Jukwaa la katiba mtaani tunasubiri tarehe ya maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jukwaa la katiba mtaani tunasubiri tarehe ya maandamano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kisiya Jr., Nov 29, 2011.

 1. Kisiya Jr.

  Kisiya Jr. Senior Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao. Na kwa mjibu wa katiba ya Tanzania,watumishi wote wa UMMA hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama cha siasa. lla tumeshuhudia mambo ya ajabu sana kwa siku za karibuni. Polisi wameonekana wakijishughulisha na propaganda za kisiasa iwe kwa makusudi au kwa amri. Mfano Jukwaa la katiba walipotangaza maandamano siku ya jumamosi tarehe 26 nov.

  UVCCM nao wakatangaza maandamano yasiyo na kikomo kusifia hotuba ya Rais,pamoja na kujua wazi dhamira ya hao magamba wadogo,wakaahirisha maandamano hayo kwa madai kwamba makundi mengi yameomba kufanya maandamano siku moja,kwhiyo polisi hawawezi kulinda.

  Binafsi nilijua kwamba polisi watatumia busara kwamba kwa kua jukwaa la katiba waliwahi kuomba kwahiyo ndiyo wanastahili kuruhusiwa yaani "COME FIRST,FIRST SERVED",Ila police wakavumilia upuuzi wa CCM.

  Hii inaonesha wazi kwamba police wamesahau wajibu wao wa kikatiba wa kulinda raia na mali zao na sio kulinda CCM na na ufisadi wao. zamani majeshi yote yalikua yanaunda mkoa wa CCM, sasa ndugu yangu KOVA ina maana hujui kwamba tupo kwenye vyama vingi?

  Ndugu DEO KIBAMBA mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba ulisema kama polisi wasipo tangaza tarehe rasmi ya maandamano wewe utatangaza tahere hiyo ulipohojiwa na BBC. Binafsi sina wasiwasi na wewe ila huko mtaani wananihoji kwamba umesahau ahadi yako? Kama umesahau nitumie fursa hii kukumbusha.

  Naomba kuwasilisha hoja.
   
 2. mkada

  mkada JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  tuwe na subira wajameni,hebu tusubiri kama mheshimiwa atasign huo mswada kwanza,manake mi naona kama anatishia nyau.
   
 3. Kisiya Jr.

  Kisiya Jr. Senior Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna kusubiri hapa,kawapooza CDM kwamba mswada atausaini ila kwakua sheria itaweza kufanyiwa marekebisho wasubiri serikali itafakari mapungufu hayo. sasa kwanini asaini muswada wenye makosa kwa makusudi?
  Hii ndo nafasi pekee tuliyonayo tukiikosa ndo basi.
   
Loading...