Jukwaa la Siasa lisilojaadili Siasa!! Uvivu wa Kufikiri na Hoja za Kufuata Mkumbo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jukwaa la Siasa lisilojaadili Siasa!! Uvivu wa Kufikiri na Hoja za Kufuata Mkumbo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 10, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukisoma kwa makini hoja zinazoletwa huku ni malalamiko ya siasa na siyo siasa! Majadiliano ni kuhusu CDM, CCM, CUF, NCCR na TLP! Wengi hawajui hata hivyo vyama vinasimamia nini. Suala kwamba inawezekana hivyo vyama havina vinachosimamia ni tofauti na WanaJF kutokujua kwamba hakuna vinachosimamia! Wavamizi kutoka facebook na kwingineko kazi yao ni kuweka comments kama 'crap' 'duh' na 'wagalatia' 'urojo'!

  Majadiliano ya kuhusu siasa yamegeuzwa taarifa na upashanaji habari! Utasikia 'chadema watoka ukumbini' ccm mara waula' 'lowasa fisadi' 'mbowe mwenyekiti wa CDM' 'JK Raisi wa Tanzania' 'Pinda aenda Malawi' 'January Makamba sio Mtoto wa Makamba'

  Sasa hapo ni siasa au taarifa za siasa? Mtu si unaweza ukapost hata jukwaa la mapenzi au ukawataarifu na huko wajue Pinda kaenda Malawi! Utasikia mtu anasema Pinda ni Mwanasiasa lazima tunjadili!!

  Inapofika wakati wa hoja ngumu ndipo utajua mawazo ya watu humu ndani! Ikianzishwa thread ya 'Uchumi wa Tanzania wazidi kuporomoka: nini kifanyike' utaona idadi ya wachangiaji!! Hakuna mawazo yatakayotolewa sana sana utasikia 'kazi yao kulipa dowans' 'ccm iondoke madarakani (as if mtu hajui sheria inasemaje) 'slaa ndio raisi'

  Sasa unajiuliza uchumi utakuwa kweli? Great thinkers ndio wameshafikiri hivyo!!

  Tatizo letu tunaelekeza hasira zetu kule ambako sio! Hatukai chini kujipanga tufanye nini kupiga hatua! Tunatumia muda mwingi kupata taarifa ambazo hatuna cha kufanya zaidi ya kuongeza hasira!

  Tunakuwa wagumu kutoa mawazo yetu kujenga chama chochote tunachoona kinafaa. Tunakuwa wepesi kutetea vyama vyetu hata kama vinakosea! Tunasahau kwamba CDM haiwezi kuanguka kisa imekosolewa! CCM haiwezi kutoka madarakani kwa kutukana!!

  Yaliyotokea bungeni yanadhihirisha nafasi ya jukwaa hili katika siasa za nchi yetu! Wengine tunasupport kwa nguvu vyama vya upinzani kuungana as if vyote vinapinga! Eti CDM wakubali kugawana nafasi na wengine!! Wengine hao ni Mrema na Cheyo!! Au Kafulila na Hamad Rashid!! Ni muungano gani huo kama sio unafiki?? Tumefikiria kwa kina kabla ya kuulilia huo ushirikiano?

  CDM na vyama vingine kila kimoja kina sera na mitazamo yake. Hakuna mtazamo wa pamoja hata kama ni kuing'oa CCM! Wenyewe kwa wenyewe wanapingana na hiyo ndio concept ya vyama vingi!

  Tatizo la CDM ni kutokusimamia ukweli kwamba 'kila chama kisimame kwa miguu yake na kitekeleze au kisimamie sera zake'. Hakukua na sababu ya kutoa kisingizio kwamba CUF wameungana na CCM Zanzibar na vyama vingine ni rafiki wa CUF hivyo hatushirikiani navyo!!

  Hakuna kosa kusimama na kutamka hilo. CDM ni CDM na CUF ni CUF! Kama ilishindikana kushirikiana wakati wa uchaguzi inawezekana vipi wakashirikiana kwenye Bunge? Huo utakuwa ni unafiki!

  Mawazo yangu kama MwanaJF, tuache kuligeuza hili kuwa jukwaa la taarifa za siasa, matusi, uvivu wa fikra, kutolea hasira nk!! Hili ni jukwaa la kushusha nondo za siasa zitakazosaidia kuleta mabadiliko katika nchi hii. Ni sehemu ya kuonyesha tofauti yetu na wao!

  Kunawatakaokurupuka 'umetumwa' 'wale wale' na mengineyo! Sijatumwa!

  Kwa faida ya ukweli na uwazi mimi ni mwanachama hai wa CDM. Siwapendi CCM kwa sababu ya kushindwa kwao kuwasaidia wananchi wa Tanzania kufikia ndoto za uhuru. Ni chama dhaifu, hakina dira wala muelekeo. Hakijui kinasimamia nini! Viongozi wake wamefika mwisho wa kufikiri. Hawana viongozi mbadala ndio maana mtu anaweza kujiuzulu na akarudi kuwa mwenyekiti wa kamati. Mtu anaweza kuwa mwizi na akawa mbunge hata kama ana kesi ya kujibu!


  CDM ni chama ambacho kimekuwa na kinaendelea kukua. Kinatoa nafasi ya mawazo mapya. Maamuzi ya Wabunge wa CDM sio lazima yawe maamuzi ya CDM ndio maana kuna kamati ya Wabunge. Endapo Wabunge hao watatoa msimamo ambao ni kinyume na yale ambayo CDM inasimamia hata wao sio zaidi ya Chama, watawajibishwa kwa ujumla wao na mmojammoja! Huo ndio uongozi!

  Hayo ndio mawazo yangu!
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  I cant say naweza kubisha sababu on the same token na definition yako ya siasa hata hii post sio siasa bali ni malalamiko ya post za wengine...
   
 3. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  duh...sasa jamani kama tumeipenda post yako tusigonge thanks???....mi nimeipenda post yako, ila naogopa kugonga THANKS (duh nimeshasema, ila siwezi kuiita crap).........halafu mkuu maneno mingi sana, nimesoma nusu tu nikachoka. summarize basi eh?
   
 4. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is one of the most useful post JF has ever received.Asante kaka!

   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mkuu hizi alama za kushangaa niaje? Manake naona zipo all over hata sehemu nyengine sijui unashangaa nini.
   
 6. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  By the way hizi habari ungetaka ziende Jukwaa gani?
   
 7. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mods waweke 'jukwaa la taarifa za siasa' au waweke 'taarifa za magazetini' au utoe mawazo yako VoR
   
 8. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii post yako imeonyesha uwezo wako mkubwa kufikiri. At least nina uhakika VoR hujavamia kutoka facebook! Thank you kwa angalizo!
   
 9. s

  simanjiro Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka yote uliyolalamikia ndio mambo yanayotokea kwenye majukwaa... tofauti ya mitazamo, uelewa na fikra ni kitu cha kawaida katika majukwaa hasa hasa yale ambayo hayana udhibiti wa sifa za kuwa mwanachama.
  ukiangalia ni kwamba jukwaa la siasa ndio linalotembelewa sana hapa JF kwahiyo lawama hizi ulipaswas uzielekeze kwa Moderators ambao kwa tafsiri ya haraka haraka ndio waliopaswa kuratibu nini kinawekwa wapi na sio waandishi. hata hivyo moderators wanajitahidi sana kuhamisha hizo posts sometimes lakini nahisi wanazidiwa na uwingi wa post hizo.

  kwa hiyo mimi nadhani tuvumiliane tu na labda katika kusaidia kuondoa tatizo hili tukubaliane kuwa na tafsiri ya siasa hapa JF, ikubaliwe na wote na Moderators waiweke sehemu ambayo watu wote wataweza kuisoma. hilo huenda likasaidia.
   
 10. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Simanjiro ahsante. Sasa nashindwa kuelewa kwa nini Simanjiro hakuna maji na wewe upo? Na Mh. Sendeka alishindaje? Kwa mawazo yako na uelewa wako ungefaa sana kuwa kwenye nafasi ya Sendeka kupitia CDM.

  Nakubaliana nawe kamanda.
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  umeongea vitu vya maana lakini sikupi 'thanks' kwa sababu na yenyewe unaiona kama chai.
   
 12. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Makandokando, ipo moja fupi 'Firstlady yuko wapi' na nyingine 'January sio mtoto wa Makamba'....kwa nini usisome hizo?

  Hizi ndefu sio lazima kwa sababu ni ndefu na hazihitaji ushabiki! vinginevyo kila nilichoandika ndicho ninachofikiri!
   
 13. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  crap! oooh sorry, thanks.
   
