Jukwaa la Katiba limeazimia kukutana na John Pombe Magufuli juu ya katiba mpya

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Jukwaa la katiba ambalo kazi yake kubwa kuratibu maswala ya katiba, leo limetoa msimamo wao kwa mwenendo wa katiba iliyosimama kwa lengo la kuhamasisha iweze kusimaiwa iili ipatikane katiba mpya.


Jukwa hilo liliratibu mkutano mkubwa watu zaidi ya 150 waliweza kuhudhuria wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, wabunge, viongozi wa dini pamoja na asasi za kiraia. Lengo lilikuwa kuwakumbusha juu ya katiba ambayo imesimama. Maadhimio ambayo Jukwaa imeyaona pamoja na kuomba kukutana na Rais John Pombe Magufuli lengo likiwa kumueleza namna katiba ilivyomuhimu kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2020.



Kwa nafasi aliyo nayo John Pombe Magufuli kikatiba yeye ndiye mtu pekee kwa sasa mwenye uwezo wa kuamua hatma ya kuokoa ama kuangamiza mchakato wa katiba. Licha ya kuomba kukutana na mkuu wa nchi pia jukwaa limeazimia vyombo wa habari kupata fursa ya kutangaza kuwezesha kuendelea kutoa elimu juu ya hsitoria ya mchakato wa katiba pamoja na muadhui ya katiba.

Pia imeomba Waziri wa katiba na sheria Dkt Harrson Mwakyembe aandae na kupeleka miswada ya marekebisho katika sheria mbili zinazo ongoza mchakato wa katiba mpya.



WhatsApp-Image-2017-03-18-at-02.51.34-1-660x400.jpeg

 
Mkuu Deo kibamba nilikuwa nakukubali Sana wakati wa vugu vugu la kina Dr Uli mboka na kuchukua maoni ya katiba, ila baada ya Yale mabadiliko waliyoyafanya Lumumba kwa kuikamua utamu wote katiba ya warioba na jukwaa la katiba kukaa kimya ,imani yangu kwenu ilipotea kabisa.

Lakini why muibuke this time after TLS election 2017...??? It seems that there is something hidden in between you & TLS , mark my bitter words wazee wa jukwaani la katiba.
 
Mchakato wa katiba haukusimama ispokuwa umevurugwa hivyo ni kurudishwa pale ulipo vurugwa na kupatikana ile katiba ya wananchi na sio ya ccm chenge na Samuel sitta
 
Sina imani na hawa jamaa wanajiita Jukwaa la katiba kwani mapambano ya kuunda katiba mpya yalipopamba moto na kuvurugwa na bunge maalum la katiba lililoongozwa na ccm wao walikaa kimya wakiongozwa na huyu jamaa aitwaye Deus Kibamba.Hivyo kwakuwa wakati mapambano yamekolea kati ya wanaotaka muundo mpya ktk katiba na wanaotaka muundo wa zamani uendelee kwa kifanyiwa maboresho kidogo tu wao jukwaa la katiba walirudi nyuma na kuwaacha jamaa wa UKAWA pekeyao.Hivyo ni heri waendelee kukaa kimya kama walivyofanya kipindi kile wakati marehem Sitta akikusanya maoni upya na kuacha ya tume ya Warioba
 
Mkuu Deo kibamba nilikuwa nakukubali Sana wakati wa vugu vugu la kina Dr Uli mboka na kuchukua maoni ya katiba, ila baada ya Yale mabadiliko waliyoyafanya Lumumba kwa kuikamua utamu wote katiba ya warioba na jukwaa la katiba kukaa kimya ,imani yangu kwenu ilipotea kabisa.

Lakini why muibuke this time after TLS election 2017...??? It seems that there is something hidden in between you & TLS , mark my bitter words wazee wa jukwaani la katiba.
Anatimiza wajibu wake na swala hili halihusiani na TLS kabisaa, acha swaga zako.
 
Huu ndo uzi wa kwanza wa MAANA wiki mwezi mzima huu.
Nipo pamoja nanyi ila kwa rasimu ya Warioba.
Uzi waweza kuwa na maana, lakini Jukwaa la Katiba hawana maana. Wanamwomba Magufuli waonane naye kwa lipi? Wao nilitegemea wafanye makongamano, na hata ikiwezekana waitishe maandamano ya wananchi kudai suala la katiba kushughulikiwa. Au wakafungue mahakamani kesi za kikatiba kama shinikizo kwa mamlaka kushughulikia suala hilo. Unapoomba kwenda kuonana na Rais, kwanza unampa nafasi ya kuamua kukuruhusu au kutokuruhusu. Hivi jukwaa la katiba wanamwona Magufuli ni wa kuwasikiliza? Hamasisheni wananchi waamke wenyewe. Kupigwa marufuku mikutano ya kisiasa alikuwa na maana ya kuzuia vyama vya siasa kuhamisisha wananchi juu ya mambo kama haya.
Wanataka wakauombe mtu wampunguze madaraka
 
Back
Top Bottom