Jukwaa la Wahariri(TEF), lataka majeruhi ajali ya moto Morogoro washitakiwe

Hivi wahariri watanzania? Desperate times call for desperate action- risk one's life in pool of explosive fuel mwanangu aende chooni.
 
Wakati mwingine ndiyo maana,na ilaani elimu na kuwaonea huruma sana wazazi walisemomesha watoto ambao hawana faida katika jamii,waliokufa katika ajari umeambia kuna walioenda pale kwa ajili ya kusaidia wengine moto uliwafwata,wewe unapata wapi ujasiri wakusema washtakiwe,watanzania MNA nini, iko wapi nguvu ya elimu zenu,mmejifunza nini shuleni,rudini shuleni mkawadai walimu pesa zenu inavyoelekea wajawafunza chochote na hela imeenda
 
Balile anajipendekeza, bila shaka anatafuta uteuzi. Kwa umaskini wa watanzania uliopo ktk awamu hii alitegemea wananchi wafanye nn?

Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa!
Eti umasikini Wa watanzania uliopo awamu hii,vipi awamu za nyuma hakujawahi kutokea matukio kama haya? Acha kujitoa akili kwa kuhalalisha uporaji,naunga mkono hoja hawa watu washitakiwe
 
Balile anajipendekeza, bila shaka anatafuta uteuzi. Kwa umaskini wa watanzania uliopo ktk awamu hii alitegemea wananchi wafanye nn?

Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa!
Hawezi kupata uteuzi kwa kauri hiyo ya ajabu. Magufuli ameshasema " sio wote waliokwenda pale walienda kuiba wengine walienda kuokoa, wengine kushuhudia , wengine wanapita tu n.k
 
Ina maana jukwaa la Wahariri linaamini waliokuwa eneo la tukio wote walikuwa wanaiba Mafuta au moto ulichagua wezi tu?


Hawa ndio maana Makonda aliwageuza geuza alivyotaka kipindi kile
Wahariri gan wanakurupuka bila kufanya extensive study ya tukio badala yake wanatumia hisia za kienyeji kuhukumu waķiwa Dar?Hao ndo wanaojiita mhimili wa nne et,,,Nyambafu
 
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kushtushwa na taarifa za vifo vya Watanzania zaidi ya 60 walioungua moto wakati wakichota mafuta kutoka katika lori lililopata ajali eneo la Msamvu, Morogoro, jana Agosti 10, 2019 likitaka waliojeruhia kushitakiwa watakapopona majeraha yao.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana usiku Jumamosi na Kaimu Mwenyekiti Jukwaa hilo, Deodatus Balile ilisema vifo hivyo vimetokana na tabia mbaya iliyojengeka kwa baadhi ya watu kuchukulia ajali kama fursa ya kujipatia mali kwa njia haramu iliyoanza miaka ya hivi karibuni.

“Tumeshuhudia picha za watu waliofariki kwa kuungua moto zikirushwa kwenye mitandao ya kijamii kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na upashanaji habari. Tunakemea tabia hii na kuitaka jamii iache mara moja tabia hii ya kinyama isiyo ya utu,” alisema Balile.

Balile pia alizungumzia watu zaidi ya 70 waliojeruhiwa katika ajali hiyo akisema wakipona wajiepushe na tabia hii ya uporaji.

“Ikilazimu, wote watakaopona katika ajali hii washitakiwe kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwao na wengine kuwa ikitokea ajali tunapaswa kusaidia majeruhi na kuokoa mali zao badala ya kupora,” alisema.

“Tunaomba viongozi wa dini, wazazi, viongozi wa kisiasa na jamii kwa ujumla itumie ajali hii kufundisha watoto na vijana maadili mema ya kuwa watu wa msaada mtu anapopata ajali kwa kusaidia majeruhi na kuokoa mali za waliopata ajali badala ya kuwapora,” aliongeza.

Hadi jana usiku, watu 64 walikuwa wameripotiwa kufariki huku 70 wakijeruhiwa ambapo baadhi ya majeruhi wamelazwa Hospitali ya Morogoro na wengine wakihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Chanzo: Mwananchi
Balile umenichekesha Sana eti tabia hii mbaya imeanza hivi karibuni
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom