Jukwaa la DINI limefunguliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jukwaa la DINI limefunguliwa

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mkanya, Oct 10, 2008.

 1. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zenu,
  Nasikitika kuwa kuna baadhi ya watu humu ambao ni wapenzi wa jukwaa la DINI kwamba hawajui kuwa ili jukwaa limerudishwa na limefanyiwa marekebisho hii inamaana kwamba unaomba ruhusa kwa mod naye atakuruhusu ili uweze kusoma nakuchangia elimu kuhusu dini nawe pia unaweza kupata elimu katika jukwaa hili la dini.
  Hii nimeigundua juzi baada ya kuwasiliana na jamaa mmoja kwasimu akaniambia kuwa jukwaa hili lilisha fungwa.
  Hivyo basi nawaombeni muwe na moyo wakuelimishana kuhusu masuala ya imani maana kila kitu kina mwisho kama ilivyo kwa huu huai tulionao itafika kipindi hatutakuwa nao tena na tutasimama ili kueleza tulicho fanya kwakipindichote cha maisha yetu hapa duniani.
  Nawakaribisha woote katika jukwaa la DINI kwa wale wanaopenda mambo ya imani maana sio wote wanao penda ila ukweli ni kwamba hili jukwaa ni zuri mno nasema hivyo kwasababu lina mada nzuri za kuelimisha na pia kama unaswali utajibiwa.

  Hatuna Ubaguzi tunawakaribisha Wasabato,Wahindu,Budha,Waislam,Wapagani walokole,Suni,wayehova,Rasta,Othodox na Wa-Masalia wasabato

  Dini zote mnakaribishwa,
  Na ubarikiwe.
   
 2. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Nikitaka kuingia huko nifanyeje? Na nimwambieje huyo mhusika ili na mimi aniruhusu?
   
 3. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu Mkanya, asante kwa taarifa.
  Naomba kujua hayo marekebisho lililofanyiwa hili jukwaa la Dini ni yapi?
  Naomba pia kujua kwa nini Jukwaa la Dini lisiwe huru kama Jukwaa la Siasa na mengineyo, ambayo yeyote anaweza kusoma/kuingia hata kama sio 'member'.
   
 4. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Chakufanya muandikie Invisible Robot umwambie naomba niweze kuliona na kuingia jukwaa la Dini.

  Jamani sisi tuna enjoy sana huku.
   
 5. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekujibu hapohapo kwenye quote,Karibu sana.
   
 6. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Mkuu, nilimtumia message Invisible Robot Jumamosi nikimwomba anielekeze namna ya ku'access' jukwaa la dini lakini naona hakuhangaika kunijibu!
   
 7. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jaribu kumwandikia tena maana wakati mwingine jamaa anakuwa busy sana ngoja na mimi ni m-pm kuhusu issue yako. Karibu sana kwenye jukwaa la manufaa.
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Walipokuwa wanataka kurekebisha walitutaka ushauri. Ila Hawakushughulika na huo ushauri tulio jaribu kutoa. Na hili la kulifungia hawakufata ushauri wetu. Tunashindwa kuelewa wanacho kiogopa ni kitu gani.

  Kwanini tuombe access kutoka kwa moderator? Naingiwa na mashaka, may be kuna kitu wanakiogopa au hawataki wasio wanachama wasome yale yanayo andikwa mule.
   
 9. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ingependeza kama mods wangelifanya kuwa la 'members only' ili kila member ambaye anataka kuingia aingie bila masharti. Hili la kuomba kwa mods mie linanijia kuwa kama yale 'mambo ya kikubwa'. Mambo ya kikubwa ni sawa uombe ruhusa, lakini hili jukwaa la kidini mie naona sio.
  Asanteni.
   
 10. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135


  Kweli inawezekana labda Mod afikilie ili jambo.Lakini jukwaa ukweli ni kwamba ni zuri kwelikweli.
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwanini lisewe free au huru kwa kila mtu anaye tembelea humu JF kama mwanzo? Huku ni kulazimishana kila mtu awe mwanachama, wengine hawana muda wa kujiunga. Wanacho taka ni ksoma kilichomo tu basi. Ila kama mtu anataka kutoa mawazo yake au kuchangia hapo ndipo itamlazimu kujiunga na uwanachama.

  Mimi sikubaliani na hili la kuomba ruhusa. Nahisi ni kuwanyima haki wale wote wanao temebelea hapa JF, aidha ukiwa mwanachama au la.

  Nataka kujuwa wanacho kiogopa ni kitu gani!?
   
 12. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mimi naona ni utaratibu watu wamejiwekea maana kuna watu wanaopenda na kuna watu walio amua kujitoa kafara hawapendi mambo ya dini.
  mm naamini kuwa watu kama wanania ya kuingia jukwaa la dini wataingia tu ila kama mtu hataki basi maana nilivyo ona ni kwamba watu wameongezeka mno ktk ilo jukwaa.
   
 13. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  wenye nia ya kuingia kwenye jukwaa la dini wataingia tu.Ur welcome jukwaa la DINI ZOTE
   
 14. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Sioni kwa nini jukwaa la dini liwe na kibali maalum toka kwa mods wakati member anataka kufaidi kilichomo na kuchangia pale inapobidi. After all Tanzania naamini dini haijawa issue kubwa japo wengine wanataka kuifanya kuwa issue kwa wakati huu.

  Ukweli ni kwamba dini inatueleza misimamo au mapokea ya wale waanzilishi wa dini hizo. However, suala la kumwamini Mungu na namna ambavyo mwanadmau anataka aishi ampendeze Mungu ni personal. Dini haimfikishi mtu kwa Mungu bali matendo yako ndiyo yatakupeleka mbele za mola au ibilisi.

  Please, acha jukwa la dini liwe accessible to JF members.
   
 15. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #15
  Oct 20, 2008
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Maane,

  Ukiangalia utaona kuwa Jukwaa la dini limesheheni mihadhara badala ya elimu tunayoitaka kwa jamii yetu. Lawama zilikuwa nyingi huku wadau wakitaka jukwaa hilo liondoshwe kabisa kwani walidai ni chanzo cha migongano ya kidini.

  Labda tungepeana namna za kuliendesha jukwaa hilo ingesaidia. Binafsi niliwashauri Mods walipe access maalum kwa wale wanaopenda mijadala hiyo kwani inaonekana kabisa badala ya kuwa watu kueleweshana masuala ya kiimani wamehamia kwenye kujadili UISLAM vs UKRISTO kitu ambacho wakati tunaanzisha jukwaa hilo halikuwa lengo letu.

  Daima mijadala ya kidini hupelekea watu kuingia kwenye chuki, hili halikuwa lengo letu hata kidogo.

  Nini kifanyike?
   
 16. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Liwekeni wazi watu wajiachia na misahafu na rozari.Atakayeleta fujo si sheria zipo ndio maana ya sheria kuwepo.
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Maane;
  Kwa angalizo tu, ni kwamba si kweli kwamba matendo ndiyo yatamuingiza mtu mbinguni. Maandiko yananiambia ni pale mtu anapomuamini Yesu kama mwokozi wa maisha yake. Yohana 3:16-19; Waefeso 2:8-9
   
 18. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  YOYO, hapo mwanzo sheria zilikuwepo watu wakazivunja ma-mod wakatoa angalizo ila bado mambo yaliendelea mm naona kama watu wakitambua kuwa kila mtu anamaoni yake hawatapata shida wahusika wajukwaa hili wao hawana matatizo hata ikitokea impact kubwa huwa wanafikia muafaka.
  Binafsi sijui lifanyweje!
   
Loading...