Jukwaa la Wahariri Watoa Tamko Kali Kufungiwa Gazeti la Mawio

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,262
2,000
Jukwaa la wahariri Tanzania, limetoa tamko lao kuhusu uamuzi wa Waziri Harrison Mwakyembe kulifungia Gazeti la Mawio. tazama Live
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesema kuwa kitendo cha serikali kulifungia gazeti la MAWIO ni dhidi ya uhuru wa habari.
TEF imeahidi kuendelea kupinga vitendo vya uonevu vinavyofanywa dhidi ya vyombo vya habari, vikisema ni sehemu ya ukandamizaji wa uhuru wa habari na uvunjifu wa sheria, inayosimamia sekta ya habari nchini.

kwa mujibu wa vyanzo vya habari Tanzania, Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga ametoa kauli hiyo Jumanne na kushauri uongozi wa gazeti hilo kwenda mahakamani kwa kuwa wanayo fursa ya kufanya hivyo.

Amesema uchambuzi uliofanywa na jukwaa hilo umebaini kuwa kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, kinatoa mamlaka kwa Waziri husika kuzuia maudhui katika habari na si kufunguia chombo cha habari.

Makunga amesema kwa kuzingatia uchambuzi waliofanya ni wazi kuwa mchakato ukiotumika kulifungia gazeti hilo umekiuka sheria.
 

Akili 09 Nguvu 01

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
517
1,000
Habari ilivofanya gazeti la Mawio kufungiwa inafanana sn na habari iliyopo kweny gazeti la Mwelekeo la wiki iliyopita cha ajabu gazeti la Mwelekeo lipo tu lakin Mawio limefungiwa
 

Imany John

Verified Member
Jul 30, 2011
2,907
2,000
Wangeafikiana juu ya kumfuta waziri husika,kama walivyofanya kwa mkuu wa mkoa wa dsm.
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,880
2,000
Nani anaye-oversee hili jukwaa la wahariri?tunapolishwa habari mbovu hatuwasikii
 

Graph

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
2,751
2,000
Hawa wa vyombo vya habari wanafiki tu, na waoga.
Wangekua wana ushikamano baada ya mawio kufungiwa ilitakiwa siku inayofuata magazeti yote na vyombo vya habari vingine waprint kilekile walichoprint mawio ili mzee wa PhD ya hasira afungie vyombo vyote tuone. Sio analeta double standard hapa.

Hadi mahakama sasa haipo independent inaendeshwa na mr. hasira, hili hata kulipeleka mahakamani wataambulia nothing.
 

Mkwere Sumbawanga

JF-Expert Member
Sep 28, 2015
684
1,000
Wamfanyie aliyefungia kama walivyomfanyia yule wa kolomije, ilifanya kazi hadi Leo inaonekana impact yake kwa aliyefungiwa kurushwa au kuandikwa na vyombo vya habar
 

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,179
2,000
Wasiziandike habari zake huyo haoni umuhimu wa kukosolewa,tatizo anachuki na gazeti hilo wala sio kilichoandikwa na gazeti
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom