Jukwaa la katiba tanzania wanagombana na sheria na siyo kamati-jaji waryoba.

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Mwenyekiti wa kamati ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya, Jaji Joseph Sinde Waryoba amesema kamati yake ipo kwa mujibu wa sheria na muda uliopangwa kumaliza kazi yake pia upo kisheria na kinachofanywa na kamati hiyo ni kuhakikisha inawafikia wananchi kwa wakati.

Jaji Waryoba ameyasema hayo siku chache baada ya kamati ya jukwaa la Katiba nchini kutoa kauli kuwa hakuna haja ya kamati ya waryoba kuwa na haraka na kinachotakiwa ni kufanyia marekebisho vipengele vya uchaguzi ili uchaguzi wa 2015 uwe wa huru na haki.

Waryoba amesema kauli hiyo ya Jukwaa la siasa ni KUGOMBANA NA SHERIA NA SIYO KAMATI YAKE.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom