Jukwaa la katiba kuunguruma Saut jumamosi

Alfu Lela Ulela

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,255
75
Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha St. Augustine Mwanza (SAUTSO) kwa kushirikiana na Asasi ya National Social Transformational (NASOT) wameandaa kongamano kubwa la Katiba jumamosi ijayo (tar.08/12/2012) ambalo limejikita zaidi katika kupima utendaji wa serikali za mitaa na uwezo wake kikatiba.

Akizungumza na waandishi wa habari alipofanya nao mkutano jana, Rais wa serikali ya wanafunzi (SAUTSO) Bw.Malisa Godlisten alisema dhamira kuu ni kupima utendaji wa serikali za mitaa na kuzikumbusha wajibu wake katika jamii.

"Watu wengi wanajadili Katiba kwa kujikita zaidi katika serikali kuu. Wengi wanajadili mamlaka ya Rais, mambo ya Muungano, Uteuzi wa bara za la mawaziri na kudhani hayo ndio mambo pekee yanayogusa maisha yao ya kila siku. Wanasahau kuwa serikali za mitaa zina nafasi pia katika maisha yao na bila kuwepo mfumo mzuri wa uongozi, wananchi wengi wataendelea kuteseka kwa maamuzi yafanywayo kwenye ngazi za chini za serikali za mitaa."

Alisema Malisa akijibu swali la Mwandishi wa MWANANCHI Bi.Zulpha Musa. Kongamano hilo litahutubiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw.Deus Kibamba, Mkurugenzi wa kituo cha taaluma SAUT, Dr.Isack Safari na wageni wengine mashuhuri. Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali mjini Mwanza wamealikwa kuhudhuria Kongamano hilo wakiwemo wanafunzi wa chuo kikuu SAUT, Chuo cha Biashara CBE, Chuo kikuu cha Sayansi ya tiba Bugando, Chuo cha Mipango na chuo cha Uvuvi Nyegezi.

Licha ya Kongamano hilo kuhudhuriwa na wanafunzi pia watakuwepo wanataaluma wa kada mbalimbali, waandishi wa habari, viongozi wa serikali na wananchi kwa ujumla. Malisa ametoa wito kwa wanajamii wote kujitokeza kwa wingi ili kutoa maoni yao kwa uhuru na uwazi kwani nafasi kama hiyo inaweza isipatikane tena karibuni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom