Jukwaa la Celebrity kwa sasa limevurugwa na watu hawa

Mwanzo jukwaa hili lilikuwa lina vitu vitamu vinavyohusu ma celebrity wetu na muziki wao kiujumla huku wanajamvi wakigusia pande zote kuhusu muziki wetu na lilinoga sana.

Ila majuzi hapa jamvini wamekuja chawa rundo humu ndani na kuharibu jukwaa kwa nyuzi za kichawa chawa ,ushabiki maandazi huku wakigeuza jukwaa kuwa Instagram ya umbea umbea. Na uteam bila wao kulipwa hata mia

Wakitoa nyuzi za kukatisha tamaa wasanii wengine wakienda mbali na kuingilia maisha yao binafsi na kuyakejeli. Yaani ukiingia jukwaa hili ni wao wanataka umtaje na kumsifia msanii mmoja tu yaani Diamond Platinumz.

Kwa mtindo huu tutasogeza mziki wetu mbele vipi? Maana hata Diamond mwenyewe anajitahid kuusogeza muziki mbele ila chawa wake ndo mnamuangusha.

Badilikeni tuongelee muziki wa wasanii na sio kupambanisha wasanii.
Celebrity sio wanamuziki tuu
 
Bro kumbe bado tu Yale ya siku ile yalikuchomaa hahaha
Hizi ni I'd tu hapa zinaficha mengi sana.
Haya sio maisha yangu maana naona unaanza kugusa maisha yangu binafsi
Mbona Mimi sijakugsa yako?

Yaani kumbe bado una makasiriko na Mimi
Hahhahah watu tuna familia kabisa ila hapa tuna act tu kazi yangu ndo hiyo na inanilipa am smart enough ndo maana wameniamini
Haya basi mkuu, nimekubali kuwa una miliki media hapa tz 😂
 
Hujaelewa na labda tu niambie hiyo team yangu unayosema ni IPI?
Ungejua kazi yangu wala usingeniletea uchawa hapa ..

Mbona sasa wewe huwa unataka mawazo yako yafanane na kila mtu? Mtu akipinga unasema chuki..

Badilika dogo kuna maisha baada ya uchawa

Hii ni kweli

Sijui huyu innocent dependent ana jambo gani na Diamond...huwezi kumkosoa akakuelewa,lazima aone ni chuki/wivu
 
Hapana usimponde lakini wanaomkosoa usichukulie kama chuki....Diamond ni binadamu kama binadamu wengine kuna mambo anakosea
Yeah ukimkosoa mtu unamjenga
Sema tatizo ni kwamba ma fans wa Mond na wasanii hawapendi msanii wao pendwa akosolewe wanafeel bad
 
Vyovyote vile atavyosema haina shida

Yeye Diamond ni nani asiambiwe bhana
Subiri watakushambulia sana kwake inno diamond ni mkamilifu hajawahi kukosea ni Mungu wake
Huu ujinga sijui wataacha lin sometime unaongea kitu cha kawaida tu ila
Unaulizwa "hivi chuki kwa diamond utaacha lini"?
 
Back
Top Bottom