Andrew Kadege
Member
- Jan 1, 2016
- 6
- 5
JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMKO LA KUUNGA MKONO UAMUZI WA SERIKALI KUHAMIA DODOMA
Ndugu waandishi wa habari, Jukwaa limewaita mahali hapa kuunga mkono na kumpongeza Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kihistoria wa kutangaza Serikali kuhamia Dodoma.
Uamuzi huo mzito ni kutimiza ndoto ya kizlendo na kiu kubwa si tu ya muasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa, Mwalimu J. K Nyerere bali shauku ya Watanzania wengi tuliokuwa tunasubiri jambo hili kutimia.
Ndugu waandishi wa habari, mtakumbuka kuwa suala la kuhamia Dodoma lilibaki kiporo tangu Rais wa Awamu ya Kwanza hivyo kwa uamuzi huu wa kuhamia Dodoma ni kututhibitishia kuwa Rais Magufuli ni mtu wa vitendo na siku zote anatazama maendeleo na si siasa.
Kwa kasi hii sisi tunachukua fursa hii kumpa pongezi na kumtia moyo aendelee hivyo hivyo kutufanya wananchi wake kuwa na matarijio makubwa sana katika kutekeleza ahadi zake nyingi na kuivusha nchi.
Ndugu Wana habari,tunasisitiza tena na kama alivyoass pia Mzee wetu Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi mjini Dodoma, kwa kiongozi kama huyu, Watanzania wenzangu hatuna chaguo lingine zaidi ya kumuunga mkono na kumsaidia afikie dira yake.
Pia Jukwaa tunampongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuonesha njia na utekelezaji wa haraka wa Agizo la Rais kwa kuagiza mawaziri kuhamia Dodoma haraka.
Tunamalizia kwa kusisitiza kwa watanzania wenzetu kwamba kwa kasi na nia njema hii ya Serikali ya Awamu ya Tano hatuna chaguo lingine muafaka zaidi ya kuungana na viongozi wetu hawa katika safari hii ya mabadiliko.
Ahsanteni sana
Imetolewa leo Dar es Salaam
28/07/2016
Andrew Kadege
0756 911 342
M/kiti wa Jukwaa Huru La Wazalendo Mkoa wa DSM.