Jukwaa la Katiba lamtaka Rais Magufuli kuanzisha mchakato wa kupatikana Katiba Mpya

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,409
20,759
Jukwaa la katiba nchini limempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa juhudu zake kubwa anazozifanya kuirejesha nchi katika sehemu inayostahili na hivyo ina imani kuwa hayo yote yataweza kuwa katika mfumo sahihi kama kutakuwepo na katiba imara hivyo wamemuomba kuanza mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya ili kukamilisha kazi nzuri ambayo ameinza ya kulikomboa taifa.

Hayo yamesemwa na mjumbe wa jukwaa hilo Bw. Hebron Mwakagenda wakati akisoma tamkoa kwa umma na kuzindua kitabu kinachoelezea mwelekeo wa katiba mpya kikiangazia uliponzia, ulipo na unakoelekea.

Chanzo: ITV
 
Ataanzisha vipi mchakato wa katiba mpya ilhali haikuwa kwenye ajenda zake? Kwa sasa anainyoosha kwanza nchi. Katiba mpya tutaanza kuijadili mwaka 2024
 
Jamaa alisha sema kuwa katiba siyo priority yake. Tusisahau kuwa hii ni Tanzania "yake" na yeye ndo anayejua kipi kizuri kwa Tanzania; wengine tutafuata tu! Hayo ndo matunda ya democracia ya tanzania!
 
Mbona ameishasema kuwa katiba anaiweka pembeni kwa sasa ananyoosha nchi, na akaongezea kuwa muhimili wa Serikali yake ukiuangalia vizuri utaona umezama kwenda chini zaidi ya mihimili mingine kwa sababu ndiyo muhimili wenye kutafuta, kutunza na kutoa fedha
 
Ataanzisha vipi mchakato wa katiba mpya ilhali haikuwa kwenye ajenda zake? Kwa sasa anainyoosha kwanza nchi. Katiba mpya tutaanza kuijadili mwaka 2024
Ni kuiboresha iliyopo mapungufu yake inatosha
 
Ataanzisha vipi mchakato wa katiba mpya ilhali haikuwa kwenye ajenda zake? Kwa sasa anainyoosha kwanza nchi. Katiba mpya tutaanza kuijadili mwaka 2024
Bila ya katiba bora inainyoosha vipi nchi?
 
HV hamjui kama ukubwa mtamu?abadilishe katba itakayomsulubu Mwenyew tusahau by kashasema hana mpango huo
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom