Jukwaa la Katiba latangaza Maandamano ya amani nchi nzima

Jeshi la polisi limeyapiga marufuku maandamano hayo ya katiba Said Mwema amema hana nia mbaya ila ni kwa usalama wa Wananchi
 
mbona nchi yeneyewe haina usalama!??
sielewi wanaposema ni hatari kwa usalama wa nchi!!
 
Mmmh! Nawashauri mtulize joto - tafuteni feni pahali mkae mjipulizie au kama hakuna feni, pale mlimani tafuteni mahali pazuri penye upepo mkae ili mshushe presha yenu. Hii ajenda mnayoileta sidhani kama ni ya kwenu itakuwa imeingiliwa na usalama wa taifa kwa lengo lao. Wawachemshe muandamane halafu CCM ipate ajenda. kwa sasa nashauri tusubiri hiyo mikutano ya ikulu na vyama ndo mwelekeo ujulikane.
 
Jeshi la polisi limeyapiga marufuku maandamano hayo ya katiba Said Mwema amema hana nia mbaya ila ni kwa usalama wa Wananchi

Said mwema kwa makusudi na bila uhalali anapora haki za wananchi. Huyu lazima kuna siku atasimama kizimbani kwa kosa la mauaji ya wananchi wasio na hatia huko Arusha.
 
heheheheeeee miafrika tena ya kitz utaionea hurumu mikwara kibao.. maoni deus kibamba ale kichapo na mtu yeyote atakae jidai anataka maandamano aandamane mwenyewe.. tumechoka na hizi kelele zisizokuwa na maana wakati watz tayari washakufa ni kazi bure..
 
MUUNGANO wa Asasi za kiraia zinazounda Jukwaa la Katiba hapa nchini, umesema mpango wa maandamano yasiyo na kikomo kupinga muswada wa mabadiliko ya katiba kusomwa kwa mara ya pili uko palepale na sasa wanatarajia kutoa utaratibu wa kutimiza adhima hiyo kesho.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba alisema kikao cha Kamati Tendaji kilichokaa juzi kilibariki maazimio yote yaliyokwishatangazwa awali na kusitiza kuwa kesho kitatangaza hatua za utekelezaji wake.

“Kamati tendaji iliyokutana jana (juzi) ilijadili kwa kina hutoba zote za viongozi, ile ya Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na ya kambi ya upinzani bungeni,” alisema Kibamba na kuongeza;


“Baada ya kupitia yote hayo kamati hiyo ilibariki maazimio yote yaliyokwishatangazwa hivi karibuni kupitia vyombo vya habari na siku ya Jumanne (kesho) tutatoa tamkoa litakalohusu utaratibu utakaotumika kutekeleza adhima hiyo,” alisema Kibamba.

Novemba 14 mwaka huu, jukwaa hilo liliitisha kongomano la Katiba jijini Dar es Salaam na kuelezea adhima yake ya kuitisha maandamano nchi nzima endapo Serikali ingepeleka muswada huo kusomwa kwa mara ya pili bungeni.

Pia likatumia fursa hiyo kuonya wabunge ambao wangeunga mkono na kupitishwa muswada huo uliosomwa kwa mara pili kuwa lingetangaza majina yao haradharani kama wasaliti wa wananchi waliowachagua.

Source: Mwananchi

Haraka sana tunahitaji hayo majina ya mibunge hovyo na michango waliyochangia bungeni kutusaliti.
Tutayapublish pote!!! tunapoweza kufika! hasa jimboni kwao. Plain stupidity!!!!!!!
 
Back
Top Bottom