wa mwezi uoni kama ni biashara sawa na ya kuuza mchicha?
  Mara watakudai lazima uwe na nyumba. Na ukiwa nayo watataka uwe na hati. Ukiwa na hati watataka mwenyekiti wa mtaa atoe ruhusa kana kwamba yeye ndiye mliki wa nyumba yako.
  Sasa basi huwa najiuliza hawa ndugu waasia wa tanzania ambao hawana hata banda la kuku na wanaishi zile nyumba tuliwanyang'anya ndugu zao na wanazilipia kodi kila mwezi. Je hawa huwa wanatoa Bond gani?huwa wana mortgage nini? mbona wanapewa mamilioni na mamilioni ya shillingi?
  Mbaya zaidi wengine walikuja hapa kama wafanyakazi wa waasia wenzao na kwa njia za kifisadi wakaanzisha vijibiashara uchwala wa viji restaurant na vijiduka vya ajabu ajabu. Kesho akiomba mkooo benki zetu hazina shida naye zitampa tu maana muasia ni mtukuka. Ni hawa hawa wakina Manji, Patel, na wengine kama hao tunaoona skendo nyingi tu. Lakini omba wewe ngozi nyeusi. Waambie sina nyumba ila nina shamba la mihogo uone kama kuna mtu atakupa.
  Utaishia kuambiwa watanzania sio waaminifu. Sasa kama sisi watanzania wote sio waaminifu! basi bank zao waziamishie kwao huko sio kuja hapa kuweka pesa za wezi wa madini na misitu yetu hapa.
  Kisha hao waasia waende huko huko wawakopeshe. Sisi tuendelee na viji saccoss vyetu na siku moja tutajkomboa tu. Hatuwategemei wao tena. Wametukatisha tamaa.
  Kigumu chama cha mirija.
   
 12. H

  Haika JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Cheyo kasema ilitakiwa ipitishwa na bunge, lakini haikuwa hivyo!!
  Huu ni uwajibikaji mbovu mwingine?
  Pia hii sikukuu nasikia ipo nchi kadhaa, lakini kwa tanzania ambao tunaishi hand to mouth, tarehe moja si siku nzuri ya kufunga benki hata kidogo.
  Jana kulikuwa na foleni kubwa hadi atm zikawa zinaharibika ovyo.
  Hili ni wazo jingine la kijinga.
  Lakini je ni authority gani ambayo inatakiwa kuthibitisha kikundi cha watanzania kisifanye kazi siku ya kawaida ya kazi?
   
 13. B

  Boma Senior Member

  #13
  Jul 1, 2008
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 190
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli Governor ka-bore sana. Kama alitaka KUONYESHA UMMA WA WATAZANIA KWAMBA ANAUWEZO WA KUTOA MAPUMZIKA kwenye sector ya mabenki bila kujali watu tunaadhirika na uchumi wa nchi siku nzima.

  Hivi benki transactions zina-contribute kiasi gani kila siku katika uchumi wa nchi.???
   
 14. M

  Mnyoofu Senior Member

  #14
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Jamani mlieko Bongo Mabenk ni kweli yamefungwa leo? Hata siamini na ninaamini haiwezekani kwasababu hii iko kisiasa zaidi na si-kibiashara. Na kama wasipofunga what will they loose, I dont believe Gavana atawasurutisha!

  Mie ningekuwa MD wa one of the Banks I would ve gone against. Coz I believe would ve made serious Bingo to open, if at all banks had to close down! Satisfying your customers must be a focus not politicians!

  Sanasana wanerembesha na kufanya a big display ma-bank yao badala ya kuyafunga!
   
Loading...