 14. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa waungwana mnaniadhibu kwa kutoa mawazo? Nigongeeni thanks jamani! Nimerekebisha kauli!

  Ghafla nimekumbuka kuna rekodi humu ndani,

  Join date: 2006
  Posts 4,563
  Thanked 3
  Thanks 1,023
   
 15. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe kwa 90%,mana kuna kitu kinaotwa low politics na high politics,inavyoonekana wewe unataka humu ndani tujadili high politics tu me nazan hata low politics zinahitaji kujadiliwa pia
   
 16. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kapotolo dawa yako moja tu! Mama Makinda! Mi sasa hivi nawapeleka kwa Bi. Mkubwa maana yeye kazi yake moja tu 'kusimamia na kuchochea hoja dhaifu'
   
 17. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  i
  nimeipenda hii mkuu, nimekugongea thanks
   
 18. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Madcheda, this is what I wanted to trigger. A constructive discussion. If you don't mind, drop a line about high and low politics. Teach us. That will enlighten us and that way we will know when to use high or low politics humu jamvini.
   
 19. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umejitahidi lakini umeteleza pia. Kusema kuwa wewe ni mwanancha hai wa CHADEMA, halafu pia CHADEMA hakijaweka wazi kuwa kila chama kinatakiwa kisimame kwa miguu yake unakuwa hueleweki vizuri.

  Mimi sio mwanachama wa chama chochote kile, lakini huwa nafuatilia mambo ya siasa. Kwa wewe kusema kuwa CHADEMA hakijaweke wazi kuwa kina sera, imani na mwelekeo tofauti na vyama vingine ikiwepo CUF mimi naona sio kweli, ili limefanyika sana. Kwa hiyo usiseme hawajasema hilo. Kwa mfano tu tafuta mchango wa Halima Mdee kwenye ule mjadala wa kubadilisha tafsiri, alisema wazi kabisa kwa kuna tofauti katika ya CHADEMA na CUF na vyama vingine hivyo kulazimisha ushirikiano sio sahihi.

  Na nina imani watu wengi wanaelewa CDM wanakataaa kushirikiana na vyama hivyo kwani kuna tofauti nyingi miongoni mwao.

  Halafu kitu kingine usilazimishe watu wajadili mambo ambayo hawana interest nayo. Mambo ya uchumi kama mtu hana interest nayo hatajadili ya nini? Kwa mfano kama mimi ni mtu wa football nitajadili basketball ya nini?

  Unatakiwa kujua siasa inaweza kuwa muhimu zaidi ya uchumi kwa watu wengine. Ukiuliza watu kati ya siasa na uchumi nini kinaanza? wengine watakuambia siasa kwanza baadaye uchumi. Ndio maana wanataka viongozi bora wa kisiasa ili washughulikie uchumi. Wengine watakuambia uchumi kwanza, siasa baadaye. Wengine watakuambie lazima vyote viende pamoja. Wengine hawana interest kabisa na siasa wala uchumi.

  Kimsingi hakuna mada muhimu kuliko nyingine in general, ila muhimu wa mada unatokana na mtu mwenyewe. Mimi nikinunua gazeti naanza kusoma habari za michezo, mwingine anaanza na ukurasa wa kwanza, mwingine anaanza na matangazo ya kazi na tenda, na mwingine hivyo hivyo tofauti. Lakini wote mwisho wa siku watakuambia wamenunua na kusoma gazeti.
   
 20. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku zote mtazamo wa mtu hauhitaji kuhojiwa. Unapokuwa na mtazamo wa jambo fulani, hicho ndicho kitu unachokiamini kuliko jambo lingine kuhusu hoja husika. Binafsi nakubalina na mtoa hoja katika hali ya kutokukubaliana naye maana kusema crap, thanks, etc ni mitazamo tu ya watu huenda wao waliwahi kusoma mambo ya shorthand, sasa ulitaka wasemeje zaidi ya hapo? Maana kwao, neno crap lina maana kubwa sana.

  Nakubaliana na uvivu. Na tatizo hilo ni kubwa nchini. Fanya zoezi mpelekee barua yenye page 3 mtu unayemfahamu, mwambie soma sasa hivi na unipe majibu. Atapitia pitia tu, dakika 1.5 atakwambia eeh, nimekuelewa. Na atatoa jibu litokanalo na kichwa cha habari tu.
   
Loading...