Jukwaa la Katiba: 'Ni ndoto Katiba mpya kupatikana 2014' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jukwaa la Katiba: 'Ni ndoto Katiba mpya kupatikana 2014'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Informer, Oct 4, 2012.

 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,437
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Christina Gauluhanga na Maneno Selanyika, Dar | Mtanzania | Oktoba 04, 2014

  JUKWAA la Katiba Tanzania limesema ni ndoto kwa Katiba Mpya kukamilika Aprili 12, mwaka 2014, kama ilivyoahidiwa na Serikali. Tathmini hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deus Kibamba, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

  Kibamba alisema, kutokana na utafiti uliofanywa katika mikoa mbalimbali, jukwaa hilo limebaini ni vigumu, Katiba hiyo kupatikana kwa wakati kutokana na utaratibu mbovu uliopo.

  Alisema muundo uliopo hivi sasa, unawanyima haki baadhi ya wananchi kutoa maoni na kusema kuwa, ni vigumu kukamilika haraka ukusanyaji wa maoni ya muundo wa Katiba mpya.

  “Tume ya kukusanya maoni ya muundo wa Katiba mpya, imeonesha wazi haiwezi kukidhi matakwa ya baadhi ya wananchi kutokana na muundo uliopo.

  Alisema utaratibu wa sasa haujawapa uwezo wa kutoa maoni walemavu wa masikio, macho na wale wa ngozi, hivyo kundi hilo limenyimwa uhuru wao wa kutoa maoni kwa ajili ya Katiba mpya.

  “Naomba kusisitiza hili, tume lazima ifanye kazi kwa umakini, kwani inaonesha makundi haya maalum yametengwa na yanatakiwa kupewa uhuru wao.

  “Ni muda mwafaka kwa tume kutafuta wataalam wa alama kama ambavyo walishauriwa, ili kuwapa haki ya msingi walemavu wa kutokusikia kutoa mawazo yao,” alisema Kibamba.

  Aliongeza katika mikoa 15 ambayo hadi sasa tume hiyo imepita kukusanya maoni, yapo maeneo mengi ambayo tume hiyo haijakutana na wananchi, hivyo muda zaidi unahitajika.

  “Ninachofikiria hapa tume hii inasukumwa na baadhi ya wanasiasa ambao wana maslahi ya kukamilisha ripoti ya ukusanyaji maoni ya muundo wa Katiba mpya, kwa maslahi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,” alisema.
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Sijui Warioba anafikiria nini?

  Maana hadidu za rejea za tume zinanyima uhuru wa kujadili muungano, lakini yeye anaruhusu. Sasa kama tunaotaka Tanganyika tuko wangi ataandikaje katiba?

  Hadidu za rejea zinatakiwa kurekebishwa haraka ili kwanza muundo wa serikali na katiba zake ujitanabahi.
   
 3. M

  MR.PRESIDENT Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani mlikuwa hamjui hilo?mwenye macho haambiwi tazama
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye bluu, wengine tulilizungumzia hili (la Hadidu za Rejea kwamba zitoke kwa Wadau wa Katiba na wala zisitoke Magogoni) kipindi kirefu sana hata kabla muswada haujapelekwa bungeni lakini hatukusikilizwa.

  Ni hatari kubwa sana endapo Katiba Mpya ya WANANCHI isipoptikana KWA UBORA WAKE NA WAKATI sahihi.


   
 5. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Labda ni kwa kutokujitambua kwa JK lakini katika mambo ambayo yangemfanya akumbukwe kwenye utawala wake ni kulipa taifa katiba mpya maana nikitu iliyopigiwa kelele kwa muda mrefu.

  Watawala wakiondoa hofu mioyoni mwao na kuwapa watanzania haki yao ya kusikilizwa itawarahisishia kuongoza bila kua na misuguano mikubwa inayolisababisha taifa lisisonge mbele.

  Ifahamike taifa sio mali ya mtu binafsi tunajua nakuamini hata wao wasiporuhusu upatikanaji wa katiba kwa wakati ipo siku taifa na watanzania wataipata katiba waitakayo sio vibaya wakafahamu kua kasi na vuguvugu la mabadiliko duniani lipo juu na kuna madhara makubwa kupoteza muda wakulizuia kwa uhuni wanao tumia.

  Kuna kero nyingi sana na zamsingi kwa sasa ambazo zinahitaji kushughurikiwa tukianzia kwenye muundo waserikali hadi kwa waongozwaji (waburuzwaji)lakini wao kwa kutokujali huona propaganda bado zinaweza kua na nafasi kwenye mambo ya msingi hasa ni kwa masrahi ya wachache hapa sinaneno kama watafanikiwa kumfanya mtawaliwa kuendelea kuvumilia ila napata hofu pale watawaliwa watakapoamua na kusema tumechoka kuburuzwa kwa sauti moja naamini huu utulivu tulio nao unaweza kuwabidhaa adimu...

  Madhara ya watu wanaodai haki zao zilizonyang'anywa na watawala duniani kote yana faamika tafadhari Rais wangu kikwete naamini ukiamua unaweza ingawa najua umeshashindwa na wewe mwenyewe ulishawahi kututhibitishia hilo tafadhari usiruhusu kushindwa na hili watanzania tunakuomba usitufikishe tusipopahitaji....
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
 7. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Michakato na elimu yote imekufa, tumegeukia NEC na CCM kwa sasa. Ama kweli Tanzania HAKUNAGA
   
 8. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Nyinyi msituchanye na hicho kijukwaa chenu cha katiba, tume ya warioba inakwenda kwa zamu imepanga ratiba , kibamba anacheza na akili zetu huku akitumika haiwezekani tume imeshatumia pesa kingi halafu leo unatuambia hatutapata katiba nzuri!!!!!!!!!!! hii ni ajabu na kweli kama alijua hayo kwa nini hakusema leo amepewa mshiko anataka kusema muda hautoshi.

  My observations
  Nimegundua huenda CCM wamegundua kuwa katiba ya ukweli inakuja sasa waanza kuwatumia wanaharakati ku-frustrate mchakato.Wamegundua kuwa warioba kaamua kufanya kweli sasa wanaanza kuleta sababu.Acheni katiba itengenezwe hadi watoe draft ndipo tutaona kama kuna makundi hayajaguswa.Mimi kila siku nafuatilia gazeti la mwanachi ukurasa wa katiba wanachi wanatoa maoni mazuri sana tena yenye kukidhi mahitaji kabisa, mh. warioba anatukanwa sana huko vijijini na watoa maoni wakitaka tume ifanye kazi kwa mujibu na si kuwashurutisha watoa maoni.Yote haya yanadhihirisha kuwa uelewa wa wananchi ni mkubwa na hivyo nafasi ya kuchakachua maoni ni finyu sana kwa tume.Baada ya kugundua hayo Warioba amerudi ktk mstari ili kuepusha balaa huko mbeleni.Lakini kwa upande mwingine ccm wamegundua kuwa hata hiyo tume ya Lubuva itakayofanikisha uchakachuaji matokeo ya uchaguzi haitakuwepo tena, sasa wanaona jua linazama na ndipo wanaanza kuwatumia akina KIMBAMBA ili mchakato usiendelee eti muda hautoshi.Wananchi wamesema hawataki RAIS kuteua, uteuzi ufanywe na wengine, tume ya uchaguzi lazima ifutike ile ya kuteuliwa na JK sasa uchakachuaji wapi na wapi????? KIBAMBA TAKE CARE
   
 9. S

  Savannah JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "..walemavu wa masikio, macho na wale wa ngozi, hivyo kundi hilo limenyimwa uhuru wao wa kutoa maoni kwa ajili ya Katiba mpya...." Kwanza kuna taasisi zinzotetea/kusimamia haki za makundi kama haya. Je, haziwezi kuhakikihsa haki za msingi za makundi hayo yanakuwemo katika katiba?.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Of course inaweza kupatikana lakini haiwezi kuwa tayari kutumika kwa uchaguzi mkuu wa 2015. Hili dude limerushwa kwa wananchi kama njia maalum ya kuzuia push ya mabadiliko ya mambo ya uchaguzi kwa kutumia mchakato huu. Sasa hivi siyo CDM wala watu wengine wanaofikiria kubadilisha mfumo wa uchaguzi nje ya sheria za sasa.
   
 11. M

  Magesi JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huu ni udhaifu mkubwa wa kmkakati ndani ya chadema katiba mpya kwa uchaguzi wa 2015 ni lazima kuwe na njia mbadala kuhusiana na chaguzi zote zinazofuata
   
 12. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Itapatikana, but itapigwa chini katika kura ya maoni...
   
 13. M

  Magesi JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tatizo ni njaa za wanaharakati wetu hawana nia ya kweli na wanayoyasimamia na kuyahubiri mbele ya umma hawa wapo kulinda maslah ya c.c.m
   
 14. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huu ni mchezo wa kuigiza tu, kenya hawakufanya hivyo? Lakini kitaeleweka tu. There is a right time for everyting.
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuna dalili Katiba Kandamizi kutumika kulazimishwa kutumika uchaguzi mkuu ujao; wanaharakati hili tunalipinga kwa nguvu zote na CHADEMA kianze kuwauliza wananchi aina za HADIDU ZA REJEA ambazo wangependa zitumike kuongoza zoezi hili.
   
Loading...