Jukwaa la Katiba (JUKATA) kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza kurejeshwa mchakato wa katiba mpya

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Dodoma. Jukwaa la Katiba Nchini (Jukata) limeandaa maandamano ya amani ya kutaka kurejeshwa kwa mchakato wa Katiba Mpya.

Akizungumza leo Jumanne mara baada ya mkutano mkuu wa jukwaa hilo wa siku mbili ambao umeshirikisha mashirika yasaiyo ya kiserikali 184 nchini.

Meneja Programu wa Jukata, Machereli Machumbana amesema maandamano hayo katika ngazi ya kitaifa yanatarajiwa kupokelewa na Rais John Magufuli.

Amesema wamekubalina kufanya maandamano nchi nzima kuunga jitihada za Rais Magufuli katika harakati za kurejesha ari na heshima ya utumishi wa umma nchini ikiwa ni pamoja na jitihada zake za kupamba na rushwa, nidhamu na kulinda raslimali za Taifa ikiwemo madini.

“Katika pendekezo hili kutakuwa na ujumbe kuhusu Katiba Mpya na kwenye maandamano haya tumepanga Rais Magufuli ndiye awe anayapokea maandamano ya kitaifa kuhusu kumpongeza yeye na kumuomba akamilishe

mchakato wa Katiba ili jitihada zake ziwe na msingi, nguvu za kisheria kwa yote anayafanya,” amesema.

Amesema bila msingi wa kisheria jitihada zake hazitakuwa za kudumu na wao wanataka waweke misingi imara hata akitoka yeye akaja mwingine atabaki katika historia alinyoosha nchi na kuleta Katiba Mpya.

Pia amesema jukwaa hilo limekuwa na kawaida ya kuandika barua kukutana na viongozi wa kitaifa na kwamba wameandika barua kadhaa kwenda Rais Magufuli kujadiliana na kupata ushauri kutoka kwake kuhusu mchakato huo.

Chanzo: Mwananchi
 
hawa tutapiga mabomu hadi watafarakana, sisi hatujaribiwi ujinga huu
 
Hii isijekuwa usanii na maigizo ya kutaka kutuletea katiba ilotoka bungeni, ile sio katiba ya wananchi ni katiba ya CCM.

Hapa tunataka katiba ya Warioba ambayo ndio maoni na makubaliano rasmi baina ya wananchi na taasisi inayoongoza Serikali.
 
Mlitaka katiba mpya.
Mnapewa taarifa ya mikakati hio
Mara imekua mnataka katiba ya warioba
Hata hawajafanyia marekebisho hio KATIBA yenyewe mmeshajiwahi hatutaki katiba ya CCM
NDIO MAANA KILA LEO NASEMA HII NCHI KUENDESHA KISTAARABU NA KWA HESHIMA IMESHAPITWA NA WAKATI
INATAKIWA TUENDESHWE KI MZOBE MZOBE TU..NA KI UNDAVA UNDAVA NDIO TUTANYOOKA,,
Hakuna kucheka na Mtu
Faida Tutaiona Mbele
Hata zamani shuleni nikipewa viboko 7 namlaaani haasa mwalimu nailaani shule masomo pamoja na wazazi kisa nlivochapwa
Leo nawashkuru walimu wazazi kwa kunisomesha kwasbb nimepata Ajira nzuri kutokana na Elimu yangu
 
Hapa naunga mkono. Wengine wanapambana na anayofanya, badala ya kupambana na sababu za kukandamizwa.

Tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Mengine ya kisiasa ni yao.
 
Sijui itakuaje na mheshimiwa alishasema katiba sio kipaumbele chake na hakutamka hayo mambo wakati wa kampeni.
 
Katiba mpya itakuwaje isijekuwa ni ile ya raisi kukaa madarakani miaka yote duniani hapa nina shaka kidogo ndani yake
 
Hatuna bunge la kuleta katiba kama ile ya warioba. Bora tuvumilie huku tukisubiri wabunge wa CCM akili ziwakae sawa.
 
Kama katiba mpya kupatikana mpaka impendezee rais, basi tusahau hakuna katiba hapo.
 
Tunataka katiba ya warioba na si vinginevyo
Warioba ni mteule wa rais katika nafasi ya mkuu wa chuo cha sokoine,na polepole ni katibu mwenezi ccm taifa

Kwa jinsi binadamu walivyo wanafiki,sitashangaa Polepole,warioba na butiku wakaanza kuipinga katiba yao iliyowafanya mpaka wakapigwa mateke na bashite
 
Sawa ila alishasema katiba sio kipaumbele chake,

Yeye alikuja kunyoosha nchi

WATU WAKO WAPI …… WAPUMBAVU SANA.
 
TUNATAKA KATIBA YA WARIOBA AMBAYO NI MAWAZO YA WANANCHI. HATUTAKI KATIBA ILIYOTUNGWA NA KUSIMAMIWA NA MZEE WA KIJISENTI.
JPM ONESHA UZALENDO WAKO KWENYE HILI.
TUNAKUTEGEMEA SANA.
YES YOU CAN
 
Hii isijekuwa usanii na maigizo ya kutaka kutuletea katiba ilotoka bungeni, ile sio katiba ya wananchi ni katiba ya CCM.
kiukweli pamoja na mambo yote ni bora kuikubali ile katiba ya Sitta .at least inakupa machache
katika mazingira ya sasa ambayo opposition ni minority bungeni.Usitegemee kupata chochote utakacho.So you take what you get.
 
Hivi katiba mpya mpaka impendezee rais? Kama ndo hivyo basi tuisahau na kama ikipatikana haitakidhi matakwa ya taifa.
 
Back
Top Bottom