Julai 5, 1996: Kondoo wa kwanza aliyeumbwa kwa njia ya kurudufu (Clone) duniani alizaliwa

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,008
1,032
VCG31N636251140.jpg

Dolly ni kondoo jike aliyeumbwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kurudufu (Clone) na Taasisi ya Utafiti ya Roslin ya Scotland na Kampuni ya teknolojia ya viumbe ya PPL Therapeutics. Kuzaliwa kwa Dolly kumeweka msingi wa maendeleo ya teknolojia ya viumbe vya kurudufu (Clone), na kuibua mawazo ya watu ya kuumba binadamu kwa kutumia teknolojia hiyo, na pia kuzua mjadala wakati aliposifiwa.

Dolly alizaliwa Julai 5, 1996, na habari kuhusu mafanikio hayo ilitangazwa hadi kufikia Februari 22 1997. Magazeti ya sayansi yaliorodhesha mafanikio hayo kama matokeo muhimu ya sayansi na teknolojia kwa mwaka huo. Februari 14 2003 Dolly alikufa kwa njia ya euthanasia kutokana na ugonjwa sugu wa mapafu na baridi yabisi.
 
Back
Top Bottom