EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba alisema kikao cha Kamati Tendaji kilichokaa juzi kilibariki maazimio yote yaliyokwishatangazwa awali na kusitiza kuwa kesho kitatangaza hatua za utekelezaji wake.
Kamati tendaji iliyokutana jana (juzi) ilijadili kwa kina hutoba zote za viongozi, ile ya Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na ya kambi ya upinzani bungeni, alisema Kibamba na kuongeza;Baada ya kupitia yote hayo kamati hiyo ilibariki maazimio yote yaliyokwishatangazwa hivi karibuni kupitia vyombo vya habari na siku ya Jumanne (kesho) tutatoa tamko litakalohusu utaratibu utakaotumika kutekeleza adhima hiyo, alisema Kibamba.
Novemba 14 mwaka huu, jukwaa hilo liliitisha kongomano la Katiba jijini Dar es Salaam na kuelezea adhima yake ya kuitisha maandamano nchi nzima endapo Serikali ingepeleka muswada huo kusomwa kwa mara ya pili bungeni.
Pia likatumia fursa hiyo kuonya wabunge ambao wangeunga mkono na kupitishwa muswada huo uliosomwa kwa mara pili kuwa lingetangaza majina yao haradharani kama wasaliti wa wananchi waliowachagua.